Nikiangalia Cuf bara haina mvuto wa kuunda serekali 2010 kwani haina viongozi shupavu wa kuweza kuongoza, viongozi wengi wa cuf sio maarufu katka nyanja za siasa ,wengi either fkutoka siasa za chini hadi kuwa cuf. hii tofauti na Cuf zenj ambapo baada ya wengi kungatuka kutoka ccm cuf zenj imekuwa na nguvu na ushawishi mkubwa, maalim seif aliwahi kuwa waziri kiongozi, hamad rashid waziri wa mambo ya ndani, abubak khamis mwanasheria wa gov, Juma duni , machano khamis, Nassor Khamis, marehemu sudi Yussuf Mgeni , ali hajji pandu ni mwanasheria mKuu na wengine ,kama cuf zenj isingekuwa na viongozi mashuhuri na maarufu wanaozijua siasa za tz basi ngalikuwa dhaifu sana na isingeweza kuleta changamoto za siasa za tz kama vile vyama vyengine vilivyopo
kwa chadema nako ndiko hivyo hivyo haina wanasiasa mashuri angalau 50 ambao wanaoweza kuwa mawaziri , manaibu au hata wakuu wa mikoa ambazo wanazijua siasa za tz, wanaoweza kupambana na ccm katika chaguzi lkn wengi wa viongozi wao ni kutoka chini.
kama utaangalia chadema inaviongozi wa 3 tu maarufu kama mbowe, slaa, zito Wengine watz waliochini wanaweza kuwafahamu.
watu wengi sasa wanakimbilia mikutanoni kuangalia helikopa jinsi inavyoruka na kutua na sio kuvutia kwa sera.
ili kiingie ikulu chadema kuna haja ya kuwa na viongozi wengi maarufu kutoka chama tawala, hivi ndivyo ilivyo nchi nyingi duniani kama vile kenya na sio kutegemea wanasiasa wasiomaarufu kama vile chadema
najua wapo wanachadema watakaoukataa ukweli na kuamini wananguvu lkn kila mtz makini anajua hizi ni nguvu za soda zikipoa mwanyaji atakunywa kiulaini
haya ni maoni yangu tu, unahaki ya kuyapinga lkn kwa hoja adhimu