Elections 2010 Chadema mnafanya makosa kutomtumia Zitto katika kampeni

Elections 2010 Chadema mnafanya makosa kutomtumia Zitto katika kampeni

tatizo chadema ni chama chenye mpangilio mbovu, hata hivyo humuoni katika kampeni zipi?
VIPI BANA, KWANI MAGUFULI ANAZUNGUKA NA KIKWETE KILA SEHEMU??? Kwenye kampeni ni kama kwenye mechi, sio kila mtu acheze striker...

Nina imani kuna good reason ya zitto kuwa zaidi magharibi na magharibi wanamuhitaji zitto zaidi... kazi anayoifanya ni nzuri sana na slaa pia anafanya kazi nzuri... kumbuka you cant put all eggs in one basket... kwani umemuona mbowe kila sehemu anapozunguka slaa??

Mmeshindwa ya mambo binafsi sasa mnataka kugombanisha chadema, they are smatter than that!!!
 
sijaelewa kumtumia vipi wakati anaipigia kampeni Chadema Kigoma na wagombea wengine na siku za kampeni bado zipo mbele.. nadhani kutokana na uwezo walio nao ni vizuri kuweka nguvu pale wanapoweza. Kwa mfano Zitto akifanikiwa kunyakua viti zaidi vya Chadema Kigoma atakuwa ametoa msaada mkubwa sana.. na kwa kadiri kampeni inavyoendelea nina uhakika tutaona confluence of talent ikija pamoja kuelekea kuwashtua CCM.. majemedari wote mkiwa eneo moja la mapambano mtaacha sehemu moja inapwaya.. ndio maana Petreaus yuko Afghanistani, wengine wako Iraq, wengine wako Pentagon...

AAahhhh MMK umenikumbusha enzi zile za Vita vya Kupambana na Nduli idi amini makamanda wetu akina Mayunga, Musuguri, Twalipo, Walden, Msuya, Kitete nk walivyokuwa wamejipanga vizuri wakati huo (1978-1979) kwa lengo moja tu la kushinda vita na hivyo kumung'oa Nduli Amini. Thanks
 
tatizo chadema ni chama chenye mpangilio mbovu, hata hivyo humuoni katika kampeni zipi?

Yah,mpangilio mzuri ni wa Kikwete na CCM yake kufotokopi ahadi za 2005.

Yani kwa kweli napata shida sana kuelewa kwanini bado kuna watu wenye akili timamu wanaisapoti CCM.Hivi wafanye nini zaidi ya waliyokwishafanya ili mliolala usingizi wa pono muamke?

Napata shida zaidi pale watu wenye upeo japo wa kuingia mtandaoni (and therefore being able to gauge facts and fictions katika utendaji,ufanisi na ahadi za CCM) wanapoendelea kupenda for the sake of kupenda.

Jamani,acheni selfishness.You're possibly WANUFAIKA wa ufisadi wa CCM.Lakini could you guys look beyond your SELF,and think of nduguzo kule vijijini,friends and even family?Kama wewe huathiriwi na ufisadi- whatever the reason-hudhani kuwa unakuwa m-binafsi kwa kutowajali wenzio wengi wanaoathirika?

Anyway,hata Nyerere na freedom fighters wenzake walipopigania uhuru kulikuwapo Waafrika waliotaka mkoloni aendelee kutawala.You-guys who still embrace CCM's tyranical and corrupt rule-are no different.
 
vipi bana, kwani magufuli anazunguka na kikwete kila sehemu??? Kwenye kampeni ni kama kwenye mechi, sio kila mtu acheze striker...

Nina imani kuna good reason ya zitto kuwa zaidi magharibi na magharibi wanamuhitaji zitto zaidi... Kazi anayoifanya ni nzuri sana na slaa pia anafanya kazi nzuri... Kumbuka you cant put all eggs in one basket... Kwani umemuona mbowe kila sehemu anapozunguka slaa??

Mmeshindwa ya mambo binafsi sasa mnataka kugombanisha chadema, they are smatter than that!!!

kaka achana nao hawajuhi kuwa nachezea ngumi zotezote, za huso, chembe, mgongo, mitama yani kila kitu wakija kustuka washahumia!!
 
Mchungaji achana na huyo jamaa anaropoka tu. Juzi kazindua kampeni nyingine Kigoma Mjini, na nyingine kule mitaa ya Kasulu. Sasa ni kampeni zipi ambazo wanasema hashiriki?

cause hazionyweshwi kwenye TV labla labla
 
Kampeni za kuikomboa Tanzania zinafanyika sehemu nyingi kwa wakati mmoja, hivyo wapiganaji wametawanyika sehemu mbalimbali wakiendelea kuwaelimisha watanzania umuhimu wa kupiga kura na kupigia kura wagombea wa Chadema kwa ngazi zote, kwa maana ya Urais (Dr. Slaa), Ubunge na Udiwani.
 
Nimekua nikifuatilia kampeini za CHADEMA lakini kitu ambacho nimekigundua mpaka sasa CHADEMA inafanya kampeini zake na Zitto anafanya kampaini kivyakevyake ZITTO NI CHACHU CHADEMA TUITUMIE MUNGU IBARIKI TANZANIA.
Mkuu unamaanisha hawamtumii kwa sababu chadema ni wadini na wakabila sana! Unamaanisha hata siku za ufunguzi wa kampeni pale jangwani hakuwepo!
 
Labda anataka waongozane na Dr Slaa kijana ata JKT hukenda nini,vita gani iyo mnapiga alongside na amiri Jeshi mkuu lazima mtawanyike ndo mwaweza fanikiwa
 
Ndugu, pia tujue kuwa Zito naye anawajibu wa kukitetea nafasi yake katika jimbo lake,hivyo si rahisi kuandamana na Dr kuzunguka nchi.
Nafikiri kubwa zaidi ni Zitto kuhakikisha wananchi wake pia wanampigia Slaa 31 oct.
 
Kwani kazi anayoifanya kanda ya magharibi ni ndogo, viongozi wa Chadema wamegawana kanda za kampeni. Viongozi wote hawafuatani na mgombea urais atawakuta kwenye kanda zao, kitu ambacho ni kizuri kila sehemu iwe active wakati wote wa kampeni.

Hapo umenena mkuu Zito kaachiwa aongoze mapambano kanda ya ziwa..
 
Back
Top Bottom