Zanzibar-ASP
JF-Expert Member
- Nov 28, 2013
- 12,151
- 44,120
Kuna msemo unasema uongo ni wa kitu cha kukufurahisha na kukaa kwa muda mfupi tu, lakini Ukweli unaweza kuwa mchungu mwanzoni lakini hudumu milele na huzaa furaha ya siku zote hapo mbeleni.
Kile kitendo tu cha Lissu kusema anakwenda kugombea na mwisho kuutwaa uenyekiti wa CHADEMA, ghafla nchi ikatikisika kisiasa, kila sarakasi zikaibuka kutoka kwa watawala, CCM, vyombo vya dola, mamluki wa ndani ya Chadema, msajiri wa vyama vya siasa, mahakama, vyombo vya habari nk.
Mwamba akasema, liwe jua au mvua, 'atakinukisha' kuhakikisha kisiasa hakuna uchaguzi utafanyika oktoba mwaka huu. Sasa hapo mpaka kesi ya uhaini zikabumbwa na Chadema kusimamishwa kufanya siasa.
Maajabu ni kuwa, tangu kuanza kufanyika kwa hayo yote, iwe mitandaoni mpaka mtaani, nguvu ya Chadema ikaongeza maradufu.
Sasa watanzania wengi wanasema, Chadema na Lissu shikirieni hapo hapo, msirudi nyuma hata nukta moja kwa sababu wamesikiliza, wakawaelewa na sasa wana imani kubwa zaidi juu yenu katika mapambano ya kumtoa na kumuangamiza mkoloni mweusi.