Uchaguzi 2020 CHADEMA na ACT, mkishindwa kuwa kitu kimoja na kuachiana majimbo mtawafaidisha CCM

Huu muungano umeingia shubiri Mara baada ya zitto kumtamani mwanachama Wa ccm aje aokoe jahazi LA kugombea urais kupitia Act kisha muungano huo.Zitto kwa hili kapotoka sana, membe aweza karibishwa upinzani ila sio kwa kugombea urais.
Membe ndo pekee anaeweza kumpa pressure magu... Kumbuka huyu anajua mbinu zote za kuingia ikulu
 
Kususia hakusaidii kitu. Sheni amemaliza muhula wake bila shida yeyote baada ya CUF kumsusia. Wenyeviti wa Mitaa nao hao wanaendelea kufanya kazi zao bila matatizo yeyote. Ni busara zaidi wapinzani kushiriki uchaguzi ili kama watafanyiwa figisu figisu wawe na ushahidi kamili. Aidha, makubaliano ya kushirikiana si lazima yawekwe hadharani.

Amandla...
 

Zanzibar ni sawasawa na uchaguzi wa ndani, na SM za mitaa ni uchaguzi wa ndani, hauna impact kama uchaguzi mkuu. Wenyeviti wa mitaa wanafanya kazi zao kama kawaida, lakini hawana ushirikiano wanaopaswa kuwa nao. Mimi mtaani kwangu mwenyekiti wa mtaa hata akiitisha mkutano anajikuta na wanaccm wachache, na amekuwa akilalamika kuwa hapati ushirikiano wa wananchi kisa wananchi wanaendelekeza siasa.

Kwenye uchaguzi huu kama watu watahamasishwa kwenda na silaha za jadi hapo nitakuelewa, ila sio hiyo kwenda kama wanaenda kwenye nyumba ya ibada.
 
Hatujafikia kwenye mambo ya silaha za jadi. Watu wataumia bure.

Amandla...
 
Hatujafikia kwenye mambo ya silaha za jadi. Watu wataumia bure.

Amandla...

Watu wapi wataumia bure, maana kama ni wapinzani ni wahanga wa vipigo toka kwa vijana wa ccm, tena kwa uratibu wa jeshi la polisi. Inaonekana unazungumza jambo ambalo hujalifanyia uchunguzi vizuri. Wapinzani wengi wamepata vilema toka kwa makundi ya ccm, na tabia hiyo imefanyika kwa uwazi zaidi toka awamu hii ya tano imeingia madarakani. Kwa macho yangu nimeona mgombea wa cdm wa udiwani akipigwa vibaya na vijana wa ccm, huku polisi wakiangalia, na kisha mgombea huyo wa cdm ndio akafungiliwa mashitaka ya kutaka kuharibu uchaguzi!

Kwa macho yangu nimeshuhudia mawakala wa cdm wakipigwa na jeshi la polisi ili wasaini fomu fake za matokeo, ili mgombea wa ccm atangazwe mshindi. Nilishuhudia kwa macho yangu kupitia kituo cha ITV, mabox ya kura yakitolewa vituoni kwenda kujazwa kura za ccm, na haya yote yalifanyika mbele ya polisi na msimamizi wa uchaguzi! Na huu ndio uliokuwa mwenendo kwenye chaguzi zote za marudio. Funga kazi ilikuwa ni ule ushenzi tulioushuhudia kwenye uchaguzi wa SM. Hapa unataka watu waende kushiriki bila silaha za jadi ili iweje labda?
 
Hiyo sio haki na inasikitisha kwa kweli. Hata hivyo silaha za jadi mbele ya silaha za moto ni collective suicide kwa kusema kweli. Na wabaya wenu watajitetea kuwa walikuwa wanajihami dhidi ya mashambulio yenu. Umwagaji damu hausaidii hata siku moja.

Amandla...
 

Mkuu nimesema mwanzo nilisema kuhusu kutokushiriki uchaguzi kwasababu najua kinachoendelea. Ukanionyesha kutokushiriki ni kosa, kwani mambo yatasonga na kutakuwa hakuna ushahidi wa kudhulumiwa. Nikakuambia kama ni kushiriki basi wapinzani waende na silaha za Jadi. Ukanaonyesha kuwa hatujafikia huko. Moja kwa moja nikajua unaongea usichokijua. Nikakupa vitu ambavyo nina ushahidi navyo kwa uchache. Sasa naona umepata mwanga wa kinachoendelea, unaogopa umwagaji wa damu!

Kwa hapa tulipofika machafuko pekee ndio yatarudisha box la kura kuheshimiwa, au tusubiri rais huyu atoke, kwani yeye ndiye sababu ya yote haya. Ila uzoefu unaonyesha ili kuheshimiana kuwepo, au uhasama ushike kasi vizuri, machafuko pekee na umwagaji damu ndio suluhisho. Nimezungumza jambo zito kidogo, lakini ndio dawa, na iwapo kutatokea machafuko, hata mabadiliko ya tume ya uchaguzi, na katiba mpya yatapatikana.
 
Ili membe nimwamini asigombee urais. Awe mwanachama tu.
 
Acha kujitia woga wewe. Lazima tuwalaze kama 20 hivi hata kama sisi tutakufa 1000
 
Umefanya very deep analysis....ila shortly, Chadema haichomoki bila ACT ....Mbowe akikaza shingo utaniambia hapa mwezi November ...[emoji41]
 
Mimi ni mpinzani kindaki ndaki lakini upuuzi wa kugombea Membe bora nipigie kampeni huu ushetani wa awamu ya tano. Membe ni shetani zaidi.
 
Zile picha za 2015 za Zitto kumbeba punda (ACT) mgongoni zimepitwa na wakati. CDM na ACT fanyeni muungano wa aina yoyote ile, hakuna yeyote kati yenu anaweza kuitoa CCM madarakani kwa kujitenga. CDM toeni mgombea uraisi wa bara, ACT watoe mgombea uraisi wa visiwani, Membe kama kweli ni mpenda haki ataingia upinzani bila kung'ang'ania uraisi.
 
Tume sidhani kama itakuwa mpya kabla ya uchaguzi. Lakin mkisusia wanakula kuna cuf na kina mrema wapinzani feki. Wataingia uchaguzi na sisyem. CDM na ACT waamue wanamsusia nguruwe shamba la mihogo au wanapambana huku wakidai tume.

Serikali za mitaa walisusa, uchaguzi wa marudio Zanzibar walisusa, chaguzi ndogo za marudio walisusa, nini kimetokea au kubadilika? Asiye na haya mkabili kwa namna inayomstahili.
 
Membe mwenyewe hata akikohoa hatusikii .
Na kwa vyombo hivi vya habari hata afanye propaganda gani hatitosikia sauti yake.
Kama ningekuwa mshauri wake ningemuomba afuge,alime bamia kama assad na ale pension yake aliyoisotea kwa zaidi ya miaka 30 ya utumishi.
 
Kwani mpaka sasa ACT ina majimbo mangapi? usisahau jimbo la jf wakati wa kuhesabu
 
Mleta mada ni ACT anaomba ajira CDM, yaani hata cdm ikisusia uchaguzi act haiwezi kutoboa labda jimbo la jf
 
Huu muungano umeingia shubiri Mara baada ya zitto kumtamani mwanachama Wa ccm aje aokoe jahazi LA kugombea urais kupitia Act kisha muungano huo.Zitto kwa hili kapotoka sana, membe aweza karibishwa upinzani ila sio kwa kugombea urais.
Majanga aliyosababisha Lowasa na Genge lake Chadema wabaki wenyewe majira yatapita na maisha yataendelea hii kuwapokea wanaccm kwa harisa zakukataliwa huko kwao badae akili zikiwatulia wanarudi huko tena kwa kashfa kubwa kwa vyama pinzani hii haikubaliki
 
Ndugu MEMBE hana kundi lolote analokwenda nalo ACT labda wapiga kura wa Jimbo la Mtama tu! kama Lowasa hakuwa na kundi lolote pamoja na ushawishi aliokuwa nao wapi Membe atakuja na kundi
 
Huu ndio ukweli nami nawaunga mkono Chadema kwaasiilimia zote! Membe akienda ACT akawe msaada wa kukuza upinzani sio aje kwaajili yakugombea uRAIS hapana this time vyama vitumie wagombea wao sio wakuazima manake bila hivyo itakuwa kila mwaka huko ugambani wanavurugana huku wanafanya mahali pakupumzikia
 
Ndugu yangu unadhani kuisema tu inatosha?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…