Chadema na dharau kwa amri ya mahakama.

Chadema na dharau kwa amri ya mahakama.

Mkuu Rutta, Nimeikamata hii kabla haijakuwa deleted........vitu vinaanza ku unfold.........

"Alichoandika Zitto facebook akakifuta..

Lissu anasema nimepewa magari 2 na Mzee Mkono. Anasema kaambiwa na Mkono. Naamini Mkono alimwambia pia mwaka 2005 alimpa Freeman Aikaeli Mbowe tshs 40m ili Mbowe asifanye kampeni Musoma vijijini. Nadhani alimwambia pia mwaka 2008 (baada ya orodha ya mafisadi kutangazwa 2007) Mkono alimpa Freeman tshs 20m za uchaguzi wa Tarime na Freeman akasema kwenye chama ametoa mkopo na akalipwa. Nadhani alimwambia pia kuwa Mwaka 2010 Mkono alimpa Mbowe tshs 200m za kampeni ya Slaa. Pia hakusahau kumwambia kuwa Rostam Aziz alimpa
Mbowe tshs 100m za kampeni. Lissu anajua
kuwa gazeti la Tanzania Daima limeanzishwa na
fedha za chama kutoka Conservative party?
Nimefanya internship yangu kwa Mkono and
Company Advocates kuhusu masuala ya
mikataba. Mzee Mkono ni Mzee wangu na alisaini
petition ya kumtoa Waziri Mkuu Pinda.
Lissu awaambie waliyemtuma wamwambie
ukweli. wote. Lissu ajue yeye ni kifaranga tu,
Mimi namtaka mama wa kifaranga ajitokeze.
Aeleze aliingia deal gani na Kinana na Sumaye
mwaka 2005 kufuati deni lake NSSF. Aweke
wazi mkataba kati yake na NHC kuhusu nyumba
ya Umma ilipo Club Bilicanas. They must know I
am not a push over. Chacha died, I won't.

Mtu ambaye hawezi kuheshimu mke wake
aliyemzalia watoto hawezi kunyooshea mtu
kidole kuhusu maadili "

Hadithi yako inatufundisha nini...?
 
mkuu matusi yako hayani yumbishi na wala si chochote kwangu.

Mahakama ina uwezo kuzidi hiyo institution na ndio maana hiyo institution imekatazwa kuujadili uanachama wake na ikakubali kupitia mnyika na leo kupitia dr slaa na tundu lissu wameonesha kuwa wame jadili uanachama wake na wamemfukuza.

!tundu lissu ana sema zitto anaendelea kuwa mwana chama sababu ya mahakama tuu, akimahanisha kuwa wao kama chadema walisha mjadili na kumfukuza kinyume na agizo la mahakama.

Wameenda mbali zaidi waki wasihi wana chama wao kuto hudhuria mikutano ya zitto ina maana wao kama wao walisha toa hukumu kumvua uanachama zitto ndio maana hawamtambui kama mwana chama wao na walishamjadili na kumfukuza.

Alaf cha ajabu zaidi nimemsikia lissu anasema kamati kuu imefanya uchunguzi sasa wao wao ndio wana fanya uchunguzi na hao hao ndio wanatoa hukumu.

Kwakweli nimeshangaa sana.

Team Zitto ndo imekula kwenu..
 
inaonesha wewe ni boya kweli unafikiri chadema wangejadili uanachama wa zitto leo hii huyo zitto angekuwa mwanachama wa chadema

mkuu matusi yako hayani yumbishi kabisa unapoteza muda.

Ukisoma kauli ya lissu na slaa utagundua ninacho sema.
 
Mimi simwelewi kabisa! Na kwa kweli nimejitahidi sana kutaka kumwelewa lakini wapi bana...kila nikijaribu naishia patupu!

Anachokitaka yeye katika kwenda kwake mahakamani ni nini? Maana tuseme hata akishinda huko mahakamani (na sijui hata atashinda kitu au jambo gani) na akaendelea kuwa mwanachama wa CHADEMA, tayari mahusiano yake na uongozi wa CHADEMA pamoja na sehemu kubwa tu ya wanachama yameshaharibika.

Ataendeleaje kuwa mwanachama wa CHADEMA katika mazingira kama hayo? Kaazi kweli kweli!
Atakuwa mwanachama wa Chadema kupitia mahakama lakini ataishi kama nguchiro…ha ha haaa
 
Nenda mahakamani ukatoe ushaidi zitto kajadiliwa usilete ujinga hapa na kwataarifa yako Keshatimuliwa sasa hana Tofauti na kafulila

mkuu parameter nilicho taka kusema nikuwa uanachama wa zitto umejadiliwa na nina shukuru wewe umekuwa muwazi kuelewa kauli za viongozi wako. kwa hiyo tukubaliane kuwa chadema wamedharau amri ya mahakama.
 
Last edited by a moderator:
Ninachoamini hii nyumba yote si safi kama tunavyoaminishwa!Dogo Zitto nae anafahamu uchafu mwingi wa hawa wakubwa na kwakua wameanza kumwaga mboga basi wategemee dogo Zitto hawezi kukubali kufa kibudu,lazima atanyea ugali ndipo hapo watu watabaki wameduwaa!
 
weka bayana kauli ya mahakama neno kwa neno...

shauri uanachama wa zitto ndani ya chadema kutojadiliwa na kamati kuu.

Agizo la mahakama lina wataka chadema kutojadili uanachama wa zitto hadi mahakama itakapo toa hukumu.
 
Ruttashobolwa, tatizo lako ni uelewa wa tafsiri ya sheria na wala sio chuki yako kwa CHADEMA, maana kinachozuiwa hapo ni matamshi yatakayoathiri hukumu ama mwenendo wa shauri lililopo mahakamani; sasa kama umeshawafukuza wasaidizi wa usaliti huyo msaliti amesalimika vipi? Hapo ndo kauli ya Lisu ilipojikita. Kama usaliti umethibitishwa kufanywa tangu 2009 sasa chama kuchukua tahadhari ya kuwataka wanachama wake kutoshirikiana na wasaliti mgogoro na mahakama unatokea wapi.?
Wakati mwingine inabdidi ushabiki uwekwe pembeni ili uwe na amani katika kufata kweli kijana.
 
ninachoamini hii nyumba yote si safi kama tunavyoaminishwa!dogo zitto nae anafahamu uchafu mwingi wa hawa wakubwa na kwakua wameanza kumwaga mboga basi wategemee dogo zitto hawezi kukubali kufa kibudu,lazima atanyea ugali ndipo hapo watu watabaki wameduwaa!

mkuu amesha anza kumwaga jaribu kutafuta.
 
amri ya mahakama ilikuwa uanachama wa Zitto usijadiliwe ...sio kila kitu kuhusu zito kisijadiliwe..
 
kwenye hili ulihitaji profesa kuelewa tofauti ya kujadili uanachama wa mtu na maelekezo kwa wanachama!
Mbumbummbu wa sheria kama #teamzitto !

mkuu siyumbishwi na matusi yako. Huhitaji kutumia sheria kujua chadema wamejadili uanachama wa zitto.
Mahakama wame wakataza kujadili uanachama wake mpaka mwisho wa shauri.

Na ukisoma maelezo ya slaa na lissu utagundua kuwa wameujadili uanachama wa zitto, sema lissu ajui kuwashauri hila anajua kuwa changanya.
 
Big up ruta.

Umeng'amua kipengele kizuri na muhimu sana.

Secretariet iliagizwa kuandaa ripoti ya kikao cha kamati kuu na kusoma kwa watu wa media. Maana yake ni kwanza kilichoandaliwa na kusomwa ni kile kilichojadiliwa na kuamuliwa kwenye kamati kuu.

Guys I loved this party bit I'm real fed up with all the shits going on within this party.

Mahakama tafadhali chukueni hatua kwenye hili.
Jamani MAHAKAMA HAICHUKUI HABARI KUTOKA MITANDAONI DUUU?UPO UTARATIBU WAKE.
NA HILI NDILO NENO LA MWISHO.
 
Umebaki unatapatapa msukule wewe....Zitto.hajao kwahiyo huenda akakuposa na kukuoa....

Zitto habari yake imekwishaaaaaaaa!!!!!!

tedo una jisumbua bure na haya matusi yako.

LAKINI NAJUA UMEONA NA KUSIKIA KAULI ZA VIONGOZI WAKO ZINA THIBITISHA KUWA UANACHAMA WA ZITTO UMEJADILIWA NA NI KINYUME NA AGIZO LA MAHAKAMA.
 
Last edited by a moderator:
Jamani MAHAKAMA HAICHUKUI HABARI KUTOKA MITANDAONI DUUU?UPO UTARATIBU WAKE.
NA HILI NDILO NENO LA MWISHO.

Hapa tunacho jadili ni kauli za viongozi wa chadema na wameyaongea na wewe umesikia kabisa na ni wazi wame ujadili uanachama wa zitto.
 
Back
Top Bottom