CCM wamejipanga kimkakati. Wakati mnahangaika na Magufuli kuwa Chato CCM wanamtuma Mbatia Mbeya Tarime etc Bashiru anaandaa ilani. Chadema watazusha ana korona mbona haonekani.
Wakati mnahangaika na kina Silinde CCM wanapanga watu muhimu wa kuwadhibiti ndani ya Bavicha. Mkikusanyika DSM Makonda anaambiwa awatoe kwenye reli mnaanza kumsema Makonda wiki nzima.
Hamjakaa sawa DC anawapanga wazee kumpinga Mbowe ,ile mnahamaki Mdude kakamatwa. Munaitisha media huku mkijua mtazuiliwa huu ni ujuha. Ukiwaahidi wananchi habari ukashindwa kuitoa unakua umeondoa imani yao kwako hawatakufuatilia tena.
Mbowe anazidiwa na kina Zito kwenye namna ya kuwasilisha taarifa. Na kutengeneza network ya habari.
Sent using
Jamii Forums mobile app