Uchaguzi 2020 CHADEMA mnarudia Makosa ya 2015

Umesema kweli kama Spika anawazuga Chadema waendelee na hoja ya kina Silinde wakati CCM wapo chimbo wanaandika Ilani na kufanya upembuzi yakinifu majimboni. Mmeshawatimua kina Silinde mnahangaika nini wakati uchaguzi ni October ni upuuzi,,,.Kajipangeni . Maamuzi ya Spika yanajulikana .Mimi binafsi Napenda Upinzani utoe changamoto hasa ubunge na udiwani ili biashara ya kuunga juhudi isije kurudia lakini Chadema imekuwa dhaifu.
 
Media zipi unasema wakati ccm nichama cha watu wakijijini wasiojuwa kusoma na kuandika. ..hapa Tz hakuna chama chenye watu wajinga kama ccm ...Hata Nyalali hilo miaka ya 1990+
tatizo wewe unakurupuka mno,soma mada basi uelewe,mleta mada kaleta point muhimu sana wewe umeandika pumba.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hawawezi kukuelewa. Kazi kubwa wanayofanya ni kutukana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Vijana hawa wasio na kazi wasio na mbele wala nyuma???? Hili ni bomu ambalo akitokea mtu akawagawia AK 47 moto wake hautazimika leo wala kesho.
uliza wale wa kibiti kiliwapata nini ?walijaribu kushika AK47
tena vijana wa chadema walivyolaini laini wataweza kweli ikiwa hata kutoka kuandamana kulazimisha ruhusa ya mikutano hawawezi ndo wataweza shika silaha?.angalau cuf ya zamani waliweza kusumbua polisi ila bavicha hawawezi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Chadema bado wana mawazo ya kutumia press conference kitu ambacho hakiwasaidii sana. Press conference zinaingiliwa na Vyombo vya dola na hazidumu kwenye mijadala. Chadema ikishindwa dimba la kati itakuja Lia
Press conference mambo.ya kizamani.sana
Wao nia yao ni kushindana na Rais,eti mbowe nae anataka kulihutubia taifa!
Watu wanaweza kumsikiliza haji manara lakini sio Mbowe
 

Chadema viongozi ndio waoga, hawasomi alama za nyakati kibiti wale ni wakulima wasio na hatia ambao mliwadhulumu pikipiki zao na mikaa. sasa Taifa unachukua kundi kubwa kuanzia wavuvi mliochoma nyavu zao, machinga, waendesha bodaboda, watu daladala, mateja, walioufutwa kazi, mliowadhulumu ni wengi mno na hata mliowanyima pension zao, pamoja na askari wasiopanda vyeo na hali duni za kazi zao.
 
jamaa yangu sisi ni watanzania hatuna chuki za kudumu na hii ni asili yetu kabisa.
lowasa alieambiwa na ccm juzi kijinyea leo karudi ccm.
dr slaa aliepigwa na mkewe arusha na akapasuliwa uso leo ni balozi wa serikali hii iliyompiga,
mbongo akishapata ugali akilala akaamka kasahau yoote ya nyuma.
nakuhakikishia hao wavuvi na bodaboda ndio wanachama vindaki ndaki wa ccm wa kufa na kupona na ndo tegemeo kubwa la ushindi wa ccm

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mh vijana wa vyama vingine wanaogopa kubambikiwa kesi za mitandao.

Kwa sasa ni ngumu sana kwa vyama vya siasa nchini Tanzania kwa sababu ccm hawafanyi siasa tena wanapigana an undeclared war inayotumia vyombo vya dola.

Kama kupost picha ya bendera ya vyama vya upinzani ni sababu ya mtu kufunguliwa kesi ya uchochezi huoni kuwa hizo siyo siasa tena ni vita ?

Njia pekee iliyobaki sasa hivi kupambana na ccm ni CIVIL DISOBDIENCE kwa sababu ccm hawatumii tena political platforms kujenga ushawishi wanatumia state apparatus kupambana un armed civilians.

CCM haishindani kwa hoja tena bali inashindana kwa BUNDUKI na hawana hoja tena za kupeleka kwa wananchi sasa hakina namna tena wananchi kitawatawala kwa hata kwa lazima na hiki ndicho kinachotokea.

CCM isingekuwa inatumia mabavu kutawala awamu ya tano isingemaliza hata miaka miwili ikiwa madarakani, this is the most ruthless and incompetent government I have ever seen katika taifa hili toka nizaliwe.


Kama bado tunaamini ccm itatolewa madarakani kwa harakati za facebook na mitandao ya kijamii tunajidanganya sana.

Kuvilaumu vyama vya upinzani katika mazingira hatarishi namna hii ya kufanya siasa ni kukosa maono, mbona wananchi tuko Neutral kwenye situation yenye injustice kiasi hiki ?



Sent using Jamii Forums mobile app
 
CCM wamejipanga kimkakati. Wakati mnahangaika na Magufuli kuwa Chato CCM wanamtuma Mbatia Mbeya Tarime etc Bashiru anaandaa ilani. Chadema watazusha ana korona mbona haonekani.

Wakati mnahangaika na kina Silinde CCM wanapanga watu muhimu wa kuwadhibiti ndani ya Bavicha. Mkikusanyika DSM Makonda anaambiwa awatoe kwenye reli mnaanza kumsema Makonda wiki nzima.

Hamjakaa sawa DC anawapanga wazee kumpinga Mbowe ,ile mnahamaki Mdude kakamatwa. Munaitisha media huku mkijua mtazuiliwa huu ni ujuha. Ukiwaahidi wananchi habari ukashindwa kuitoa unakua umeondoa imani yao kwako hawatakufuatilia tena.

Mbowe anazidiwa na kina Zito kwenye namna ya kuwasilisha taarifa. Na kutengeneza network ya habari.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mazingira "mfu" ya uwanja mpana wa demokrasia yamedidimiza kwa kiwango kikubwa harakati za mageuzi ya siasa na uchumi kwa kipindi hiki
 
CCM walianza kutengeneza ilani ya uchaguzi ujao, siku ile Magufuli alipo apishwa. Tangia hapo wanaendelea kuiboresha mpaka siku ya kampeini zitakapoanza.
Lakini CHADEMA hata siku ya kampeini watakuwa hawajatoa ilani yao. Mtu akidadisi hilo ataambiwa aangalie kwenye website ya chama. Ukifungua website unakutana na manene haya - still under construction!
 
Chadema bwana sikilizeni ushauri makamnda

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Chadema is there to stay. Iko kwenye damu. Hapa nikipost tu taarifa za chadema kwa wiki moja tu IGP, DGIS hawalali kunitafuta.....sleepless night pengine hata kutemwa kazi zao. Hiyo ndiyo nguvu ya chadema.
 
Mbowe si kwamba hajui chama kinapaswa kuwa namna gani .Mbowe anaogopa kuwa na wanachama kwakuwa chama kikiwa na wanachama ipo siku watataka kukiendesha na kukirudisha mikononi mwao.Mbowe anafurahia kuwa na mashabiki na si wanachama.Anajua sifa ya mtu atakaye weza kuwa Katibu mkuu lakini ana hofu ya kuwa na Katibu mkuu mwenye sifa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…