Uchaguzi 2020 CHADEMA na ACT, mkishindwa kuwa kitu kimoja na kuachiana majimbo mtawafaidisha CCM

Membe hana ushawishi wowote zaidi ya wapiga Kura wachache pale Mtama na wengi wao kule ni ccm kumbuka Nape atagombea pia
 
siku zote umoja ni nguvu ila haiwezekani kupata umoja wa vyama vya upinzani kwa nchi maskini , yenye watu wenye njaa na iliyoharibiwa mfumo wake wa elimu kwa kujazwa siasa ya kipumbavu ya ujamaa na kujitegemea my foot!

Muungano wa watu maskini huwa ni wa muda, wenye mashaka, huwa ni wa kinafki , wa kibinafsi na wa kimaslahi zaidi, na katika hali hii ngumu ya kiuchumi wanasiasa wanapopigania matumbo yao ni ngumu mno kwa wao kuungana!

ila itapendeza mno kama Membe ataenda ACT akajijenge kisiasa na kuanza safari ya kuutafuta urais. Huyu mzee namshangaa kwanini hatangazi kujiunga upinzani na muda unakwenda sababu sisiem hawamtaki ni mtu asiekubali baadhi ya taratibu za chama

kwa akili zangu naamini tukiangalia haki tu bila kuhusa mengine Membe kafukuzwa sisiem bila kosa lolote, kudai kwake demokrasia ndani ya chama kwa kutaka kumchallenge boss wao kumemponza!

asichokijua Membe ni kuwa alikuwa katika genge lenye watu wengi wenye local education sasa yeye vile kwenda kwenda ulaya akadhani na wenzake wana akili ya kizungu kumbe hola, wote ni wa hapa hapa wenye mawazo mgando ya zidumu fikra za mwenyekiti!!
 
Huu muungano umeingia shubiri Mara baada ya zitto kumtamani mwanachama Wa ccm aje aokoe jahazi LA kugombea urais kupitia Act kisha muungano huo.Zitto kwa hili kapotoka sana, membe aweza karibishwa upinzani ila sio kwa kugombea urais.
Anzisha chama chako bro Lungwe
 
Chadema na ACT hawawezi kabisa kushirikiana,kutokaba na historia ya vyama hivyo,wanachoweza kufanya ni kuishi kwa kuvumiliana,na kuukubali ukweli kuwa kwao kushirikiana ni kama mbingu na ardhi
 
Wewe Salary Slip ni mchumia tumbo tu, unataka Chadema waunge mkono mtoto wa shetani kuwa mgombea wa urais ?

Membe hana ushawishi wowote wa kisiasa zaidi ya kuwa mpiga kelele tu unafikiri kusini Membe anaushawishi kuliko wale wanacuf walioinyanyasa ccm mwaka 2015?

Unataka CHADEMA yenye wanachama millions kadhaa iwaachie ACT ambayo haina hata wanachama hivi unaakili kweli wewe ? Unajua jasho walilotumia CHADEMA kujenga chama waje wajiue kwa kukijenga ACT kwa mikono yao wenyewe?

Kama mnampenda Membe mfuateni huko ACT tuachieni CHADEMA kama hatuna mgombea tutamsimamisha mwanachama yeyote siyo Membe.
 
Lissu anakuja tarehe 28 July
 
Huu ndio ukweli ndugu
 
Membe hana “kundi kubwa la wanaCCM”. Ile ya Lowassa ilikuwa exceptional. Atapata shock kubwa. Just wait and see. Now that wanaCcm wanajua modus operandi ya JPM (mzee wa visasi bila kupoteza muda), hakuna mwanaCCM serious anayeweza kujitokeza hadharani na kumfuata Membe huko anakotaka kwenda.

Hongera CHADEMA kwa kuepuka makosa ya mwaka 2015. Hata Zitto analijua hilo ila anafanya kubahatisha tu atleast aokote majimbo kadhaa
 
Membe huyu alikuwa mwizi kama wengine na hakuwahi kusaidia kupata hiyo tume huru anayoisema. Leo bila aibu anapretend kuimba nyimbo mnazozipenda na baadhi ya watu wanaanza kumpigia makofi na mnamuona kama vile ni mkombozi wa wapinzani

Hatari sana!
 
Huu muungano umeingia shubiri Mara baada ya zitto kumtamani mwanachama Wa ccm aje aokoe jahazi LA kugombea urais kupitia Act kisha muungano huo.Zitto kwa hili kapotoka sana, membe aweza karibishwa upinzani ila sio kwa kugombea urais.
Unafikili Zitto angefanyaje wakati Bernard Membe alikuwa na hisa ndani ACT Wazalendo tangia kuanzishwa kwake.
 
Membe huyu alikuwa mwizi kama wengine na hakuwahi kusaidia kupata hiyo tume huru anayoisema. Leo bila aibu anapretend kuimba nyimbo mnazozipenda na baadhi ya watu wanaanza kumpigia makofi na mnamuona kama vile ni mkombozi wa wapinzani

Hatari sana!
Ndiyo unafiki wa wanasiasa wa ccm kazi yao kubwa ni kutafuta fursa ya kuiba Mali za umma tu.
 
We lofa kabila!Uwezo wake wa kuelewa kilichoandikwa ni mdogo sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…