mwanamakambako
JF-Expert Member
- Jan 3, 2014
- 780
- 120
Hahahaaa wallah umenifanya nicheke bila chuki.Mkuu, utaambiwa una KAHIDI....
tatizo watu wanachukulia sheria kama quruan au biblia, unapowataka wanachama wasishiriki mikutano ya zitto wkt zitto bado anajulikana ni mwanachama halali wa chadema ambaye ana haki ya kufanya mikutano kupitia uanachama wake tayari lile zuio linahusu uanachama wa zitto kuzuiwa kupitia haki yake ya kufanya mikutano ka mwanachama wa chadema.tayari wamekaidi amri ya mahakama,mtasikia kesho
sasa nani asiyejua kwamba kuna mgogoro kati ya zitto na cdm ? Is it not obvious kwa kila mtu kwamba kama si mahakama leo zitto asingekuwa mwanachama wa cdm ? Wewe kumbe issue ni kuwekewa vikwazo ! Wewe ulitaka awe treated kama mwanachama mwingine yeyote ?, obviously hilo haliwezekani, kwa sababu hapo alipo tayari ana mgogoro na chama, na lazima awe treated with suspicion......
Kwa hiyo cdm wanachofanya ni kujaribu kumzuia kwa kiwango wanachoweza asiharibu chama zaidi....kama si zuio la mahakama wangekwenda mbali, wangemfukuza !
Kitendo tu kwamba hawajamfukuza ingawa walipenda sana kufanya hivyo kinaonyesha wameiheshimu mahakama !
Chadema ni chama chenye ndoto za kushika dola na kilitegemewa kiwe chama cha kwanza kuheshimu amri za vyombo vya dola ikiwemo mahakama.
Sote tuna fahamu zitto kabwe aliweka zuio mahakamani dhidi ya kamati kuu ya chadema kujadili uanachama wake na kutokana na mwenendo wa shauri hilo mahakami, mahaka iliagiza chadema kutojadili uanachama wa mh zitto kabwe hadi mwisho wa shauri yani hukumu.
Siku ya ijumaa John Mnyika alionekana kwenye vyombo vya habari akisema hawatojadili uanachama wa zitto kutokana na agizo la mahakama na shauri linalo endelea.
Lakini cha ajabu leo kwenye kikao cha chadema na waandishi wa habari kilicho kuwa na lengo la kutoa na kueleza maazimio ya kamati kuu, wameonesha wazi kuwa wame kahidi agizo la mahakama na kuya dharau na ni wazi walijadili uanachama wa zitto.
Kurugenzi ya Habari imenukuu maneno yaliyo somwa na dr slaa ya kionesha kamati kuu imejadili uanachama wa zitto.
Na nukuu
" chama kina wataka wanachama wote na wapenzi wote kuto shiriki mikutano ,ama shughuli zozote za kisiasa zitakazo andaliwa na zitto kabwe na washirika wake kwa jina la chadema"
kwa hayo maneno hapo juu haihitaji kuwa profesa kuelewa kuwa chadema wamemjadili zitto pamoja na uanachama wake hivyo wame kahidi maagizo ya mahakama na kuyasigina kabisa kama hawatambui uwepo wake.
Hayo maneno yaliyo somwa na dr slaa leo yanaonesha kabisa chadema kuto heshimu mamlaka za nchi.
Wananchi wanatakiwa kujua hawa chadema mambo yanapo kwenda kombo kwa upande wao ndio huwa wa kwanza kusema wanaonewa.
Nimejiuliza kilicho wafanya chadema kuto subiri jumatatu baada ya hukumu ndio wajadili uanachama wa zitto?
Hivi kwanini mh Tundu Lissu unashindwa kuwa mshauri mzuri kwa chama chako?
Chadema kwa hili la leo ni dharau kubwa kwa mahakama.
Karibuni wana jamvi.
Kwenye hili ulihitaji Profesa kuelewa tofauti ya kujadili uanachama wa mtu na maelekezo kwa wanachama!
Mbumbummbu wa sheria kama #TeamZitto !
yani Tundu Lissu anasema zitto ni mwana chama lakini papo hapo tamko lao linaonesha haki za zitto kama mwana chama wa chadema amepokonywa.
Ni wazi wameujadili uanachama wa zitto na hapo ndipo walipo kahidi amri ya mahakama.
MACHADEMA ni manafiq,mapu.bav. ,mawongo na MAJING. SANA!!
pole sana ndugu yangu, naona unajitoa ufahamu, na wewe ni mmoja wa waliompeleka z akafungue kesi mahakamani nini, kwa taarifa yako hapo ndio mmempoteza kabisa, kwani mpaka sasa hana chake, kuitetea ccm yakupasa uwe na akili kama ya chizi, jitambue.
na wakishindwa case utawasikia wanasema kuwa ikulu imeingilia case na kusingizia watu wengine na wata tunga adithi kama kawaida yao.
Sote tuna fahamu zitto kabwe aliweka zuio mahakamani dhidi ya kamati kuu ya chadema kujadili uanachama wake na kutokana na mwenendo wa shauri hilo mahakami, mahaka iliagiza chadema kutojadili uanachama wa mh zitto kabwe hadi mwisho wa shauri yani hukumu.
Siku ya ijumaa John Mnyika alionekana kwenye vyombo vya habari akisema hawatojadili uanachama wa zitto kutokana na agizo la mahakama na shauri linalo endelea.
Lakini cha ajabu leo kwenye kikao cha chadema na waandishi wa habari kilicho kuwa na lengo la kutoa na kueleza maazimio ya kamati kuu, wameonesha wazi kuwa wame kahidi agizo la mahakama na kuya dharau na ni wazi walijadili uanachama wa zitto.
Issue nadhani sio Kumshauri Zitto aombe radhi? Aombe Radhi kwa lipi? Nadhani tunapaswa na tulipaswa wote kwa pamoja kusimamia Misingi na kanuni za Chama. KK ifuate katiba katika kuwadiscipline wanachama ikiwa ni pamoja na kuwapa haki yao ya kusikilizwa na vikao vya juu kama BK. Wanachama wanapaswa kuhoji masuala ya chama katika vikao halali. Hii ndio itaifanya CHADEMA izidi kusimama, hakuna mshindi kwenye hili, whether ZZK ataondolewa uanachama wake kama Hakuna Demkrasia ya kweli ndani ya CHADEMA bado KK itakuwa haijaitendea Haki, Kama suala la Nidhamu litaangaliwa kwa ZZK peke yake na akina Lema Wataachwa wabehave the way they wish, hata kuwatukana na kuwakashfu viongozi wa juu kwenye mitandao na live, kutumia nguvu kunyang'anya personal properties za watu basi CHADEMA haitakuwa imeleta ukombozi wa kweli wanaoutumaini watanzania, CHADEMA would be another Catastrophic ghost in a face of an Angel.
Lisu hajui sheria ni mbishi wa wala hajui sheria.
Haina haja ya kubishana nanyi.
Na tuone nani mshindi