Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,771
- 41,027
Kubwajinga
1. Matangazo ya gazetini pekee ya mwaka mmoja hayatoshi kuweka sura ya ruzuku kusambazwa kwa kuwa hayawezi kutaja orodha ya wilaya zote zilizopokea ruzuku. Si unajua kwamba huwa zinachapwa audited statements ambazo ni summary? Sheria ya vyama vya siasa inasema msajili anawajibu wa kuchapa mahesabu ya vyama. Sasa kamuulize msajili kwa nini hachapi wakati CHADEMA inampelekea kila wakati? CHADEMA wakati wote inaweka wazi matumizi yake kwa wanachama kupitia vikao ikiwemo kiasi kilichosambazwa na jina la eneo. Mimi ya kwetu niliyapata Zanzibar. Lakini baada ya baraza kuu unakumbuka Tamko la CHADEMA lilionyesha kwamba wajumbe walijadili na kupitisha ripoti ya fedha ikiwemo mgawanyo wa ruzuku?
2. Hilo la Uchagga wa sekretariati acha kuwasingizia. Mbona iliwahi kusemwa hapa kwamba Wasukuma ni wengi kuliko wachagga? Kama wasukuma ni zaidi ya 30% katika makao makuu ya CHADEMA kwanini unawataja wachagga tu wakati mwenyewe umesema ni 25&, au unafanya spinning? Na ni kiongozi gani wa sekretariati au mbunge ambaye amechaguliwa kwa shinikizo la Freeman kutokana na mchango wake ambao amechangia chama yeye kama Freeman?
Hebu Mods tuleteeni tena hapa tamko la CHADEMA walilolitoa kujibu suala la Uchagga, au tupe link ambapo suala hili lilishajadiliwa na kujibiwa na Zitto, Mnyika, Kitila na wengineo.
Wallah napata uchungu haya mambo kurudiwa rudiwa ili hali yalishajibiwa mpaka makada wa CCM wakasalimu amri wakati huo
Asha
Jamani kuna mtu mwenye ile makala ya Mzee Mtei aliyoandika "CHADEMA ni nini, CHADEMA ni nani?" ambapo aliweka wazi historia ya kuanzishwa kwa CHADEMA na wakina nani alianzisha nao na katika maeneo gani? Iliwahi kuwekwa hapa JF na kati ya Zitto au Mnyika; hebu toeni link basi
Asha
Inaonekana kuwa lengo kuu la kundi hili ni kulinda maslahi binafsi. Furaha kubwa ya kundi hili ni kuhakikisha kuwa ruzuku ya shilingi milioni 66 inayopata CHADEMA kila mwezi haifiki mikoani. Badala yake inatumiwa nao kwa mishahara na posho za safari za magari na helikopta zisizokwisha na zisizo na manufaa yoyote kwa chama.
Kuna habari kwamba baadhi ya wale walioko makao makuu wamenufaika na fedha za CHADEMA, kiasi cha kuanzisha miradi na biashara ambazo hawakuwa nazo kabla hawajajiunga na CHADEMA.
Kwa jumla kundi la kwanza la CHADEMA lililoko makao makuu linatuhumiwa kwa ubadhirifu, ufisadi, udikteta, matumizi mabaya ya fedha ikiwa ni pamoja na matumizi ya helikopta ambayo hayana tija yoyote katika ujenzi wa chama.
Juu ya yote, kundi hili linaaminiwa kuwa lina mawakala wa chama tawala ambao wamekaa pale kukomba tu fedha ya chama zinazowapeleka mikoani, huku wakiuacha Mkoa wa Dar es Salaam ukiwa hauna uhai wa chama kwa sababu safari ndani ya Dar es Salaam hazina posho.
Lengo kuu la kundi hili ni kuhakikisha kuwa lengo la chama cha upinzani la kushika madaraka ya utawala linatimia. Hili ni kundi lenye uchungu wa kweli na chama. Ni kundi linalotaka nguvu zote za chama zielekezwe kwenye kujenga chama ngazi zote.
Ni kundi linalotaka kujenga mtandao wa chama nchi nzima. Kundi hili linataka chama kiwe na ofisi mikoani kote na wilayani ili wanachama wapate mahali pa kukutana, kupata wanachama wapya, kufundishana sera za chama, na kubadilishana mawazo juu ya ujenzi wa chama utakaosaidia kuleta ushindi katika chaguzi mbalimbali. Kwa kifupi hili ni kundi linalotaka chama kiwe cha watu wote badala ya kugeuzwa kuwa kampuni ya watu binafsi.
Kundi hili la pili lililoko mikoani ambalo ndilo lenye uchungu na chama linapinga vikali matumizi ya helikopta wakati wa kampeni za uchaguzi, wakati wagombea ubunge na udiwani hawapewi hata shilingi moja ya kuwawezesha. Kundi hili pia linataka ruzuku ya chama isiishie kufujwa makao makuu, bali ifike mikoani ili kusaidia kufungua matawi na kuwafikia wananchi wa vijijini ambao hawana habari zozote za CHADEMA.
Asha,
Inaelekea wewe ni mndani kabisa wa Chadema, jambo ambalo ni zuri na litasaidia kufikisha haya malalamiko.
Lakini ningekushauri usiwe mshabiki asiyedadisi, kama walivyo wa Simba na Yanga. Kama tunavyowachamba CCM, tusione kichefu-chefu kuhitaji fafanuzi za yale yasiyoeleweka kwenye upinzani, iwe ni CHADEMA au hata TADEA.
Kwa hiyo, ukweli unabaki pale pale kuwa, CHADEMA inatakiwa kujibu malalamiko ya wanachama wake, bila kuzunguka-zunguka otherwise hawatakuwa na tofauti yoyote na wanamtandao.
Kama kuna wanachama mikoani wanaolalamikia malipo, jibu ni kuchapisha tu mgawanyo na kuwaumbua kuwa mbona walipewa kiasi husika? Ila kama makosa yalifanyika katika ugawaji, CHADEMA bado ni wachanga kwa hiyo wangeeleza tu wanachama wake kuwa kuna makosa yaliyofanyika na hayatarudiwa. Lakini kumuingiza au kumlaumu msajili wa vyama, sidhani kama ni solution.
Kuhusu ukabila, hili sio la ajabu. Vyama vilipoanzishwa vilianza kwa milengo ya kikabila, kimajimbo na kidini, hasa kwa kutokana na waanzilishi au viongozi wake wa juu. Ni NCCR pekee ambayo ilikuwa kwa kiasi si ya kijimbo kwa vile base yake ilikuwa pale mlimani, mpaka Mrema alipoingia ndio ikaanza kuwa na mwelekeo wa kikabila.
Kwa kifupi ni kuwa vyama vyetu vyote vilianza kwa misingi isiyo mizuri ambayo ni tofauti na maandiko ya katiba zao. Kwa hiyo image za hivyo vyama zinatakiwa zibadilike kama vinataka kukua na kutwaa nchi. Kuficha kichwa mvunguni wakati kiwiliwili kiko nje ni mchezo wa kitoto.
My take:
you make your own mind!
Hivi mkjj una uwezo wa kujibu humu wakati wewe mwenyewe unashutuma nzito kuhusu Chadema katika moja ya threads humu JF? Ama kweli unamoyo, duhh, wala huoni haya?
oh no sir!.. nakuthubutisha uoneshe tuhuma nilizotoa dhidi ya Chadema... labda nilipitiwa.... nisaidie kuona hiyo/hizo tuhuma.
Aidha kiswahili kinakupiga chenga au unataka kunipiga mimi chenga, na maanisha unashutumiwa au unashutuma nzito zinakukabili. Usibabaishe. Zimo humu JF tena niliziona jana au juzi kama hazijafutwa sijui.
Aidha kiswahili kinakupiga chenga au unataka kunipiga mimi chenga, na maanisha unashutumiwa au unashutuma nzito zinakukabili. Usibabaishe. Zimo humu JF tena niliziona jana au juzi kama hazijafutwa sijui.
Mwaka thread ref .Ndiyo utaanmika unalia lia nini na una uwezo wa ku prove maneno yako ? Hakuna hadihi hapa wala dana dana ngoma unayo weka thread link tujimwage kama huna sema umekurupuka maana ni sehemu ya maisha kwa watu wa aina hii kukurupuka .Kakurupuka Sitta na Ristamn utakuwa wewe bwana?
Hii hapa: http://www.jamboforums.com/showthread.php?t=11397
Na kichwa cha habari: Mwanakijiji Awagombanisha Chadema
achana nao hao Dar-es-salaam hawa Lunyungu na kundi lake la spinners na whinners. Wanataka kugeuza walichosema kwa kukusingizia hujui kinyerere wakati wewe ni mzawa halisi !