Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
CHADEMA na ACT-WAZALENDO: Hoja 7 Zinazowafanya Watanzania Wasiwe Tayari Kumwaga Damu kwa Kuandamana.
Vyama vya CHADEMA na ACT- Wazalendo vimekutana na kuwaambia waandishi wa habari eti kuanzia jumatatu wataanza maandamano yasiokuwa na kikomo kwa kile walichodai eti kuibiwa kura katika Uchaguzi uliofanyika Oktoba 27-28, 2020.
Maandamano hayo yasiyo halali wamepanga kuyafanya Tanzania Bara na Tanzania Visiwani.
Makala hii baada ya kufanya utafiti katika pande mbili za Muungano, bara na visiwani, inafafanua sababu za watanzania kutojihusisha na maandamano ya CHADEMA na ACT- Wazalendo.
Hoja ya kwanza:
Watanzania ni watu wa amani. Hawataki kupoteza amani iliyoasisiwa na wazee wa Taifa hili chini ya Mwalimu Julius Nyerere na Mzee Abeid Amani Karume.
Hoja ya pili:
Watanzania walishiriki kupiga kura na kuchagua washindi wa uchaguzi kwa ngazi zote za urais, udiwani na ubunge kwa hiyo hawaoni kwa nini waandamane wakati wao ndio waliowachagua washindi.
Hoja ya tatu:
Maendeleo. Watanzania wote kwa sasa wanaendelea na shughuli zao za maendeleo na maisha ya kila siku yanaendelea vizuri na kuwafanya wapate mkate wao wa kila siku. Kwa mantiki hii maandamano hayatawalisha chakula na walishamaliza uchaguzi.
Hoja ya nne:
Watanzania kwa sasa wameshajua kuwa CHADEMA na ACT- Wazalendo wana ajenda za kuuza rasilimali za nchi kwa mabeberu kwa hiyo hawako tayari kuuzwa nchi yao na utu wao.
Hoja ya sita:
CHADEMA na ACT- Wazalendo kukosa wagombea wenye mvuto na sera za maendeleo. Wagombea kama Babu Seif na Tundu Lissu wote ni wachumia tumbo na makuwadi wa mabeberu. Hawa sio chaguo la Watanzania.
Hoja ya saba:
Watanzania wenyewe wameamua kuchagua maendeleo sio vurugu. Baadhi ya maendeleo hayo ni upatikanaji wa maji, umeme, barabara na mengine mengi wameshayafaidi kwenye muhula wa kwanza wa Rais Magufuli. Kwa mantiki hiyo hawahitaji majaribio ya uongozi wakati asali wameanza kuiramba.
Badala ya CHADEMA na ACT- Wazalendo kuhamasisha umwagaji damu katika taifa huru la Tanzania, watumie muda huu kujitathimini kwa nini hawakuchaguliwa na wananchi. Waache mihemko kwani damu waliyopanga kuimwaga haitawaacha salama.