Chadema msiba wa Salome hawahusu?

Chadema msiba wa Salome hawahusu?

Kila kinachofanyika hapa wao wataendelea kulalamika kwa sababu nia yao ni kuidunisha na kuipondea JF. Walianza kwa maneno mengi tu kuwa imekosa mwelekeo nk bila mafanikio.

Hizi hasira zote na explosion zote hizi zimeanza baada ya mkataba wa Buzwagi kuwekwa hapa. Mambo yakaanza, vioja vikawa vingi kisha wakatulia.

Ilipowekwa mikataba mingine miwili wa Tanesco na Richmonduli ndio wakagundua kuwa JF kuna serious issues zinaendelea kwa hiyo wakatafuta namna ya kuvuruga mambo hapa. Hapo pia wakashindwa.

Hii habari kuwa mikataba zaidi ya madini imevuja ikiwemo ile ya wakati wa JK akiwa madini ndio imewachanganya zaidi na sasa ndio explosions na matusi dhidi ya JF all day long!

Live with it guys, JF is here to stay na mikataba yoooote itawekwa hapa kwa watanzania kuiona kabla haijatafsiriwa kwa kiswahili na kusambazwa bure nchi nzima!
 
na usisahau alikuwa wa kwanza kueneza picha za mauti ya mwenziwe kama njugu, yaani baada kufikiria ubinaadamu katake advantage maimail yanazunguka kwa picha alizopiga zitto

Wengi wetu hapa ni washabiki/wanachama hii approach unayotumia kuwaattack wapinzani sio kabisa, bila wewe nisingejua kuwa kuna picha zinasambazwa kwenye emails. Yani kama ni moto wewe umeongezea kuni au mafuta.
 
Unayosema ni kweli, tangu tuweke mkataba wa Buzwagi na sasa wa Richmond, naona mashambulizi ndiyo yanakuwa makubwa zaidi. Hata hivyo hilo huja na territory. Tungekuwa hatuna maana kama tusingetarajia mawimbi ya mashambulizi yao.

Walianza na email ya "Dr. Slaa", na sasa wanashindwa hata kuficha kucha zao, kwani wamezitoa kuparua mtu yeyote ambaye kwao ni tatizo. Wanataka kumfanya Zitto awe hoja ya msiba wa Mbatia na hivyo kupoteza mwelekeo wa kujadili kiini cha matatizo ya ajali nchini mwetu. Hawataki kuona mapungufu ya serikali isipokuwa wanataka kulazimisha watu waone mafanikio yake.

JF itaendelea tena bigger and better.. wiki ijayo tutakuwa na mambo mazito ambayo Inshallah, siyo tu yataendelea kuliamsha taifa bali pia kulithubutisha Taifa zaidi na zaidi. Hapo ndipo tofauti ya kijiko na chapeo itakapoonekana.

Ndiposa, mstari wa maamuzi unazidi kuchorwa ardhini na ukuta wa tofauti za kifikra unazidi kupandishwa. Hatimaye kambi mbili zinazohitajika hapa JF zitakuwa dhahiri zaidi. Sasa wamefikia mahali pa kufuatialia nani "anampenda nani"! Hoja lazima zijibiwe kwa hoja, na hoja zenye nguvu lazima zishinde.

Tutaendelea pasipo hofu, husuda, woga, au kusita kwa namna yoyote kuonesha ni jinsi gani hoja zao ni dhaifu, kwani zinajengwa kwa msingi dhaifu. Kwa hili, kundi la tatu litaendelea kufuatilia na kuamua kutokana na hoja. Mapambano haya tuliyaingia kwa hiari, na hatutakoma, hatutarudi nyuma, hatutakatishwa tamaa na yeyote yule hata kama atajivika vazi la kondoo! Tumewapinga watawala wetu, tutawapinga na wapambe wao!!

Tutaendelea kuwakosoa na kukosoa sera zao potofu, na kukebehi mwelekeo wao wa kibabe! Hatutawaonea aibu, hatutawaficha, na wakati utakapofika (na hauko mbali) wale wote waliohusika na kulibaka taifa letu, na kuchota mali ya wana na mabinti zetu, huku wakiendelea kupepea vibendera vyao, wakizungukwa na wapiga saluti, huku wakiimbiwa nyimbo za pongezi na wakicheua mafuta ya mali za Watanzania, watasimama Mahakamani! Iwe katika mahakama ya sheria au mahakama ya watu, kwa hakika watajibu, iwe kwa hiari au kwa nguvu za sheria!!

Wale waliomua kuchagua upande wa watawala wetu na kuwatetea na kuwalinda, na kuwapaka rangi ili wapendeze, huku wakiwamwagia manukato na marashi wakati wamevunda na wao wanakaribishwa! Hatutalia mada zetu zikifutwa au kuhamishwa, hatutalalamika kwa kujaza posting zile zile watu wasipotujibu, na MoDs wakiamua kufanya lolote hatulia kama watoto waliodekezwa!

Tutaheshimu jambo forums, tutalinda kanuni ya msingi wake, na tutaitetea pasipo majigambo yoyote yale. JF itadumu, na hasa baada ya wimbi la pili la mapambano lijalo.

kwani unabii wa kuanguka kwa CCM utatimia, kwani uko mbioni, na unafanya hima kutimia!

M. M.
 
Kila penye kusifu nasifu huwa siangalii itikadi.Nilisifu sana kwa kutuletea mikataba hii na niliomba kama ku uwezekano wa kupatikana yoote basi iletwe hapa tuijadili.

Mkuu sidhani kama kuna mtu anaipondea JF wala kubeza kazi na hoja za member humu.Woote hatuwezi kuwa sawa kimtazamo na maendeleo yanakuja baada ya kutokea migongano(conflicts) katika jamii husika alisema karl marx.

Sasa basi naomba tu hii ya kusema kuwa fulani wanaipondea JF iishe sio kauli nzuri kwa kweli
 
vitendo vitaongea zaidi ya maneno.

Mbinu za kupondea JF nakuhakikishia kuwa zitashindwa and for your information, watu wengi serikalini wameona jinsi watu walivyodefy nature na kuweka mkataba hapa na sasa wanatafuta namna ya kuivujisha mingi zaidi ili iwekwe hapa.

JF is here to stay baby na mafisadi mtashindwa tu na mbinu zenu
 
Kila penye kusifu nasifu huwa siangalii itikadi.Nilisifu sana kwa kutuletea mikataba hii na niliomba kama ku uwezekano wa kupatikana yoote basi iletwe hapa tuijadili.

Mkuu sidhani kama kuna mtu anaipondea JF wala kubeza kazi na hoja za member humu.Woote hatuwezi kuwa sawa kimtazamo na maendeleo yanakuja baada ya kutokea migongano(conflicts) katika jamii husika alisema karl marx.

Sasa basi naomba tu hii ya kusema kuwa fulani wanaipondea JF iishe sio kauli nzuri kwa kweli

tofauti yetu na chama tawala ni kuwa hatuhitaji kusifiwa wala kuomba kusifiwa. Tunaongozwa na matamanio ya Taifa lenye viongozi wanaowajibika, lenye uwazi, na ambalo linasukumwa na maslahi ya maendeleo ya watu wake.

Hivyo juhudi za baadhi ya wanachama kuongoza mashambuzi ya kuharibu mtiririko wa mada kwa sababu zao binafsi ni juhudi ambazo zimezaliwa ili zishindwe! Lengo la kuwawekea mikataba hiyo hapa siyo kuonesha nani ana uwezo wa kufanya kitu fulani, lengo letu ni katika kuchangia mjadala wa mustakabali wa Taifa.

Kila mmoja atimize wajibu wake, lakini kuanzisha mada kumjadili mwanachama mwingine ni kitendo cha kutishia na kunyanyasa mtu. Kama una swali na unaona la msingi muandikie chemba muulize akikujibu yanaisha huko. Sasa kwenda kuanzisha mada juu ya mada.. ndiyo nini hicho?
 
Wale waliomua kuchagua upande wa watawala wetu na kuwatetea na kuwalinda, na kuwapaka rangi ili wapendeze, huku wakiwamwagia manukato na marashi wakati wamevunda na wao wanakaribishwa!
Naona kelele ni nyingi hapa,iwapo mtu atashindwa kuafiki hoja zako ambazo kwa wengine zinaonekana kuwa ni za kichochezi zaidi badala ya hoja, ina maana kuwa wao ni watetezi wa hao unaowaita wamevunda?
 
Kangala na mataputapu...
 
Naona kelele ni nyingi hapa,iwapo mtu atashindwa kuafiki hoja zako ambazo kwa wengine zinaonekana kuwa ni za kichochezi zaidi badala ya hoja, ina maana kuwa wao ni watetezi wa hao unaowaita wamevunda?

the answer is A!
 
Back
Top Bottom