Mkuu Rutta, Nimeikamata hii kabla haijakuwa deleted........vitu vinaanza ku unfold.........
"Alichoandika Zitto facebook akakifuta..
Lissu anasema nimepewa magari 2 na Mzee Mkono. Anasema kaambiwa na Mkono. Naamini Mkono alimwambia pia mwaka 2005 alimpa Freeman Aikaeli Mbowe tshs 40m ili Mbowe asifanye kampeni Musoma vijijini. Nadhani alimwambia pia mwaka 2008 (baada ya orodha ya mafisadi kutangazwa 2007) Mkono alimpa Freeman tshs 20m za uchaguzi wa Tarime na Freeman akasema kwenye chama ametoa mkopo na akalipwa. Nadhani alimwambia pia kuwa Mwaka 2010 Mkono alimpa Mbowe tshs 200m za kampeni ya Slaa. Pia hakusahau kumwambia kuwa Rostam Aziz alimpa
Mbowe tshs 100m za kampeni. Lissu anajua
kuwa gazeti la Tanzania Daima limeanzishwa na
fedha za chama kutoka Conservative party?
Nimefanya internship yangu kwa Mkono and
Company Advocates kuhusu masuala ya
mikataba. Mzee Mkono ni Mzee wangu na alisaini
petition ya kumtoa Waziri Mkuu Pinda.
Lissu awaambie waliyemtuma wamwambie
ukweli. wote. Lissu ajue yeye ni kifaranga tu,
Mimi namtaka mama wa kifaranga ajitokeze.
Aeleze aliingia deal gani na Kinana na Sumaye
mwaka 2005 kufuati deni lake NSSF. Aweke
wazi mkataba kati yake na NHC kuhusu nyumba
ya Umma ilipo Club Bilicanas. They must know I
am not a push over. Chacha died, I won't.
Mtu ambaye hawezi kuheshimu mke wake
aliyemzalia watoto hawezi kunyooshea mtu
kidole kuhusu maadili "