Mwande na Mndewa
JF-Expert Member
- Feb 26, 2021
- 1,117
- 3,153
Leo Chadema wanaanza mikutano yao ya kisiasa Jijini Mwanza ambapo ndio kitovu cha kanda ya Ziwa,takwimu za sensa kwa namba zinaitaja Mwanza kama mkoa wenye watu wengi kuliko mikoa yote,Mwanza ikiwa na wakazi 3,699,872 kitakachofanyika Mwanza kitapokelewa Kagera yenye wakazi 2,989,299 kitafanyiwa kazi Geita yenye wakazi 2,977,608 kitasemwa Mara yenye wakazi 2,356,255 kitafurahiwa Shinyanga yenye wakazi 2,123,654 kitapelekwa Simiyu yenye wakazi 2,078,428 hivyo basi,Jambo hilo litakuwa limewafikia Jumla ya watu milioni 15 ambayo ni kama robo tu ya watanzania wote,Kama mgombea wa CCM au Chadema atakuwa na mtaji wa takribani wapiga kura 11.2 Milioni ambao ni wanachama wa CCM,based on voters behaviour,tuchukulie mfano wananchi 29M wamejiandikisha,halafu wananchi kati ya 12 - 16M wakatajitokeza kupiga kura mwaka 2025, Ikiwa Mgombea wa CCM tayari anakura takribani 11M, ni wazi kuwa tayari Mgombea wa CCM ni Rais anayesubiri kuapishwa.
Tabia ya wapiga kura wa kanda ya ziwa ni kuwa wana msimamo,mwaka 2015 Mikoa ambayo Hayati Rais Magufuli alipata kura nyingi ukiacha Dodoma mingine yote ni mikoa ya Kanda ya Ziwa(Geita,Mwanza,Kagera,Shinyanga n.k) Kanda ya ziwa wanatabia ya ukweli ulionyoika,koleo wataita koleo na kijiko wataita kijiko,ndio maana walimchagua tena Rais John Pombe Magufuli katika uchaguzi mkuu wa Urais wa mwaka 2020,kesho Chadema wanaenda kuanzia mikutano yao jijini Mwanza,hii si kwa bahati mbaya,kanda ya ziwa ina wapiga kura wengi kuliko kanda yoyote ile Tanzania,kanda ya ziwa ina determine urais wa nchi hii hivyo mwanasiasa yeyote anapaswa kuchagua maneno na kauli zao kuhusu watu wa kanda ya ziwa na hasa kwa kipenzi chao kama Hayati Rais John Magufuli.
Watu wa Kanda ya Ziwa wana falsafa yao inayosema “Kama matendo yako yanavutia wengine kuwa na ndoto zaidi,kujifunza zaidi,kufanya kazi zaidi na kukua zaidi,basi wewe ni kiongozi”,hili limedhihirishwa na Rais Magufuli aliyeonesha kwa vitendo kuwa yeye ni kiongozi ambaye anataka kutimiza malengo yake ya kuleta mabadiliko na maendeleo ya kweli pasipo kuyumba wala kuyumbishwa na kundi lolote,alikuwa ni kiongozi mwenye msimamo na asiyependa kujikweza wala kutumia fedha za walipa kodi kwa mambo ya anasa badala yake anaelekeza fedha zitumike kwa manufaa ya watu wote na kwa faida ya muda mrefu kama vile kuboresha huduma za afya, upanuzi wa barabara na kuwekeza katika elimu,hivyo viongozi ndani ya Serikali na hata kambi ya upinzani inapaswa kukubaliana na falsafa hiyo iliyowakilishwa vyema na Hayati Rais Magufuli.
Utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi na Ahadi za Rais katika Mikoa ya Kanda ya Ziwa ni kielelezo kingine cha wazi kabisa kuwa Wananchi wa Kanda hiyo wameuona na kushuhudia wema wa Rais Magufuli kwao,amejenga miundombinu na huduma za kutosha mpaka wapinzani wakaona waitumie propaganda kuwa Kanda hiyo inapendelewa na kuonyesha choyo kwa watu hao (Hoja nyingine ya kuwanyima Kura) na kwa kweli jamii hiyo ya watu wanajua kukirimu sana mtu aliyewafanyia wema,Hayati Rais Magufuli alikuwa mwema sana kwao na wakamlipa kwa kumpigia kura nyingi,Enzi Mwaka 2019,kanda ya ziwa ilichangia Trilioni 34 kwenye uchumi wa Tanzania sawa na 25.9% ya pato la Taifa,Kanda ya ziwa ilizalisha zaidi ya 90% ya dhahabu Tanzania,Kanda ya ziwa ilizalisha zaidi ya 50% ya pamba na kahawa iliyouzwa nje ya nchi,Kanda ya ziwa ilizalisha zaidi ya 95% ya mauzo ya samaki ndani na nje ya nchi,Kanda ya ziwa ilivutia zaidi ya 80% ya watalii ama mapato ya utalii Tanzania,Kwa maana kwamba Serengeti national park hutembelewa na zaidi ya 80% ya watalii wanaokuja Tanzania,bila Serengeti utalii Tanzania ni kama haupo.
Mwanamuziki maarufu wa Afrika Kusini, Miriam Makeba amewahi kusema, “Umri mkubwa ni kitu cha kujivunia maishani. Kwani unakuwezesha kujua namna zote dunia inavyogeuka ili kama huwezi kugeuka nayo basi uweze kuipisha isije ikakuponda wakati inageuka”.Awamu ya tano Rais Magufuli alikiwezesha chama chake cha CCM kwenda na wakati na kugeuka sanjari na mabadiliko ya kisiasa na kiuchumi ili kisipondwe na kuwekwa chini na wanamageuzi wanaotaka kuona Tanzania yenye viongozi waadilifu na wenye nia ya kuleta maendeleo ya kweli kwa watu wote na awamu hii ya sita Rais Samia nae anakwenda na wakati sanjari na mabadiliko ya kisiasa na kiuchumi,tunapoelekea 2025 Uchaguzi ni maarifa,mipango na akili,hakuna kitu kina guarantee ushindi katika mpambano wa kisiasa kama kuchanga karata zako vyema,na kwa kuitazama CCM chama changu,ni wazi kuwa Viongozi wake na Mgombea mwenyewe amejipanga vyema sana.
Ukizungumzia kanda ya ziwa haumaanishi eneo la ardhi ila kuna vitu tunaangalia mfano ushawishi pili muingiliano tatu tamaduni.Ushawishi ukweli ni kwamba ushawishi wa kanda ya ziwa umesambaa mpaka Tabora,kigoma na katavi na hub ya biashara ni Mwanza,Pili muingiliano ni mkubwa sana kwasababu tabia na tamaduni za hawa watu zinaendana sana mfano msukuma(mwanza,shinyanga,simuyu na munyamwezi (tabora) pia waha(kigoma),wahangaza(kagera) na wasubi (geita) hawa ni jamii moja pia na tamaduni za hawa watu zinafanana sana,Sasa basi,Chadema leo mtajibu maswali magumu kutoka kanda ya Ziwa kwanza kwa kumtukana Hayati Rais Magufuli,naamini kwa dhambi hii maandalizi ya mkutano wenu Mwanza yatadoda,pili mtakodisha bodaboda kwa michango yenu ili muwajazie mafuta waandamane kwenda Furahisha,mliwaita wasukuma washamba mkawabatiza "Sukuma Gang" hii haikuwa sawa kumpa mtu jina ambalo si lake,na mwisho mlifurahia kifo cha Hayati Rais Magufuli,hii dhambi itageuka laana juu ya mikutano yenu kote kanda ya Ziwa,mlipaswa kuwa na hekima na busara,ila sasa muda unawahukumu.
Nikiishia hapa, Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078854
-Bachelor of Business Administration in International Business.
-Master of Leadership and Management.
Recent Publications;-
-Assessment on the effect of Micro-Financing on Poverty Reduction.