Chadema na dharau kwa amri ya mahakama.

Chadema na dharau kwa amri ya mahakama.

wakati tundu lissu anasema hayo kuwadanganya watu, we soma maneno ya dr slaa aliyo nukuliwa na kurugenzi ya habari na yanaonesha wazi uanachama wa zitto umejadiliwa.

Hebu niambie hayo maneno ya dr slaa yana maana gani? Kama lissu anasema zitto bado ni mwana chama na hayo maneno yanatoka wapi na yana maanisha nini?

tatizo watu wanachukulia sheria kama quruan au biblia, unapowataka wanachama wasishiriki mikutano ya zitto wkt zitto bado anajulikana ni mwanachama halali wa chadema ambaye ana haki ya kufanya mikutano kupitia uanachama wake tayari lile zuio linahusu uanachama wa zitto kuzuiwa kupitia haki yake ya kufanya mikutano ka mwanachama wa chadema.tayari wamekaidi amri ya mahakama,mtasikia kesho
 
Last edited by a moderator:
Ni kwakua watetezi wa Zitto ni magenge ya watu hafifu wanaoshindwa kuelewa mopaka ya utendaji wa ndani wa Chama na Mahakama.
Zitto, ataondoka

Chadema wamejadili uanachama wa zitto kinyume na agizo la mahakama.

hivi [/color=red]mapoka[color] ndio nini?

hivi
 
Mawasiliano ya Zitto na mtu anayejiita chademampya ni vizuri yakafahamika.

Katafute gazeti la ----- la kabla ya mwaka mpya utayakuta mkuu I mean la week ya mwisho kuelekea mwaka mpya au ngoja kuna wadau humu watakuweke vipande vyake usome...
 
Last edited by a moderator:
Chadema ni chama chenye ndoto za kushika dola na kilitegemewa kiwe chama cha kwanza kuheshimu amri za vyombo vya dola ikiwemo mahakama.

Sote tuna fahamu zitto kabwe aliweka zuio mahakamani dhidi ya kamati kuu ya chadema kujadili uanachama wake na kutokana na mwenendo wa shauri hilo mahakami, mahaka iliagiza chadema kutojadili uanachama wa mh zitto kabwe hadi mwisho wa shauri yani hukumu.

Siku ya ijumaa John Mnyika alionekana kwenye vyombo vya habari akisema hawatojadili uanachama wa zitto kutokana na agizo la mahakama na shauri linalo endelea.

Lakini cha ajabu leo kwenye kikao cha chadema na waandishi wa habari kilicho kuwa na lengo la kutoa na kueleza maazimio ya kamati kuu, wameonesha wazi kuwa wame kahidi agizo la mahakama na kuya dharau na ni wazi walijadili uanachama wa zitto.
Kurugenzi ya Habari imenukuu maneno yaliyo somwa na dr slaa ya kionesha kamati kuu imejadili uanachama wa zitto.
Na nukuu
" chama kina wataka wanachama wote na wapenzi wote kuto shiriki mikutano ,ama shughuli zozote za kisiasa zitakazo andaliwa na zitto kabwe na washirika wake kwa jina la chadema"

kwa hayo maneno hapo juu haihitaji kuwa profesa kuelewa kuwa chadema wamemjadili zitto pamoja na uanachama wake hivyo wame kahidi maagizo ya mahakama na kuyasigina kabisa kama hawatambui uwepo wake.

Hayo maneno yaliyo somwa na dr slaa leo yanaonesha kabisa chadema kuto heshimu mamlaka za nchi.

Wananchi wanatakiwa kujua hawa chadema mambo yanapo kwenda kombo kwa upande wao ndio huwa wa kwanza kusema wanaonewa.

Nimejiuliza kilicho wafanya chadema kuto subiri jumatatu baada ya hukumu ndio wajadili uanachama wa zitto?

Hivi kwanini mh Tundu Lissu unashindwa kuwa mshauri mzuri kwa chama chako?

Chadema kwa hili la leo ni dharau kubwa kwa mahakama.

Karibuni wana jamvi.
unatukaribisha kwenye matapishi?
 
Last edited by a moderator:
Kuna tofauti ya 'wanachama/wapenzi wasishiriki shughuli za kichama zilizoandaliwa na Zito' na 'Zito asiandae shughuli za kichama'
 
tatizo watu wanachukulia sheria kama quruan au biblia, unapowataka wanachama wasishiriki mikutano ya zitto wkt zitto bado anajulikana ni mwanachama halali wa chadema ambaye ana haki ya kufanya mikutano kupitia uanachama wake tayari lile zuio linahusu uanachama wa zitto kuzuiwa kupitia haki yake ya kufanya mikutano ka mwanachama wa chadema.tayari wamekaidi amri ya mahakama,mtasikia kesho

yani Tundu Lissu anasema zitto ni mwana chama lakini papo hapo tamko lao linaonesha haki za zitto kama mwana chama wa chadema amepokonywa.

Ni wazi wameujadili uanachama wa zitto na hapo ndipo walipo kahidi amri ya mahakama.
 
Last edited by a moderator:
chadema kama chama katiba yao inawapa mamlaka ya kumpiga maruufuku mtu yeyote kujifanya shughuli za chama that has nothing to do with judicial proceeding. pili uanachama wake haujajadiliwa ungejadiliwa asingekuwa mwanachama leo hii angekuwa kama mkumbo na mwenzake mwigamba

Mkuu hawa Visebengo wa Lumumba huwa wamekremishwa lines za kuja kuchafua hewa hapa jukwani... Darasa ulilompatia kama haja kuelewa tena baaaaasi... Kinacho ni kera kuliko ni jinsi ambavyo hawana uwezo wa kupambanua mambo kwa mapana! Hawaoni hawasikii hawapimi athari za kupanda kwa bei ya umeme na gesi kwa mapana na marefu! Hawaoni athari za kutoa eneo lote la bahari kwa wawekezaji! Hawani athari za kuwaua wananchi badala ya majangili.... nahisi humu ndani wanaoandika pengine ni robot...Lumumba CCM yote ni Janga kwetu Watanzania, Nshindwa kuelewa alie format brains zao kiasi cha wao kushabikia ngono 24/7 badala ya kujadili mambo yenye maslahi mapana kwa nchi yetu ...
 
kwa nini wanaomtetea zitto ni watu dhaifu sana....?hoja hawana poor team zitto
 
Mkuu Ruttashobolwa,jifunze kusoma na kuelewa na sio kulazimisha maandishi yasomeke utakavyo wewe:

Zitto hajajadiliwa at all,angalia mtiririko wa watu waliojadili kule kwenye uzi wa kurugenzi ya habari ya cdm,kuna zaidi ya mistari 10 kwa kila mtuhumiwa ila kwa zito kuna mistari mingapi iliyomjadili? Nways najua haya ni mapendo tu hata wengi wetu we do love the guy but we respect our leaders
 
Mbona wako sahihi zuio ni la kutojadili uanachama wake nitogauti na mikutano. Chama kiko sahihi
 
Nhnnn...ungeli-quote maelezo ya TL kidogo ningekuelewa. Hata hivyo cdm wako juu na hawaogopi chochote. Ilo tu linanifanya niione cdm mkombozi.
 
Kama kawaida kesho utasikia ama wakili wa Zito mgonjwa ama jaji flani anao hudhuru ama vinginevyo ila hadi sasa Zito ajue t's over and out
 
Nadhani mleta maada atakuwa alikuwa amelewa maana zito hakujadiliwa ndani ya kikao bali maani ya chama ndo yalitaka zito asipewe ushilikiano sehemu yeyote akiitisha mkutano.
 
Mkuu hawa Visebengo wa Lumumba huwa wamekremishwa lines za kuja kuchafua hewa hapa jukwani... Darasa ulilompatia kama haja kuelewa tena baaaaasi... Kinacho ni kera kuliko ni jinsi ambavyo hawana uwezo wa kupambanua mambo kwa mapana! Hawaoni hawasikii hawapimi athari za kupanda kwa bei ya umeme na gesi kwa mapana na marefu! Hawaoni athari za kutoa eneo lote la bahari kwa wawekezaji! Hawani athari za kuwaua wananchi badala ya majangili.... nahisi humu ndani wanaoandika pengine ni robot...Lumumba CCM yote ni Janga kwetu Watanzania, Nshindwa kuelewa alie format brains zao kiasi cha wao kushabikia ngono 24/7 badala ya kujadili mambo yenye maslahi mapana kwa nchi yetu ...

Mwanangu naona unavyogawa dozi za ukweli!
 
Back
Top Bottom