CHADEMA, na wapinzani wote kwa ujumla, kila dalili inaonesha nyie ni zaidi, mshindani wenu Mkuu CCM anaonesha kila dali ya uoga, kutokujiamini na kukata tamaa. Hana uwezo tena, anajishika na kila aina ya tawi mpaka matawi wasanii, matawi malori, matrekta, mabasi, kuhonga nauli bali hayo matawi kamwe hayaoneshi kufua dafu popote. Tawi pekee la kuwatisheni CHADEMA ni ile kauli ya mshindani wenu mkuu kuwa "nimekupa cheo mshahara mzuri halafu umtangaze mpinzani?! utanitambua"
CHADEMA ni Hiyo kauli pekee tu ndiyo ya kuishughulikia kwa sasa. Pangeni vizuri ishu za mawakala wenu, zichambueni vilivyo teknikalitizi za ujanja ujanja na wizi wa kura, tumieni kila mbinu halali ndani na hata nje ya nchi, msianzishe fujo lakini kamwe kamwe asilani msikubali tena kugeuza shavu la pili, msikubali tena kumwachia Mungu, watayarisheni vilivyo wapiga kura wote Bara na Visiwani, hata wanaccm ambao dalili zinaonesha wengi wao watakupigieni kura kisirisiri, wajiandae kukataa kura zao kuchakachuliwa na Tume isiyo huru ya uchaguzi. CHADEMA mkiweza hilo historia mpya inakwenda kuandikwa tarehe 24 Oktoba 2020.
Washirikisheni wananchi wote wa Tanzania na Pambaneni mpaka tone la mwisho. Wananchi wa Tanzania wapo nyuma yenu, nyinyi pamoja na ACT Wazalendo (kwa upande wa Zanzibar) ndo tegemeo letu pekee wana wa nchi hii lililobaki, tarehe 24 oktoba ni nafasi ya dhahabu (golden chance), itumieni vema.
Mungu ni mwema Wanamageuzi, kuna kila dalili nchi Itakombolewa Oktoba mwaka 2020.
Kama ni ndoto, basi ni nzuri na lazima ifanyiwe kazi kweli kweli. Tukipunguza nguvu huku kwetu Kilimanjaro imeenda, na bahati mbaya wananchi wamekwisha enda kibra.
Sasa hivi Mbowe ana kazi kubwa sana kuwa shawishi wapiga kura na wala sio wanasiasa. Wananchi hawatutaki zaidi ya nusu wamekwenda CCM na idadi ya wanao ondoka inaongezeka kila siku.
Wana chadema,ofisi na uongozi karibu wa kata zote wameenda CCM, Madiwani na uongozi wa kata zote za wilaya ya Hai walikuwa Chadema wameenda CCM, na zaidi ya hayo Madiwani wote wa kata zote waliojuizuru Chadema kwenda CCM wamewarudisha kugombea katika kata hizo hizo.
Mmachame anaheshimu sana Elimu na Utajiri, cha ajabu wasomi karibu wote wamerudi CCM na matajiri ndio wanaoifanyia kampeni na kugharamia uchaguzi wa CCM.
Nipo Kata ya Uswaa, Machame, Hai:
Tumeshinda nae na kalala hapa Uswaa, Waziri wa zamani Mama Rita Mlaki, Mzaliwa wa Machame Kusini, na katembelea karibu nyumba zote na akiwa na kundi la vijana wa Chadema akieneza Injili ya CCM.
Wanasema Vijana hawana kazi-- sababu Mbowe, Hawana chakula majumbani --- sababu Mbowe, wanakunywa pombe ya Banana- -imeileta Mbowe ili wawe mazuzu yeye anapiga pesa.
Wanasema umasikini na shida zote Hai ameleta Mbowe na kwa Upoyoyo wao wanakubali na ndio kinacho semwa, Sokoni, Hospitali, Kwenye vikao vya mbege, kwenye mabasi, bodaboda na hasa baada ya kushuka neema Siha, sasa hivi Siha ndio wenye hali nzuri kimaisha na ndio Halimashauri inayoongoza Mkoa wa Kilimanjaro, huduma za wenzetu ni bora kwa sababu wameenda CCM. Na kwa bahati Mbaya wana Siha ni Wamachame.