PreGE2025 CHADEMA Msimbazi yamtaka Patrick Asenga ajieleze kwa kupinga Agenda ya 'No Reforms, No Election' mtandaoni

PreGE2025 CHADEMA Msimbazi yamtaka Patrick Asenga ajieleze kwa kupinga Agenda ya 'No Reforms, No Election' mtandaoni

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Kwangu Lissu bado hafai naona, kwanza ni dikteta kama Magu tu japo alikuwa anamsema sana.

Nimesoma katiba ya chama chao, amempokonya Ruge nafasi yake kinyume na sheria, swagga za Magu kabisa.
Dikteta ni huyo mliye naye
 
Msilaumu watu wenye mawazo tofauti na Lissu, jiulizeni mmekosea wapi, sio kila mtu ni pandikizi
Mawazo tofauti yana utaratibu wake ktk kuyatoa hususani kwa viongozi walio na nafasi ya kuingia kwenye vikao vya maamuzi...

Lakini kiongozi mwenye nafasi ya kuingia vikao, maamuzi fulani yakafanyika kwa pamoja yeye akiwa sehemu ya maamuzi hayo halafu akatoka nje na kuyapinga nje ya utaratibu, kiuhalisia huyo anakosa sifa ya kuwa sehemu ya jumuiya au taasisi hiyo..

Mwacheni ajieleze tuone atajitetea kwa kusema nini. Ameipata ile iitwayo "natural justice". Hiyo itakuwa hivyo kwa wote walioandaa waraka huo...!
 
Msilaumu watu wenye mawazo tofauti na Lissu, jiulizeni mmekosea wapi, sio kila mtu ni pandikizi
Mawazo tofauti yanatolewa katika vikao kabla ya maamuzi au kupigiwa kura! Jambo au hoja ikishapitishwa na kikao au mkutano wa Chama lazima itekelezwe na wote waliopinga na waliounga mkono, kinyume chake ni usaliti au uhaini! Kama ni kiongozi anapinga maamuzi ya chama anapaswa kujiuzulu nafasi yake na kama hawezi kuvumilia kabisa ajiondoe katika chama.
 
Back
Top Bottom