Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,771
- 41,027
Mzee Mwanakijiji
Mfumo wa CHADEMA umeweka check and balance ili kudhibiti hali hii; na hata yameelekezwa katika taratibu za fedha(finnancial regulations) ambazo zimepitishwa na vikao vyama chama.
Mnyika.. hoja yangu inashambulia moja kwa moja huo mfumo wa chama. Kama umepitishwa na vikao vya chama haufanyi kuwa sahihi bali unauhalalisha tu. Dhana ya mgongano wa maslahi inapata nguvu pale ambapo mtu ambaye ana maslahi binafsi (deni) anapata nafasi ya kusimamia kile ambacho ni cha umma (public funds) ambapo maslahi yake binafsi pia yamo.
Daktari licha ya utaalamu wote alionao inapendekezwa mara nyingi asimtibu ndugu yake wa karibu isipokuwa kama ni lazima kweli hii ni katika kumsaidia kuwa objective katika kazi yake. Hivyo daktari bingwa wa magonjwa ya wanawake mke wake anapopata matatizo ya ujauzito anaenda kwa daktari mwingine.
Vivyo hivyo majaji; kesi ya ndugu yake wa familia inapokuja mbele yake anatakiwa kujitoa ili kuhakikisha kuwa hata mwonekano wa mgongano wa maslahi hauwezi kutokea. Hata kama huyo ndugu yake waligombana miaka iliyopita na hawazungumzi. Hawezi kusema "naweza kusikiliza kesi hii kwa sababu huyu ndugu yangu hatuzungumzi". Akiruhusiwa na akamkuta ndugu yake hana hatia.. watu watasema "kamuachilia ndugu yake".
Sasa, Mbowe anaidai Chadema milioni 42; Sasa hilo la kukiposhesha chama mimi sina tatizo nalo hata kidogo. Ni haki ya mtu yeyote mwanachama au mtu mwingine kukikopesha chama kwa taratibu zilizopo na kwa makubalianao. Lakini hapa pia kuna maswali mengine.
a. Je amekikopesha kwa riba na ni riba ya kiasi gani? Matumaini yangu ni kuwa hakuna riba at all. Lakini kama kuna riba, tutaingia kwenye tatizo jingine kabisa ambalo naweza kuliona kama ukungu kutoka mbali.
b. Kama Mbowe ni mshiriki wa mijadala ya matumizi ya fedha za chama na mipango ya chama kuhusu fedha mbalimbali je anashiriki katika mijadala ya kiasi gani kitumike kulipa madeni ya wadeni wa chama? Kama ndiyo, tatizo jingine liko wazi.
c. Kama chama kinapanga matumizi ya fedha zake, Mbowe kama Mkopeshaji ana nafasi gani ya kuelekeza (steer) fedha za chama katika kulipa madeni wakati yeye ni mdeni mkuu?
Sasa, hapa ninachozungumzia ni mwonekano wa mgongano wazi wa maslahi.
Mbowe ajitoe kwenye kutia sahihi za matumizi ya fedha za chama na asihusishwe katika maamuzi (anaweza kushiriki mijadala lakini bila ya kuwa na nguvu ya kura) hadi pale atakapolipwa deni lake. Hili la mwisho linamhusu Ndesa vile vile.