PreGE2025 CHADEMA Msimbazi yamtaka Patrick Asenga ajieleze kwa kupinga Agenda ya 'No Reforms, No Election' mtandaoni

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Team Mbowe, unajua Mbowe hakublvunja kambi yake
 
Na kwa nini mnahitimisha kuwa wanaopinga No election without reform ni wafuasi wa Mbowe, mbona jamaa toka uchaguzi uishe amekaa kimya hajaongea lolote.

Nadhani Pro Lissu mnaendeshwa na fear of the unknown, mnadhani kila anayepinga ni Pro Mbowe, hamtaki mawazo tofauti na yenu, mnakuwa kama ccm tu. Mnanishangaza..
 
Watakubali tu
 
Kaka unahitaji miwani gani kulitambua hilo wakati G55 wote ni ile team yake ya kampeni ikiongizwa na meneja wa kampeni Mr. Naftali?
 
Kaka unahitaji miwani gani kulitambua hilo wakati G55 wote ni ile team yake ya kampeni ikiongizwa na meneja wa kampeni Mr. Naftali?
Lissu na timu yake anachukua juhudi gani kumaliza makundi ndani ya chama, kumbuka hilo ni jukumu lake. Ndio maana alimwambia Mbowe aende sabbatical ili wao waweke chama vizuri. Mbona hafanyi hivyo?
 
Wasusie tu ni haki yao
 
Lissu na timu yake anachukua juhudi gani kumaliza makundi ndani ya chama, kumbuka hilo ni jukumu lake. Ndio maana alimwambia Mbowe aende sabbatical ili wao waweke chama vizuri. Mbona hafanyi hivyo?
Mtu wa kwanza kuvunja kundi alipaswa kuwa Mbowe.

Kazi ya Lissu ni kuwaonyesha upendo, kuwapq nafasi kama alivyomteua Ruge.

Mwisho Lissu amewapa wazee wa chama kazi ya muafaka na usuluhishi na alishasema hadharani.

Je alipaswa afanye nini zaidi?
 
Lissu atakuwa na kazi kubwa ya kufukuza, No reform no election itawaondoa wengi chadema.
Kwanza lisu atakuwa na balaa zaidi baada ya mwaka mmoja kwasasa ni trela....kwasasa acha adili na madalali
 
Mtu wa kwanza kuvunja kundi alipaswa kuwa Mbowe.

Kazi ya Lissu ni kuwaonyesha upendo, kuwapq nafasi kama alivyomteua Ruge.

Mwisho Lissu amewapa wazee wa chama kazi ya muafaka na usuluhishi na alishasema hadharani.

Je alipaswa afanye nini zaidi?
Kwangu Lissu bado hafai naona, kwanza ni dikteta kama Magu tu japo alikuwa anamsema sana.

Nimesoma katiba ya chama chao, amempokonya Ruge nafasi yake kinyume na sheria, swagga za Magu kabisa.
 
Kwangu Lissu bado hafai naona, kwanza ni dikteta kama Magu tu japo alikuwa anamsema sana.

Nimesoma katiba ya chama chao, amempokonya Ruge nafasi yake kinyume na sheria, swagga za Magu kabisa.
Weka ushahidi wa katiba mkuu
 
Hiki chama kilitumika kama kwa manufaa ya wengine, sasa wamebanwa. Na wengine walidhani ni cha kanda ya kwao. Afukuzwe tu
 
Kwangu Lissu bado hafai naona, kwanza ni dikteta kama Magu tu japo alikuwa anamsema sana.

Nimesoma katiba ya chama chao, amempokonya Ruge nafasi yake kinyume na sheria, swagga za Magu kabisa.
Huoni Ruge ameasi?
 
Msilaumu watu wenye mawazo tofauti na Lissu, jiulizeni mmekosea wapi, sio kila mtu ni pandikizi
Kakosea nini? No reform no election ni maazimio ya kamati kuu tena aliyatoa mbowe mwenyewe na baadae yakabarikiwa na mkutano mkuu baada ya majadiliano sasa kivipi kashinda Lissu ndio wanaigeuza kma ni agenda yake binafsi?

Wanatafuta sababu tu za kujiondoa kwa chama.
 
Wako sahihi awajinishwe
 
Baada ya. CCM kujiikomboa na udikteta, chadema wamepata wa kwao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…