CHADEMA Must Reform and Restructure now!

Mchugaji,

Nadhani umezungumza swala ambalo mimi nimekuwa nikiteta sana na baadhi ya ndugu na jamaa pindi baada ya uchaguzi.
Ukweli ni kwamba CHADEMA kina future pana sana nchi Tanzania, ni chama pekee ambacho kinaweza kuwa mshindani wa CCM na tegemeo kwa Watanzania wengi ambao wamepoteza matumaini katika swala zima la maendeleo.

Lakini swala la CHADEMA kuwa chama mbadala sio swala lelemama, ni swala ambalo kazi kubwa zaidi inabidi ifanyike. CHADEMA kinabidi kikae chini kama chama na kufanya uchambuzi yakinifu wa tunapotoka, tulipo na tunapokwenda. Chambuzi hii yakinifu inaweza kukipa chadema picha sahii ya nini kifanyika.

Kwanza nakubaliana kabisa Wabunge wote wa CHADEMA wasishike nafasi zozote kwenye chama. Wao waongeze nguvu na uchapa kazi Bungeni, walete hoja nzito ambazo zimejikita kwenye uchunguzi yakinifu, wawasukume CCM bila kuchoka kwenye kila kona. Pili Chadema iweka mkakati wa kuhakikisha inatetea majimbo yote iliyoshinda mwaka 2010 katika uchaguzi wa mwaka 2015. Na kwa serikali zote za mitaa ambazo zinaongozwa CHADEMA basi wawahakikishie wanchi wa sehemu hizo kwamba chaguo mlilochagua ni sawa kabisa.

Pili, CHADEMA ijiendeshe kisasa na kiuwazi zaidi. Nilazima baadhi ya watu waajiriwe na walipwe mishahara minono ilikuongeza ufanisi. Nilishasema KITILA inabidi ajiliwe full time na ajikite kwenye CHADEMA Strategy department. Hii iwe department ambayo ita craft na kuandaa njia za kuexecute strategy zote za chama. Hawa ndio Brain ya Chama, wanatengeneza njia zote za ushindi kwa majimbo mbishi, hapa ndipo strategy za kuondoa mchezo wa kuchakachua matokeo zitakopo anzishwa. Department hii inabidi ipewe vifaa vya kisasa na tekinologia ya juu.

Tatu, Chadema lazima itanue ramani yake ya ushindani ( stretching Political Map) hasa kwenye majimbo ya Kusini mwa Tanzaia na Zanzibar.

Mwisho, ni wazi kabisa gatcha politics haiwezi kukifanya chama hiki kikawa chama bora Tanzania. Hivyo basi hoja nilazima ziundwe kwa facts na kwa uyakinifu kabisa kuonyesha umuhimu wake kwa maendeleo ya Tanzania.
 
Ushauri wa Rev Kishoka unaegemeaa zaidi mafanikio Chadema iliyopata katika uchaguzi huu bila kuangalia historia yake na mwelekeo. Haifichiki Chadema yenye mvuto imeonekana zaidi chini ya Uongozi wa Mbowe na hili lazima likubalike kama msingi wa kujenga chama hiki.

Kwa nini chadema imekuwa na sauti na mafanikio zaidi kisaisa chini ya Uenyekiti wa Mbowe? ni swali bora la kujiuliza na kuanzia hapo tusonge mbele kuijenga chadema imara. naamini kwa dhati kabisa mbowe ameonyesha uwezo wa kiuongozi katika kuunganisha na kujenga taasisi imara ya kichama yenye mwelekeo wa kukua. Hii yaweza kutokujadiliwa vema kwa sababu tuu ya kuweka suala la mvuto mbele zaidi kuliko mikakati na busara za kiuongozi ambazo Mbowe amaezionyesha katika uenyekiti wake.

Mbowe ameweza kuifanya chadema sasa kuwa chama kikuu cha upinzani nchini na kukubalikaa katika maeneo mengi nchini akishirikiana vema na Wenzake. Naamini Mbowe ni msikivu, mweledi, mwenye upeo na kiu kubwa ya mabadilko ya kisiasa chini kwa dhati.

Tutumiee msingi wa mafanikio yake kuipelekaa chadema mbele zaidi. watanzania lazima wakubali mabadilko na gharama zake kwa kuwa tayari kushiriki kwa dhati kwenye mustakabali wa mabadilko ya uongozi wa nchi kwa dhati. Sishangai chadema kukosa wagombea katika majimbo mwaka huu kwani hiyo ni tabia ya watanzania kuvutika baada ya dalili fulani. CCM hupata wagombea lukuki kwa ajili tuu ya mfumo mkongwe na matarajio makubwa ya wagombea kwamba bado CCM hakijwa na chama mbadala. Sasa ipo chadema baada ya matokea hayaa.
 
are u serious freeman hakuweza kukijenga chama, labda una bifu nae binafsi
acha chuki binafsi, kutoka viti 11 mpaka viti 46 unasema chadema haijakuwa, eti hakijaandaliwa kikamilifu.......
nenda kwenye mkutanno wa chadema halafu umsikie freeman akiongea ndio utajua kama ana mvuto au hana, utayameza maneno yako


by the way dr slaa sio mbunge na ni mtendaji mkuu wa shughuli za chama

Sambamba na Dr. Slaa kama Mwenyekiti, Chadema na Dr. Slaa vinanahitaji mtu mwenye uwezo kama Willy Lwakatare kama Katibu Mkuu kuratibu shughuli za Chama na kusaidiana katika kukijenga na kukiongoza Chama.
chadema ina watu wengi wenye uwezo na lwakatare ni one of them

:sad:


wacha hizo wewe watu wanajitahidi wewe unaleta majungu
 
Wewe si ndio ulikuwa anaishabikia CCJ ambayo couldn't see the light of day.Kama una huo upeo wa kujua kiongozi gani ni mzuri na yupi sio mbona ukujua kama Richard Kiyabo na wenzake walikuwa wababaishaji.

Chadema hapo nyuma kilikumbwa na migogoro mikubwa kama sio weledi wa Mbowe kisingeweza kufika hapa kilipo Kutoka wabunge 5 mpaka wabunge 23 wa kuchaguliwa.Mimi nina kubaliana na wote wanaosema Dr Slaa(Phd) awe mwenyekiti lakini sio kwa kubeza mchango wa Mbowe.
 
Mageuzi katika nchi yoyote ile hayaji kwa mara moja, ni safari ndefu but naamini watanzania wako tayari kwa safari hiyo na wengine walishaianza.
 
Hivi mnkumbuka Nyerere alifanya nini kuimarisha TANU? Aliachana na Serikali akawekeza nguvu zake zote kukijenga Chama. Tuna tatizo moja la kukimbilia kutatua matatizo ya Kitaifa ilhali tatizo kubwa mabalo ni fundisho la chaguzi zilizopita tunaliona halina maana.

Chadema inahitaji Mwenyekiti na Katibu Mkuu ambao watawekeza muda, nyenzo na nguvu zote kukiimarisha chama na kukijenga. Kazii hii inajumuisha kutoa elimu ya uanachama, kujenga itikadi na sera za Chadema kwa wanachama wake, kuhakikisha kuwa kila kona Chadema inajijenga kifikra na kiidadi kwa kuwa na madarasa ya kufundisha Wana Chadema na kuwapika kisawasawa.

Aidha kasi hii itatumika kujenga ngome imara isiyorubunika katika ngazi za wilaya hata mkoa na kuhakikisha ufanisi wa kichama katika kuongeza wanachama, kutafuta michango na kuhakikisha kuwa Wanachama wake wanajiandikisha katika daftari la kupiga kura.

Ama kazi ya Mwenyekiti iwe ni kuangalia ukuaji huu wa chama na mbinu za kushindana na kina CCM na CUF, huku wale waliojko Bungeni kina Freeman, wanapigana vita ndani ya Serikali na kuimarisha Chadema Kiserikali.

Sasa chukulia mfano wa kilichotokea kwenye Uchaguzi, Freeman kama Mwenyekiti, alikuwa na nafasi ndogo sana kwenda kufanya kampeni kwa Wanachama wengine kwa kuwa yeye alibidi atete jimbo na kuendesha kampeni ya kutaka yeye achaguliwe. Hivyo kama wangekuwa na Mwenyekiti na Watendaji wa kichama wasioshikwa na uwajibikaji kijimbo, ingekuwa ni kazi rahisi sana kwa Mwenyekiti kufanya kampeni na kuhakikisha kuwa chama kinakua.

Nyakati zimebadilika na ni wazi kuwa lazima kuwe na mabadiliko ya namna fulani.

Ninachoomba ni kila mtu kutumia muda kusoma na kutafakarti na kuona kama ninachosema kina mantiki na kina uwezo mkubwa wa kukijenga chama ili ikifika 2014, kuwe na miundombinu bora ndani ya Chama na kuwezesha kutoa wagombea mahiri wa Udiwani na kuingia TAMISEMI na ikifika 2015, kusiwe na ile kazi ya kubahatisha ya kuhangaika kutafuta ni nani anafaa kugombea jimbo fulani au kusubiri tena wale watakaotemwa na CCM.

Chadema has a choice to ignore what I am offering as advise or take into consideration and accept another set of eyes that can help them to become succesful.
 


you got it wrong, hata hao CCJ na kusaidiwa na mzee Mwanakijiji niliwachamba..
 
Katibu mkuu ndiye mtendaji mkuu wa chama,Dr Slaa akiwa mwenyekiti atakuwa mwangalizi tu na sio mtendaji. Mnakuja na mada ndefu kama mnatakia mema chadema lakini ukipitia vyema mada hizi unagundua waleta mada wamelewa propaganda za ccm,mbowe ni mtu muhimu sana kwa chadema na huwezi ukajua mpaka uingia kwenye mikutano ndo utamjua. Watu wengine ni wazuri sana kuropoka kwenye vyombo vya habari ila mbowe yuko very strategical.kama mko nje ya chadema ingieni ili muujue mfumo,msifikiri mafanikio haya yamekuja kwa bahati mbaya,watu waliwekeza kama huamini soma utangulizi katiba ya chama toleo la 2006, mbowe aliwekeza muda na mali,slaa alikuwa mtendaji bora wa chama na pia alikuwa mbunge bora kabisa. Propaganda za kuwa wabunge waachane na chama wawe wabunge bora ni bullshit!!makada wazoefu wote ni wabunge isipokuwa wachache tu wakikaa pembeni makada wapya itabidi waanze upya. Akina Mkumbo wanayafanya hayo kwa kusaidiwa na makada wazoefu...
 
Wapenzi wa kweli wa Chadema ni heri waanze kwa kuwafahamu wanaowatakia mema na wale wenye ajenga zinazovishwa ngozi ya kondoo kumbe ni mbweha. Wanadai wanaitakia mema Chadema kumbe lengo lao hasa ni kupandikiza hoja za nguvu zinazowalenga watu fulani fulani ndani ya Chadema huku wakisukumwa na chuki binafsi zisizo na msingi wowote. Huu si muda mwafaka wa kutaka kuwagawa wananchadema kwa kumshambulia mwenyekiti Mbowe kwa dhihaka zisizo na kichwa wala miguu, huku ni kubomoa na si kujenga. Huu si muda mwafaka wa kuitaka Chadema iunganishe nguvu zake na CUF au NCCR mageuzi bila kutafakari hali halisi, huku si kujenga ni kusambaratisha. Kuna wale ambao kama yangekuwa matakwa yao Mbowe au Marando hawangekanyaga milango ya Chadema - eti Mbowe hana mvuto wala hoja, jamani wakati mwingine tujaribu kuwa wakweli kwa nafsi zetu na tuweke chuki binafsi kando.
 
kimsingi chadema ni chama ambacho kinapendwa sana na watu wengi kwa kuwa kinaonyesha jinsi gani wanakuja kulikomboa taifa kutoka katika wimbi la umaskini na ufisdadi uliokidhiri.
tamko lao la jana kuhusiana na matokeo ya urais yameweza kuwaongezea imani kubwa kwa wananchi hususan waliopiga kura na wale ambao hawakupiga kura ivyo itasaidia kukuza chama na kutokana na dr slaa kutokuwa mbunge na kuwepo kwa raslimali fedha na watu wa kutosha ni muda muafaka kuzunguka hasa maeneo ya vijijini na kusambaza habari za kuleta abadiliko. ni matumaini ya wengi kuwa ifikapo mwaka 2015 itakuwa imejiimarisha sana vijijini na pia kwa kuwa wapenzi wake wengi ni vijana na wasomi watu watakuwa wameenda dhule wengi na kuelewa hali halisi. nashukuru angalau mwanga unaonekana kwa mbali.
 
Mimi naona Rev. bado hajajua yuko wapi maana huu ushauri ni wa mtu anayewaongelea 'hao' pasipo kujiweka kwenye viatu vyao ndio maana anajikuta kwenye matamshi ya kilawama. Nakubaliana kabisa kwamba kazi aliyoifanya mbowe ni laana kuibeza, pamoja ya kwamba mafanikio ya CHADEMA sio ya mtu mmoja, katika kila timu kuna king-pin. Rev haonekani kutambua hilo ndio maana amejikita zaidi kwenye umimi wa watu hao. Hapo ndio panapofanya wengi wetu tushangae na kutilia shaka dhumuni lake. Hivi kama Mbowe asingekua mtu makini, ile njama ya mafisadi ya kumtumia Zitto kukisambaratisha chama wakati wa uchaguzi mkuu wa CHADEMA uliopita si wangeshatumaliza? Mbowe alikubali kumeza pini pamoja na kudhalishwa kote ilimradi chama kifike mbali. Haya mengine ya kupunguziwa majukumu kama ushauri yanaeleweka, lakini pia yatoe nafasi kwa wengine kuyachangia pasipo kuchachamaa. Lakini kama tunakubali kwamba CHADEMA si chama bali ni itikadi, basi na sisi tuchangie mawazo kama wadau hii itapunguza lugha ya lawama na dharau kwa mafanikio ya wazi yaliyokwisha patikana kwa CHADEMA.
 
Mchungaji ana maono makali na yenye hekima is time now chadema to go down there and dig out matatizo ya umma, kwa msingi huo nasi ccm hatulala kama tunayataka mamlaka haya yabaki kwetu = faida ya demokrasia kwa watz
 
Asante Rev. Kishoka, naamini wenye mapenzi mema na Chadema wamekuelewa, mimi nimeposti post kuhusu Chadema hawajajipanga, nakubali udhaifu wangu nilitaja majina na udhaifu wao, hivyo ikaonekana ni matukano.

Safu ya uongozi uliyoipendekeza ni nzuri, ila kwa maoni yangu, safu hiyo mpya ya uongozi pia ipinge baadhi ya dhana zilizojengwa dhidi ya Chadema, hivyo kwa ushauri wangu, Mwenyekiti akiwa denomination fulani, katibu mkuu awe denomination nyingine na nilitaja jina, halafu Rwakatare awe naibu katibu mkuu.

Kuna mafanatic wa Chadema ambao bado ni waumini kuwa Chadema ni chama cha kina fulani, na hao akina fulani, ndio wamewakabidhi chama kina fulani, hivyo hao waliokabidhiwa, chama ni mali yao. Ndio maana Zitto alipogombea Uenyekiti nilimuuliza amepata wapi manlaka ya kutaka kwenda juu bila ruhusa ya wenye chama?, Zitto na kiburi chake na kujiamini kwake kulikopitiliza, akataa ushauri wa kuomba baraka kwa wenye chama na kutangaza straight atawavaa wenyewe. Kilichofuatia sote tunakijua.

Hivyo ili kuondoa dhana ya Chadema ni chama cha kina fulani na ndio wamepewa kifamilia, hao kina fulani wakubali kupisha uongozi wa kitaifa zaidi ili kuifuta hiyo dhana ya kifamilia hata kama wamechaguliwa katika chaguzi halali ndani ya chama.

Angalizo kwa wapenzi wa Chadema na mashabiki wa chama hiki, Chadema sasa imefika level za juu kabisa, sio chama chenu tena, ni chama cha wote, ni chama cha kitaifa, kama kinavyopendwa Kaskazini, tungependwa kipendwe vivyo hivyo na Kusini. Tunawashukuru na kuwaheshimu waasisi wa chama hiki tangu walipokiasisi na kukitoa hapo kilipoanza mpaka hapa kilipofika, hapa ndio mwisho wao, its about time kuunda more capable team kukiondoa kwenye the running lane na kukipaisha kabisa angani na kuenea Tanzania yote.
 
Si Mbowe, Si Slaa, Chadema kimetegemea mtandao wao makanisa na hakitaenda zaidi ya maeneo ya ushawishi wa makanisa hayo, period!

Walio maofisini wanafanya kazi ya uwakala wa kanisa na chadema no wonder sasa hivi ofisi za serikali na mashirika zimegeuka vijiwe vya siasa! But its known na hakuna siri. Kuna vyuo vya makanisa sasa hivi ni kama matawi ya Chadema. Uchaguzi unakwisha anaetoa kauli ya kukubali matokeo ni Pengo!

Hakuna strategist awe Kitila au Baregu anayeweza kuwavua Chadema hiyo ngozi ya Ukrsito waliyojivika. Kamwe chadema hakitakuwa chama cha Kitaifa. Kinaweza kuwa kama chama-mwenza wake wa Ujerumani ambacho mnajua ni wakala wa kanisa.
 
Cdm ni wasikivu sana, haya ya rev kushoka 90% safi ila kumkandia freeman si haki, mafanikio haya ya chadema hayawezi kumuepuka freeman, turejee pia kuwa ni mbowe aliyejitoa muhanga kuuacha ubunge na kuwapigania wenzake 2005 na kuwapata hao watano majimboni na wamama takribani 5 from 2-3mp. Ni jitihada zake na ubunifu wake na timu aliyeiongoza waliwafikia watz; ni freeman aliyejitokeza tarime licha ya kitisho cha kifo cha wangwe..., tunataka mabadiliko hayo ili wapiganaji wawe na venue za kutosha kutuamsha
 
Hizi hadithi za udini wa CHADEMA zimeongelewa saaana na watu wa CCM wakati wa kampeni, pamoja na JK mwenyewe, katika jitihada za kuepukana na tsunami ya mabadiliko iliyoongozwa na CHADEMA, na kuhujumiwa na NEC na dola. lakini haikuwa na impact yoyote kwa wapiga kura. hiyo ndiyo habari njema. watanzania wanakwenda mahali ambapo wameshachoka kulishwa kasumba, wanaweza wao wenyewe kuchambua pumba ni zipi na mchele ni upi. talk of PEOPLE'S POWER!! Sasa ndugu yangu, inaonekana wewe una udini. umeipa lebo ya udini wa kikristo CHADEMA. tujiulize swali, kwa nini haya yote yanasemwa sasa, na hayakusemwa mwaka 2005 wakati Mbowe alipogombea urais? si kweli kwamba hoja ni kwamba mwaka huu kulikuwa na tishio la kweli la madaraka kuhama kutoka ccm? OK, kama ishu ni Dr. Slaa kuwa mgombea urais, huyu amekuwa mbunge tokea 1995, na amekuwa maarufu katika mengi. juu ya yote, alipoanza kuibua kashfa kubwa kubwa nchi hii, hakuna mtu yoyote aliyetukumbusha kwamba Slaa ni mkristo na ni Padri. ni pale tu alipoonesha nguvu yake kubwa kisiasa, ndipo tukaanza kusikia Padri...padri... miaka yote hii watu walisahau kwamba yule ni padri, ila wamekumbuka mwaka huu 2010.

It is very interesting kwamba fimbo iliyotumika kuipiga CHADEMA mwaka 2005 ilikuwa ni ukabila. lakini mwaka 2010 ikatafutwa fimbo nyingine, udini. hiyo ya ukabila iliendelea kusemwa lakini ilionekana hii ya udini ni nzuri zaidi. kama nilivyosema, kwa bahati nzuri watanzania hawana muda na argument kama zako mkuu. wanamsikiliza Slaa na wanamwelewa, na ndio maana amekuwa Star katika uchaguzi wa 2010. tunachozungumzia hapa ni jinsi ya kuimarisha hiyo status yake, ili ituwezeshe watanzania wote kupambana na mfumo mbaya unaokandamiza watanzania sasa hivi. Slaa na CHADEMA wamejitokeza kuwa real threat kwa system iliyoko madarakani, tokea NCCR ilipojaribu mwaka 1995 na kusambaratika. tunachohitaji ni jinsi ya kuisaidia CHADEMA ili isizidiwe kete na maadui wake, bali iondoe kasoro zilizopo zinazoizuia kwenda mbele zaidi. lengo lako ni kutukatisha tamaa. nakuhakikishia wapo wengi ambao hawatakatishwa tamaa na hoja kama hizi unazotoa
 

Mchungaji umeanza vizuri sana kutoa ushauri kwa chadema na kwa sehemu kubwa sana maelezo yako yanamshawishi mtu kuamini kwamba umefanya hivyo kwa nia njema kabisa ya kuwatakia mema chadema. Lakini kwa jinsi ulivyomzungumzia mwenyekiti wa chadema basi hapo ndipo ulipopotezea mwelekeo wa ushauri wako. Huwezi kuzungumzia mafanikio ya chadema unayoyakubali huku ukisema mwenyekiti hafai. You totally missing the point! Vinginevyo unaweza kuwa na chuki binafsi na mbowe ama la una agenda ya siri. Inawezekana unafahamu kabisa kuwa mafanikio ya chadema yamechangiwa sana na mbowe kwahiyo ili kupunguza nguvu ya ukuaji wa chadema basi unaona utoe ushauri "kwa nia njema" ya kukijenga chama huku moyoni ukitamani chadema ife kabisa kama si kupoteza mwelekeo. Unapotoa ushauri halafu unatoa na maagizo, unataja majina kwamba fulani awe mwenyekiti, huyu awe katibu kwa kuwa nanihii hana sifa sijui mvuto as if ni mashindano ya miss tanzania unashindwa kueleweka kabisa. Najua viongozi wa chadema ni wanachama hapa jf watakusoma na watasoma ushauri wa watu wengine na hatimaye watafanya maamuzi yatakayokijengea chama heshima na kitaendelea kukua na kufika kona zote za nchi na hili si suala la kulala na kuamka tu tayari kila kitu kimekamilika, inahitaji muda kuyakamilisha hayo yote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…