Chachu Ombara
JF-Expert Member
- Dec 11, 2012
- 6,067
- 10,938
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) John Mnyika akizungumza na wanahabari mchana wa siku ya Jumamosi Septemba 7, 2024 Makao Makuu ya CHADEMA, Dar es Salaam amesema kuwa...
“Kwa aina ya bunduki walizokuwa nazo hao watu waliokuja kumchukua (Mzee Ally Mohamed Kibao ambaye ni mjumbe wa sekretarieti ya chama taifa (CHADEMA)) kwenye basi si bunduki ambazo kwa kawaida hutumiwa na Jeshi la Polisi, ni bunduki ambazo hutumiwa na Idara ya Usalama wa Taifa.
Wakati tukifuatilia taarifa zaidi na wakati tukijiandaa kuchukua hatua zaidi kuja kwenye vyombo vya habari kueleza tu kwamba kiongozi wetu na mwenzetu ametekwa na vyombo vya ulinzi na usalama, nitoe wito kwa IGP wa Jeshi la Polisi Mkuu wa Jeshi la Polisi kueleza iwapo Ally Kibao ametekwa na Jeshi la Polisi, waeleze sababu za kumteka, yupo wapi, na ana hali gani.
Kwa kawaida huwa tunajizuia sana kuzungumza kuhusu Idara ya Usalama wa Taifa lakini kwa sheria ya idara ya Usalama wa taifa kuna mtu mmoja tunaweza tukamtaja na tunaweza kumzungumza, Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa natoa wito kwake ajitokeze aeleze iwapo idara ya usalama wa taifa imemteka Mzee Ally Mohammed Kibao, yuko wapi?
Pia soma
- Kiongozi wa Madaktari (Dr. Ulimboka) atekwa, aokotwa akiwa katika hali mbaya sana