Uchaguzi 2020 CHADEMA na ACT, mkishindwa kuwa kitu kimoja na kuachiana majimbo mtawafaidisha CCM

Ni kweli, lakini kutoshiriki inaweza kuwa ni hasara zaidi kisiasa kwa hivi vyama.

Mkuu mimi bado msimamo wangu uko palepale, bila tume huru ya uchaguzi ni kupoteza Muda. Nilitarajia wapinzani kila wakisimama ni kuiponda tume, hadi tume ipoteze kujiamini na isiwe katika mazingira rahisi ya kuibeba ccm. Lakini naona wanaongelea uchaguzi tu, huku wakiiacha tume kama chombo sahihi cha kusimamia uchaguzi. Hii ya kuachiana sehemu uko sahihi, lakini kwa tume hii, hata chama kimoja kikijitoa na wanachama wake wote waende chama kimoja, bado hakuna lolote litakaloendelea.
 
Huu muungano kwenye kura za urais na mgombea urais ndipo penye walakini.

Kiukweli kwangu Membe sioni influence yake kabisa ukiacha hiyo mikoa ya kusini, sasa kipi bora;

(a) Kumsimamisha Membe asaidie wagombea ubunge mikoa ya kusini ambayo hatuna uhakika kama kweli ana hiyo influence?

Au

(b) Chadema imsimamishe mgombea urais wake ambae inaamini anaungwa mkono na kundi kubwa la watu Tanzania nzima kwa ujumla, na sio kanda fulani pekee?

Mleta mada umejaribu kusisitiza kwenye umoja ni vizuri, lakini pia tuangalie kwa jicho la pili nguvu za wagombea hasa wa Urais kutoka vyama vyote viwili, tusilazimishe tu bora fulani ana jina basi apewe hiyo nafasi, napenda hapa tutazame zaidi nguvu/uungwaji mkono wa wagombea wa hivyo vyama viwili.
 
Wewe ni mpiga debe tu wenye saccos wapo busy na watashiriki
Who are you?
 
Hawa wapinzai syo wakuwaamin kabisa ile 2015 walipoteza majimbo na kata kadhaa kwa uroho wao wa fedha na wakutoshiriana .
 
👏🏽👏🏽👏🏽👏🏽👏🏽👏🏽👏🏽👏🏽👊🏽👊🏽👊🏽
Wanataka kurudia kosa lile lile la 2015 Chadema walipomkaribisha fisadi lowassa. Fool me once shame on you, fool me twice shame on ME.

Huu muungano umeingia shubiri Mara baada ya zitto kumtamani mwanachama Wa ccm aje aokoe jahazi LA kugombea urais kupitia Act kisha muungano huo.Zitto kwa hili kapotoka sana, membe aweza karibishwa upinzani ila sio kwa kugombea urais.
 
Nashauri ACT-WAZALENDO wasiwaamini hawa cdm wawaulize cuf walichofanyiwa 2015 jimbo la ukonga!!
 
Kwa mtazamo wangu,kwenye uraisi wamsimamishe Lissu na huyu Membe anaweza kutumika kumpigia kampeni katika hiyo mikoa ya kusini na kwingineko anakoweza kusaidia ila sio kuja kugombea uraisi kupitia upinzani.Hamahama imeshawavunja moyo wananchi na itakuwa kosa kubwa zaidi kurudia kitu kile kile hasa kipindi hiki cha kuelekea kwenye uchaguzi.
 
Yes, especially ACT wakimsimamisha mgombea visiwani, basi Chadema wasimamishe mgombea bara.
 
Yes, especially ACT wakimsimamisha mgombea visiwani, basi Chadema wasimamishe mgombea bara.
Sasa CHADEMA nao wanasimamisha mgombea uraisi huko Zanzibar na teyari mmoja kashachukua fomu kama hiyo picha hapo juu kwenye mada inavyothibitisha.

Tatizo naloliona ni kila chama kina nia ya kujijenga bara na visiwani hivyo wanaona kutoshiriki ni kudumuza vyama vyao bila kujali watashinda au laa wakiamini kitendo cha kushiriki tu katika hizi chaguzi kinasaidia kujenga uhai wa chama hata kama hawatashinda.
 
Tuliwambia humu mkakaza shingo! Asiyesikia la mkuu huvunjika guu, sasa baada ya kuvunjika ndio akili zinawarudi,

Same kwa Mashinji tukiwaambia huyo jamaa hafai, bado mkajifanya much know,,
Yani nyie hat muwekewe kujifunza kwa picha hamuwezagi kuelewa kamwe

Sent from my SM-T585 using JamiiForums mobile app
 
Together we shall overcome
 
iseeee
 
Huu muungano umeingia shubiri Mara baada ya zitto kumtamani mwanachama Wa ccm aje aokoe jahazi LA kugombea urais kupitia Act kisha muungano huo.Zitto kwa hili kapotoka sana, membe aweza karibishwa upinzani ila sio kwa kugombea urais.
Yameshatimia sasa kwa Membe kujiunga ACT.
 
Kwa tume hii ya uchaguzi ni ngumu sana kutoboa!!!...Sijui kwa nini mnajisahaulisha

Kwa tume hii hii kusingetokea mtafaruku wa kipandikizi tokea kwa kina lipumba na mwenziwe slaa jiwe asingetoboa.

Hivyo hivyo bila mwungano Malawi, Mutharika angekuwa bado rais kule.

Mwungano kwanza mambo ya tume yanaweza rekebishika baadaye.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…