Chadema na usimamizi wa fedha zake; mgongano wa maslahi?



teh teh teh teh
Wenye fedha wanapoanzisha chama lazima waweke kanuni zitakazolinda masilahi yao. Kama hiyo signatory lazima awe mwenyekiti na mwingine akijaribu kuuwania huo uenyekiti kutokana na kanuni zao ni za kimasilahi wanaona signatory itatoke nje ya control yao.

Wanamkanya kijana kaa chini tunaomba jitoe ,kijana akijitoa wazee wa kanuni wanaona masilahi yao ya u signatory kijana anayatia ktk hali tete ,huyu kijana pamoja amejitoa leo lakini siku za usoni atautaka tena u signatory. sasa kinachofuata ni kuhakikisha tuna m-changanya kijana ama ahame chama ama a give up.
 
Mimi nafikiri hii ilikuwa sababu tosha kabisa ya kumuengua Zitto katika kugombea uenyekiti. Kwani Mbowe anakidai chama.
 
Wewe spinning huiwezi....kachukue shule kwanza kwa wenzako then uje. Kamuuliza angalau Makamba namna ya ku-spin, hii ya kwako ni nyeupe mno....

Umeninyanyua sana kunipeleka kwa Makamba kujifunza, wakati napata "shule" ya bure hapa hapa JF kuwa Mbowe ni mdai mkubwa wa chama, 42m na huenda zikaongezeka! Wakati huo huo yeye ni Mwenyeki na mtia saini wa cheque kuna soma zuri la spinning kushinda hili?

Kama spinning ukajifunze wewe hii yako ni aibu hata kuita ni spinning!

Ukweli utabaki chama aanzishe Mbowe na familia yake, wahangaike nacho mpaka kufika hapo kilipofika halafu mje wa kuja kuleta mambo yenu accounting concepts na blah blah zenu.

Mimi toka nimeijua Chadema nimekuwa nikisikia hizi nyimbo za Mbowe kudai chama, madeni hayaishi na hakuna mchanganuo wa madeni mnapewa figure tu. Akina Kafulila walio jaribu kuhoji yaliyo wakuta ni historia. Wahenga walisema kapu la mjanja mjinga hatii mkono Mbowe ataendelea kukamua tu after all shamba la bwana Kheri na Mbuzi wa bwana Kheri!
 
Labda kwa sababu wameshiriki kikamilifu katika kupambana VITA dhidi ya Ufisadi(kwa kuanzia na ile list of shame)

Wao hawakufanya hilo; wao walilikuza tu hilo zaidi ya yote sioni.

.......
kingine sikioni so far kinachoweza kunifanya niwachangie,nina wasiwasi hela nitakazowachangia zaweza kutumika kulipa madeni kwa Mbowe na Ndesa(nisieleweke vibaya hapa)..

Hofu yako hiyo ni ya msingi.


Nililiuliza hili wiki chache hapo nyuma juu ya vitega uchumi vya Chadema.. watu wakadhani nawawangia!
 
Shalom, Mku tunazungumzia tanzania na sii nchi ambazo zinafanya malipo ama transfer ya fedha kwa njia hizo. Bongo inafahamika kabisa uwezo wa signatory na ndicho kinacholeta matatizo yote haya. Hakuna mtu hapa anasema Mbowe kaiba fredha ama hatuna imani na Mbowe isipokuwa ni utaratibu mbaya uimetumika na ndio sababu kubwa ya matatizo yote ndani ya Chadema toka nimsikie Kabourou hadi hawa kina Juju.

Na waswahili husema lisemwalo sana mwisho huaminika na maadam tumaona wapi matatizo yameanzia na upo uwezekano mkubwa wa Mbowe kutokuwa msaini wa cheque, mimi sioni tatizo liko wapi maadam hatua hiyo itaondoa kinyongo na fikra mbaya ambazo zinaweza kukigharimu chama. Kuweka sign cheque ni hatua ya mwisho kabisa ya malipo na bahati mbaya biashara nzima ya chama Chadema ni kazi za kanisa yaani kinachoingia hakizai isipokuwa kinatumika na bahati mbaya kuliko yote ni mali ya wanachama wote...Hii ni kazi ya kuaminiana na bahati mbaya Wadanganyika hatuwezi kuaminiana inapofikia ktk maswala ya fedha hasa pale mshika fedha ama mweka sahihi anaposhamiri kimaisha kuwashinda wengine, hoja huzuka!

Na amini maneno yangu watu hawatajali una mali kiasi gani ama umekikopesha chama kiasi gani maadam wanahisi kuna kamchezo wataendelea kudhani hivyo..Kibaya kwa Chadema mtu wanayemdhania hayo ndiye mwenyekiti wa chama..Angekuwa Mkandara hapa wala wasingekuwa na shida kwa sababu wanajua wanaweza kunivaa wakati wowote..Hivyo kuwepo kwa misingi bora za uhasibu kulingana na mazingira yetu ni muhimu zaidi..

Naomba ifahamike kwamba hapa tunatoa mawazo yetu ktk kujaribu kuboresha hali ya kisiasa ndani ya chama na sii kubisha tu ili mradi kubisha pasipo kuangalia misingi ya ulipaji na hasa uwekaji sahihi ikiwa ndio mamlaka ya mwisho ktk matumizi..

Hivyo sioni shida kubwa ya kuweka mtu mwingine badala ya Mbowe kwani sidhani kama kazi za mwenyekiti ni pamoja na uwekaji sahihi malipo ya chama.. Sidhani kama hiyo ndio kazi ya wenyeviti hata hao CCM wasiaminika kabisa hawafanbyi hivyo...Ila kama kuna mchango kwa sababu ya Mgombea aidha iwe Urais ama Ubunge hapa naweza kubali mgombea kuwa mweka sahihi kinyume cha hapo mkuu hutaweza kubadilisha mawazo ya Wadanganyika wengi. na kila mnavyojaribu kuweka sababu ndo mnavyo wapa mashaka na watazidi kuhoiji vitu ambavyo hata hawana uhakika navyo...
 

kwa kuandika hayo ulioandika je huoni kama the so called wapiganaji wenzako watakuchukia?
 

- Hewala mkuu, wala hakuna cha kuongeza hapa!

Respect.


FMEs!
 
kwa kuandika hayo ulioandika je huoni kama the so called wapiganaji wenzako watakuchukia?
Wanichukie kwa sababu gani?..Umemsikia Kitila Mkumbo akizungumza na kutoa shukran zake. Mbowe wangu, anafahamu nachozungumza sii kwa kulenga maslahi yake bali kuondokana na adha hizi zote ambazo hazina mpango..Kwani biashara zake tu kwa mwaka ni mtaji mzima wa Chadema, na hizi fujo ni lazima zikome na pengine njia bora zaidi ni yeye kuwa mbali na cheque hizo. Ni ushauri, taabu iko wapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…