Chadema na Makamanda Tujifunze Mbinu za Medani #2

Chadema na Makamanda Tujifunze Mbinu za Medani #2

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
31,698
Reaction score
41,733
Somo #1 lilikuwa kwenye kuutambua uwanja. Kutambua uwepo wa washirika, wadaiwa, maadui na wasiohusika kwa kujua au kutokujua kwao.

CHADEMA na Makamanda tujifunze Mbinu za Medani #1

Somo #2 mkononi liangazie kwenye kutambuana sisi kwa sisi kama wapiganaji.

Ni muhimu tukayafahamu na kuyakubali mazingira halisi tuliyomo hata kama ni machungu na yenye ukakasi. Hakuna lisilokuwa na dawa au ufumbuzi.

Ni muhimu pia tukawa wawazi kwani ni kwa namna hiyo tu ndipo tutaweza kupiga hatua mbele.

Hadi sasa, sisi zaidi ni kundi la wenye uelewa (elimu) ambao kimsingi ni juu ya kilicho kiwango cha wastani.

Kundi hili ndilo lenye wanaoonekana mitandaoni na lina uwezo wa kutosha wa kupambanua mambo.

Kundi hili lina uwezo wa kusoma katikati ya mistari, linaweza kuusoma mchezo, linaweza kuona kuchezwa shere hata kama mcheza ni Madelu, nk.

Ni nia na dhamira ya dhati ya adui kuona kuwa makundi mengine zaidi hayaelimishwi. Lengo likiwa ni kuyafanya kwa kadri inavyowezekana yasijue kuwa nayo yanahusika kwenye harakati hizi.

Kuzuiwa kwa mikutano ya kisiasa na makongamano kinyume na sheria ni mwendelezo wa agenda yao hiyo.

Hakuna kinachoshindikana chini ya jua.

Udhwalimu utashindwa.
 
Angalizo:

Tunapokuwa tunatambua watu kugawanyika kwenye makundi mbalimbali, yaani ya:

"wapambanaji (wadai), washirika, wadaiwa, maadui, wasiohusika (kwa kujua au kutokujua),"

ni muhimu tukawa macho na maoni na ushauri wao.

Ushauri au maoni ya maana kwa mdai yanaweza vipi kutoka kwa wadaiwa, maadui au hata wasiohusika? Kwani wasiohusika, pili pili asizozila zinaweza kumuwasha namna gani?

Kuwasikiliza watu wa namna hii ni sawa na kupokea ushauri kutoka kwa mamba mwenye njaa kuhusu namna ya kuvuka mto salama na kuweka kumuepuka mamba yeye.

Au nasema uongo ndugu zangu?
 
Habari leo mujini, katiba mpya sikia,
Yadaiwa kama deni, Mdaiwa kakimbia!
Mapolisi kulikoni, wadai kuwazuia?
Enyi msiohusika, hoho vipi ziwawashe?
 
Back
Top Bottom