CHADEMA mwendo mdundo

Chadema kuna shida kubwa ya uongozi nadhani Mbowe anapashwa kujiuliza sana .Kukubalia mawazo tofauti ndiyo jibu na kuna haja ya kuangalia upya uendeshwaji wa Chama . Tusikate tu naamini sasa kwamba kuna tatizo kubwa kuliko ninavyo dhani Chadema wanaweza kubadilika na nadhani tatizi si la Chama ni wachache ndani ya Chadema .Uongozi ujiangalie upya .
 
Kamende usisahau kuwa aliyeanzisha hii thread ni Ibrah na wachangiaji wengi watakuwa kina kanda2, chuma, Tumaini na kubwajinga.
bahati mbaya saana na wewe umechangia
 
Mkuu kwanini Tusianze kuhoji kwenye CHAMA TAWALA KWANZA ? Au mambo ya CCM yana kwenda vizuri ?[/FONT]
Mkuu naomba kutofautiana na wewe kwa asilimia 100 and beyond, Yaani unataka CHADEMA iwe inapimwa kwa kufananishwa na CCM, kwa hiyo unachotaka kusema ni kuwa kama CCM wanaboronga sana basi CHADEMA waboronge kidogo.?

Hatuna haja ya kuhoji chama tawala kwasababu tumeshawaona walivyo hovyo sasa tunataka kumpa CHADEMA tunahitaji ajiweke vizuri bahati mbaya tunapomwambia kakaa uchi afunike ni mbishi na anataka tuendelee kumfananisha na maiti aliyelala uchi. C'mon!!! Khaaa
 
mwafrika ndio aina wanachama unategemea mabadiliko..family club..na walevi wa pombe.
 
Tatizo lenu ni ulimbukeni tu..!
 
Jina la mchawi wa CHADEMA nitaliweka wazi mpaka atakapoachia ngazi ili tuweze kujenga upinzani wa kweli na kuikoa nchi.

Kuhusu binti wa kimachame, hiyo isikupe shida manake hawawekeki ndani ndio maana hata Mbowe alikimbilia Marangu.
 
Mkuu Lunyungu,
Maneno yako ni ya busara sana ingawa imekuchukua muda kidogo kukubali ambayo wengine tuliyaona siku nyingi.

Mtanzania yeyote anayeipenda nchi yake angependa kuona kunakuwepo na upinzani wa kweli nchini hata kama yeye sio mwanachama wa upinzani au wa chama tawala, kwani inaimarisha utawala.

Tatizo ni kuwa Watanzania wengi wamejifungia sana kwenye itikadi na ushabiki wa vyama kiasi kuwa, wamefikia wakati wanajitahidi kuyapamba matatizo ndani ya vyama vyao kama vile ni matatizo ya ndani ya ndoa.

Kwa nini tusiyakubali matatizo na kujaribu kuyatafutia ufumbuzi badala ya kuyaficha na kukataa uwepo wake?
 
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesema propaganda na shutuma mbalimbali zinazoendelea katika chama hicho wamezizoea na haziwatingishi kwani watazimaliza katika vikao vya chama.

Kimedai kwamba hali kama hiyo imekuwa ikitokea mara kwa mara kunapokaribia uchaguzi mkuu, kwani Chadema ni ya wanachama na si Mwenyekiti wake Freeman Mbowe au Katibu Mkuu, Wilbroad Slaa.

Akifungua Kongamano la Baraza Kuu la Vijana wa Chadema(BAVICHA) Kanda ya Dar es Salaam, Kaimu Katibu Mkuu wa chama hicho, John Mnyika alisema kuanzia mwaka 2004 kwa nyakati tofauti wamekuwa wakikumbana na masuala kama hayo lakini yamekuwa yakimalizika bila kukiathiri chama.

Alisema hata kuondolewa kwa maofisa katika chama hicho si jambo la ajabu la kusababisha shutuma mbalimbali ambazo hawakuwahi kuzitoa awali wakiwa ndani ya chama.

"Hata Mzee Halimoja aliondolewa na hapakutokea malumbano ya aina hiyo hivyo kuna msukumo fulani ili kuyumbisha chama, jambo ambalo wanachama hatudanganyiki kukigawa chama.

"Propaganda zinazoendeshwa baina ya chama chetu kudaiwa kutaka kuwaondoa vijana katika ngazi za uongozi si za kweli hivyo tunawataka wale wanaotoa shutuma mbalimbali kwa chama hicho kuwasilisha vielelezo na siyo kuropoka kama vichaa," alisema.

Alidai kwamba chama hicho kimekuwa kikitoa nafasi mbalimbali kwa vijana na hakuna mpango wa kuwaondoa vijana kwani waanzilishi wake walistaafu ili kuwaachia vijana nafasi.

Hivi karibuni wanachama wawili wa chama hicho, David Kafulila na Danda Juju, walijivua uanachama wa Chadema.

Kafulila ambaye alikuwa Ofisa Habari wa Chadema, amejiunga na NCCR-Mageuzi.

Juju hajasema chama anachohamia. Alisema fedha zinazopatikana kwa njia ya ujumbe mfupi (SMS) zinaingia katika akaunti za kawaida za chama na hazina usiri wa aina yoyote.

Aliendelea kusisitiza kwamba wako tayari kukaguliwa mapato yake na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwani chama hicho kimekuwa kikikaguliwa hesabu zake kila mwaka na kupata hati safi.

Katika hatua nyingine, Chadema kimemuomba Rais Jakaya Kikwete iwapo atashinda uchaguzi ujao, ateue vijana wenye sifa za uongozi .

Aliwataka vijana kutumia kongamano hilo kukosoa na kujadili masuala mbalimbali yahusuyo mwelekeo wa chama kwa kufuata maadili kwani wao ni walinzi wa chama na yeyote atakayeenda kinyume cha Chama achukuliwe hatua kwani bila kufanya hivyo chama kitakuwa kimefilisika kimaadili.

Aliwasihi kujadili mustakabali wa chama hicho hasa katika kipindi hili ambacho taifa linatarajia kuadhimisha miaka 48 ya uhuru.

Aliwapongeza viongozi wa jimbo la Dar es Salaam kichama kwa kufanikiwa kupata viti 14 katika uchaguzi wa serikali za mitaa tofauti na viwili walivyokuwa navyo.

Awali, Ofisa wa VIjana Taifa, Ali Chitanda alisema kongamano hilo la siku moja linawashirikisha wajumbe kutoka kata 50 katika jimbo la Dar es Salaam.

Watapata fursa ya kujadili kuhusu matokeo ya uchaguzi wa serikali za mitaa na ushirikishwaji wa vijana katika uchaguzi mkuu ujao.

Kutoka: http://www.habarileo.co.tz/kitaifa/?n=4601
 
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesema propaganda na shutuma mbalimbali zinazoendelea katika chama hicho wamezizoea na haziwatingishi kwani watazimaliza katika vikao vya chama.

Kimedai kwamba hali kama hiyo imekuwa ikitokea mara kwa mara kunapokaribia uchaguzi mkuu, kwani Chadema ni ya wanachama na si Mwenyekiti wake Freeman Mbowe au Katibu Mkuu, Wilbroad Slaa.

Akifungua Kongamano la Baraza Kuu la Vijana wa Chadema(BAVICHA) Kanda ya Dar es Salaam, Kaimu Katibu Mkuu wa chama hicho, John Mnyika alisema kuanzia mwaka 2004 kwa nyakati tofauti wamekuwa wakikumbana na masuala kama hayo lakini yamekuwa yakimalizika bila kukiathiri chama.

Alisema hata kuondolewa kwa maofisa katika chama hicho si jambo la ajabu la kusababisha shutuma mbalimbali ambazo hawakuwahi kuzitoa awali wakiwa ndani ya chama.

“Hata Mzee Halimoja aliondolewa na hapakutokea malumbano ya aina hiyo hivyo kuna msukumo fulani ili kuyumbisha chama, jambo ambalo wanachama hatudanganyiki kukigawa chama.

“Propaganda zinazoendeshwa baina ya chama chetu kudaiwa kutaka kuwaondoa vijana katika ngazi za uongozi si za kweli hivyo tunawataka wale wanaotoa shutuma mbalimbali kwa chama hicho kuwasilisha vielelezo na siyo kuropoka kama vichaa,” alisema.

Alidai kwamba chama hicho kimekuwa kikitoa nafasi mbalimbali kwa vijana na hakuna mpango wa kuwaondoa vijana kwani waanzilishi wake walistaafu ili kuwaachia vijana nafasi.

Hivi karibuni wanachama wawili wa chama hicho, David Kafulila na Danda Juju, walijivua uanachama wa Chadema.

Kafulila ambaye alikuwa Ofisa Habari wa Chadema, amejiunga na NCCR-Mageuzi.

Juju hajasema chama anachohamia. Alisema fedha zinazopatikana kwa njia ya ujumbe mfupi (SMS) zinaingia katika akaunti za kawaida za chama na hazina usiri wa aina yoyote.

Aliendelea kusisitiza kwamba wako tayari kukaguliwa mapato yake na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwani chama hicho kimekuwa kikikaguliwa hesabu zake kila mwaka na kupata hati safi.

Katika hatua nyingine, Chadema kimemuomba Rais Jakaya Kikwete iwapo atashinda uchaguzi ujao, ateue vijana wenye sifa za uongozi .

Aliwataka vijana kutumia kongamano hilo kukosoa na kujadili masuala mbalimbali yahusuyo mwelekeo wa chama kwa kufuata maadili kwani wao ni walinzi wa chama na yeyote atakayeenda kinyume cha Chama achukuliwe hatua kwani bila kufanya hivyo chama kitakuwa kimefilisika kimaadili.

Aliwasihi kujadili mustakabali wa chama hicho hasa katika kipindi hili ambacho taifa linatarajia kuadhimisha miaka 48 ya uhuru.

Aliwapongeza viongozi wa jimbo la Dar es Salaam kichama kwa kufanikiwa kupata viti 14 katika uchaguzi wa serikali za mitaa tofauti na viwili walivyokuwa navyo.

Awali, Ofisa wa VIjana Taifa, Ali Chitanda alisema kongamano hilo la siku moja linawashirikisha wajumbe kutoka kata 50 katika jimbo la Dar es Salaam.

Watapata fursa ya kujadili kuhusu matokeo ya uchaguzi wa serikali za mitaa na ushirikishwaji wa vijana katika uchaguzi mkuu ujao.
 
Monday, 30 November 2009 07:51 Na Elisante Kitulo

SIKU chache baada ya maafisa wawili wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kutenguliwa nyadhifa zao na kujivua uanachama, chama hicho kimeibuka na kupinga madai kuwa kinawaengua vijana kushika nyadhifa za uongozi na kudai hizo ni propaganda za CCM kukichafua.

Akizungumza Dar es Salaam jana katika Kongamano la Baraza la Vijana wa Chadema (BAVICHA), Kaimu Katibu Mkuu CHADEMA,Bw. John Mnyika alisema kuwa propaganda hizo zinaenezwa na CCM kwa nia ya kukichafua chama chake ili kikose imani kwa Watanzania.

Alisema wakati huu ambapo nchi inajiandaa kuingia katika uchaguzi mkuu hapo mwakani, mengi yatasemwa kuhusu chama chake ili kuonesha kuwa kuna mpasuko kama ilivyo kwa CCM, hasa ukizingatia kuwa CCM imefilisika kimaadili na hivyo kuingiwa na hofu ya kushinda katika uchaguzi ujao.

"Chadema ni chama cha kizazi kipya, sisi ndio tulioanzisha kaulimbiu ya 'vijana ni taifa la leo' na si kesho kama ilivyokuwa awali, sasa iweje tulaumiwe kwa kuwatenga vijana wakati ndio chama pekee chenye asilimia 30 ya wabunge vijana, hizo ni propaganda tu," alisema.

Alisema kuwa propaganda hizo zimeibuka baada ya kutenguliwa nyadhifa kwa waliokuwa maafisa wawili wa chama hicho kutokana na kwenda kinyume cha maadili ya chama.

Kwa mujibu wa Bw. Mnyika, si kila kijana anaweza kuongoza na kuwa wakati mwingine ni bora kuwa na waziri mzee kama Dkt. Slaa kuliko kuwa na mawaziri vijana kama waliopo sasa ambao hawawezi kuongoza wizara.

Aidha, Bw. Mnyika ameonesha wasiwasi kutokana na kauli ya CCM kutumia bilioni 40 katika uchaguzi mkuu ujao na kukitaka chama hicho kitoe mchanganuo wa mapato na matumizi ya pesa hizo.

Alisema mwaka 2005 Rais Kikwete alichangisha pesa kupitia harambee kwa madai kuwa ni pesa safi kumbe za mafisadi wa EPA, na kuongeza kuwa kama kweli CCM imedhamiria kukusanya pesa safi katika uchaguzi ujao ni vyema ikawachukukulia hatua watuhumiwa wote wa waliopora fedha za EPA, hasa kampuni ya Kagoda.

"Si busara kutumia shilingi bilioni 40 katika uchaguzi ambazo ni sawa na kutumia milioni 200 kwa kila jimbo wakati ambapo wakina mama wajawazito wanakufa kwa kukosa huduma nzuri wakati wa kujifungua," alisema.

Akizungumzia tuhuma za matumizi mabaya ya fedha za ruzuku Bw. Mnyika alisema CHADEMA imekuwa ikipata hati safi kila mkwaka na kuongeza kuwa Baraza Kuu la chama hicho lilishatoa mapendekezo kuwa mahesabu ya vyama vya siasa yakaguliwe na Mkaguzi Mkuu na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali (CAG).

"Kwa kuwa Dkt. Slaa aliwataja mafisadi na Zitto Kabwe ambaye anaendesha mapambano dhidi ya mafisadi anatoka CHADEMA, sasa wanataka kukifanya chama kionekane cha mafisadi ili kuwachanganya wananchi," alisema.

Alisema kuwa mtu yeyote mwenye tuhuma za msingi za ufisadi dhidi ya chama chake, atoe mchanganuo wa ufisadi huo kama ambavyo CHADEMA ilifanya kwa mafisadi wa CCM.

Katika kongamano hilo ambalo linahusisha vijana 50 kutoka katika mikoa ya kichama ya Ilala, Temeke na Kinondoni, vijana hao walijadili taarifa za uchaguzi wa serikali za mitaa na kupanga mikakati ya Uchaguzi Mkuu ujao.

Katika hatua nyingine, Grace Ndossa anaripoti kuwa
Bw. Mnyika amesema chama hicho hakiongozi kwa ukabila wala siyo cha mtu binafsi kama inavyoelezwa bali kinafuata taratibu, sheria na kanuni za siasa.

Bw Mnyika aliyasema hayo wakati akizungumza katika kipindi cha Mambo Leo kinachorushwa na Radio Times ya jijini Dar es Salaam.

Alisema kuwa watu wengi wamekuwa na fikira potofu kuwa chama ni cha mtu binafsi ambaye kinaongozwa kwa matakwa yake kitu ambacho siyo kweli wala hakiongozwi kwa ukabila.

Alisema kuwa ndani ya chama hicho kuna watu wa makabila mengi katika nafasi za uongozi na kwamba, wanaosema kinamilikiwa na wachaga wanakionea.

"Tumekuwa tukipata malalamiko mengi kuwa CHADEMA ni chama cha mtu binafsi, siyo kweli. Hii ni taasisi inayoshughulika na mambo ya siasa na ni chama makini ambacho hakipendelei mtu wala kutazama kabila wala dini, tunafanya kazi za kusaidia jamii," alisema Bw. Mnyika.

Alisema kuwa CHADEMA kiko salama na kitaendelea na oparesheni sangara nchi nzima ili kiweze kuwa na watu wengi na wamejipanga kushinda uchaguzi wa mwakani.

Chanzo: Gazeti la Majira
 
Ingekuwa vizuri akitwambia kuwa chama chake kazi yake ni usindikizaji. Anatabiri ushindi kwa Kikwete kwa kipi alichofanya kwa vijana? kuwateua wawili au watatu kuwa mawaziri?

Ana hakika gani kuwa CCM itampitisha kuwa mgombea wake? au na yeye amenunuliwa kuanza kumpigia debe JK? au kuwa mpiga debe wa CCM
 
Mpe ushauri wote halafu uone ni lini Chadema wataingia madarakani.Hivi nyie upinzani mnauchukuliaje? CCM hawakuhusu kwa lolote lile! mnajikomba nini kule ? we are tired of CCM na wewe mnawapawapa ushauri ili msiingie madarakani!

Wapinzani wetu bwana!
 
Hakuna direct quote,

Yaani muandishi anafanya kitu headline halafu hakiwekei direct quote, ila upupu mwingine kibao kauwekea direct quotes. What should I gather from this?

Nikisema sijaridhika kwamba Mnyika kasema maneno hayo yaliyo katika headline mtanishangaa?

Nikifikiri habari imepindishwa kisiasa ili Mnyika aonekane amesema ambacho hajasema nitakuwa nime stretch mambo?

Kulikuwa na kazi gani kutupa a word by word account of what Mnyika said about Kikwete, instead of paraphrasing and posibly corrupting his words?

Katika environment yetu ya uandishi na siasa zetu uchwara nitakuwa nakosea nikiwa siiamini hii article?

I mean hata hiyo indirect quote yenyewe haisemi kwamba Mnyika ametabiri Kikwete atashinda.

Katika hatua nyingine, Chadema kimemuomba Rais Jakaya Kikwete iwapo atashinda uchaguzi ujao, ateue vijana wenye sifa za uongozi .

Hivi hiki kichwa cha habari kina tofauti gani na kile kinachosema "Rais ampiga mkewe" halafu ukifungua habari unakuta kumbe rais wa chama cha ndondi kampiga mkewe uswahilini kwetu huko?

Pengine hata hiyo habari ya rais inaweza kuwa na afadhali.

Where is our journalistic integrity?
 
Jahazi linazama hilo jamani nyie kaeni na ubishi wenu mficha ugonjwa mauti humfichua....

Chama si watu watatu chama ni taasisi, hata wakiondoka wote na ka group kao sisi tunasonga mbele tu. tatizo la watanzania ndo hilo kudhani ka kikundi kadogo kanaweza kuwa threat kwa chama, hilo wazo lazima lishidwe kabisa.
 
WAACHE WAONDOKE, wasigeuke nyuma.
 
Nilisema,hawakunisikia.nilihubiri,hawakuniamini..
sasa wanalia, eti wanataka niwafute machozi!!

not every ant-CCM is patriotic citizen.most of opposition politicians are MAFISADI.
FREEMAN MBOWE is the gangstar of the gang of fake politicians.
 
Too personal and too low for Notradammus(Sic)
 
kazi nzuri bwana kingunge kwani ndo hswa jukumu lake ndani ya ccm, hawataki upinzani at the same time hawafanyi kazi nzuri duh ndo nchi letu tunaburuzwaaa! ukiuliza unambiwa nyien wtz mnalalamika sana hamfanyi kazi so kwa mazingira yapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…