Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 19,362
- 48,879
Hiyo ofisi pamoja na ofisi ya NEC ni upuuzi mtupu. Wamekuwa chanzo cha matatizo. Ni wanafiki wakubwa. Hii ofisi, kwa unafiki inaofanya, ni aheti ingefutwa, ni hasara, haina faida kwa yeyote. Hizi ofisi mbili zimekuwa kama idara za CCM.
Ujumbe ni sahihi, lakini hawana credibility ya kutoa kauli hiyo. Ni sawa na jambazi la kutumia silaha liwakusanye watoto wanaodokoa uji, liwaambie watoto kuwa wawe waaminifu waache udokozi wa uji.
Na asiwe mnafiki, aeleze wazi ni chama gani hakina demokrasia ndani yake. Kama ana ubavu aitaje CCM, kuwa hairuhusu wagombea wengine wakati Rais aliyepo madarakani anapogombea. Au awaulize kwa nini Rais ni lazjma awe mwenyekiti wa Chama huku wengine wakiambiwa hawatakiwi kuwa na kofia ya chama na Serikali.