Elections 2010 Chadema mnafanya makosa kutomtumia Zitto katika kampeni

Elections 2010 Chadema mnafanya makosa kutomtumia Zitto katika kampeni

Joined
Jan 16, 2007
Posts
721
Reaction score
178
Nimekua nikifuatilia kampeini za CHADEMA lakini kitu ambacho nimekigundua mpaka sasa CHADEMA inafanya kampeini zake na Zitto anafanya kampaini kivyakevyake ZITTO NI CHACHU CHADEMA TUITUMIE MUNGU IBARIKI TANZANIA.
 
Kwani kazi anayoifanya kanda ya magharibi ni ndogo, viongozi wa Chadema wamegawana kanda za kampeni. Viongozi wote hawafuatani na mgombea urais atawakuta kwenye kanda zao, kitu ambacho ni kizuri kila sehemu iwe active wakati wote wa kampeni.
 
tatizo chadema ni chama chenye mpangilio mbovu, hata hivyo humuoni katika kampeni zipi?
 
ongezea hapo zitto haivi chungu kimoja na Dr slaa
 
tatizo chadema ni chama chenye mpangilio mbovu, hata hivyo humuoni katika kampeni zipi?

inatia kinyaa pale mafisadi wa ccm wanavyojaribu kutoa ushauri kwa chadema (as if wanaitakia chadema mema).
 
ongezea hapo zitto haivi chungu kimoja na Dr slaa

Mkuu umepiga tapu tapu nini leo! Zitto leo amefungua Kampeni rasmi huko Bukombe akimnadi Mgombea wa CHADEMA Prof Kahigi!
 
Mkuu umepiga tapu tapu nini leo! Zitto leo amefungua Kamapeni rasmi huko Bukombe akimnadi Mgombea wa CHADEMA Prof Kahigi!

Mchungaji achana na huyo jamaa anaropoka tu. Juzi kazindua kampeni nyingine Kigoma Mjini, na nyingine kule mitaa ya Kasulu. Sasa ni kampeni zipi ambazo wanasema hashiriki?
 
ongezea hapo zitto haivi chungu kimoja na Dr slaa

Kama haivi chungu kimoja na Dr. Slaa, Zitto angekuwa anaomba kura kwa ajili ya Dr. Slaa? Acha kupanda mbegu za chuki.
 
Mkuu umepiga tapu tapu nini leo! Zitto leo amefungua Kamapeni rasmi huko Bukombe akimnadi Mgombea wa CHADEMA Prof Kahigi!
Watu wa type ya kina paulss wanaorukia ku-argue bila data ni wa kuwaacha hajui leo Zitto yuko wapi na anafanya nini mradi kaona neno Zitto basi atatapika anavyojua yeye hata kama ni ushabiki but it is too low.
 
sijaelewa kumtumia vipi wakati anaipigia kampeni Chadema Kigoma na wagombea wengine na siku za kampeni bado zipo mbele.. nadhani kutokana na uwezo walio nao ni vizuri kuweka nguvu pale wanapoweza. Kwa mfano Zitto akifanikiwa kunyakua viti zaidi vya Chadema Kigoma atakuwa ametoa msaada mkubwa sana.. na kwa kadiri kampeni inavyoendelea nina uhakika tutaona confluence of talent ikija pamoja kuelekea kuwashtua CCM.. majemedari wote mkiwa eneo moja la mapambano mtaacha sehemu moja inapwaya.. ndio maana Petreaus yuko Afghanistani, wengine wako Iraq, wengine wako Pentagon...
 
Kama haivi chungu kimoja na Dr. Slaa, Zitto angekuwa anaomba kura kwa ajili ya Dr. Slaa? Acha kupanda mbegu za chuki.
sio chuki ndugu, ni ukweli ulio wazi hata wewe unajua
Watu wa type ya kina paulss wanaorukia ku-argue bila data ni wa kuwaacha hajui leo Zitto yuko wapi na anafanya nini mradi kaona neno Zitto basi atatapika anavyojua yeye hata kama ni ushabiki but it is too low.
Mkuu yaani tatizo leni mtu akitofautiana na nyinyi basi ni mpuuzi
 
Unafanya makosa makubwa kufikiri kwamba Zitto hatumiki (sio kutumiwa) katika kampeni hizi. Anatumika mno!
 
ongezea hapo zitto haivi chungu kimoja na Dr slaa

Mkuu yaani tatizo leni mtu akitofautiana na nyinyi basi ni mpuuzi
Tofautisha kupingana kwa tofauti za kiitikadi na kukupinga kwa kusema uongo, hapa wewe unasema uongo bila kuwa na data za wapi Zitto yupo. Inawezekana ni upenzi wa kitoto tu unaokusumbua ili uonekane kwa watu na wewe umepinga. Angalia video hii na tembelea link hii Zitto na Demokrasia

Last edited by a moderator:
Unafanya makosa makubwa kufikiri kwamba Zitto hatumiki (sio kutumiwa) katika kampeni hizi. Anatumika mno!

Umenena! Chadema lazima wajue baada ya kujaribu kuuchafua uongozi wa juu wa Chadema kwa tuhuma za ukabila, dini, na ngono, sasa weanahamishiwa katika nafsi za viongozi. Watapenda kuleta vurugu kati ya Mbowe na Slaa, Slaa na ZIto na hatimaye Mnyika na wazee wa chadema.
 
Ni mgawano tuu wa Majukumu, kama vile Mbowe na Ndesaa watakavyo tumika kanda ya Kaskazini, Tindu Lisu Kanda ya kati, Zitto atatumika zaidi Nyanda za Juu Kusini.
 
Nimekua nikifuatilia kampeini za CHADEMA lakini kitu ambacho nimekigundua mpaka sasa CHADEMA inafanya kampeini zake na Zitto anafanya kampaini kivyakevyake ZITTO NI CHACHU CHADEMA TUITUMIE MUNGU IBARIKI TANZANIA.

Tanzania ni nchi kubwa, na makazi yamezagaa, Chadema wanatumia mbinu nzuri kuhakikisha kila mtu anatumia nafasi yake kuhakikisha Kura zinapatikana. Fuatilia Kazi nzuri ya Zitto huko Kigoma, na viongozi wengine kwenye majimbo yao. Kama kila mmoja akipata wapiga kura Million Moja kwa Dr. Slaa, inatosha kabisa kuipa Chadema madaraka ya nchi.

Kikubwa ni kwa Chadema sasa kuimarisha huu mkakati, na kutafuta njia za kulinda Kura!
 
mbona kikwete hatembei na naaape nauye. zitto yupo na anaendelea na majukumu yake kama alivyopangiwa na chama, pia kumbuka jimbo lake ni moja kati ya majimbo ambayo ccm inayataka kwa nguvu zao zote na wameisha tangaza kama ulivyomsikia kinana akiongea, kwa hiyo zito anapambana sana na anatumika sana
 
Back
Top Bottom