Uchaguzi 2020 CHADEMA msifanye kama wanavyofanya CCM

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Kutenda kosa kwakuwa CCM inatenda kosa sio Kinga kwenye adhabu ya kosa ulilotena.

Kama CCM na wagombea wake Kuna kosa la uchaguzi wanalitenda njia sahihi ya kwanza ni kupeleka Tume au kwa msajili kwa maandishi makosa yao. Kama hatua haichukuliwi dhidi ya mlalamikiwa ndio mfikirie kufanya vinginevyo.

Fuateni sheria inavyosema kabla ya kuchukua njia zenu. Makosa mawili hayatengenezi jema moja.

Mkifanya hivyo hata dunia itakuwa shahidi.
 
Inahitajika Subra ya hali ya juu sana kuona mwenzako anafanya kosa halafu haukumiwi wewe kosa lilelile unahukumiwa fastaa UVUMILIVU WAKE HATA MIMI SIUWEZI.

KAFA KADA FASTA WATUHUMIWA WAMEPATIKANA NA DPP KAPROCESS CASE, WENGINE AZORY, SAANANE NA KUPIGWA RISASI LISSU HADI LEO WALE WATU HAWAJAWAHI KUJULIKANA.

DOUBLE STANDARDS.
 
Kesi ya mauaji Njombe wameshughulikia fasta wakati ya Lissu hadi sasa hajakamatwa hata mtu wa kumsingizia au wa sinema tu kama yule kichaa wa Kova kule Kawe
 
Hahaha kama ulikuwa hujui kwa serikali hii ya ccm kila mwanachama wa chadema tayari ni mtuhumiwa, wanasubiri kosa wana mkamata mwana chama wa chadema yeyote aliyeko jirani.

Hakuna upelelezi wa aina yoyote nchi hii kwa sasa, ukisikia bado wanapeleleza jua hiyo kesi ni ya kutengenezwa wana tafuta namna ya kumshindilia mtuhumiwa.
 
Ukiiba kuku kwakuwa masoud aliiba pia bila kukamatwa sio sawa. Kazi yako Ni kutoa taarifa polisi na kutoa ushahidi mahakamani dhidi ya masoud ili ahukumiwe badala ya kuiba ukitegemea kutendendewa Kama masoud
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…