CHADEMA na vita ya panzi kunguru hayuko mbali!

CHADEMA na vita ya panzi kunguru hayuko mbali!

View attachment 3196700

CHADEMA imeuonyesha ulimwengu mzima jinsi ilivyo chama cha kitoto.
Panzi wawili, Mbowe na Lissu wako busy kutukanana, kusutana, na kurushiana vijembe hadharani katika kuwania uenyekiti wa chama.

Wenzao CCM hatua hii huwa inafanyika hata kabla ya uchaguzi wa mwenyekiti wa chama, wakienda kuchagua mwenyekiti wao huwa wana a unanimous decicion.

CHADEMA wachanga wa kuendesha vyama wanaparurana hadharani kama hawana akili nzuri, na mparaganyiko wa chama hauko mbali. Matokeo yake Kunguru-CCM atawala wote.

Mark my words.
vita vya panzi furaha ya kunguru, hiyo picha ya BBC bana dah!🤣
 
Hamtegemei kura za Wananchi mnachotegemea ni vyombo vya Dola kuwaweka madarakani hamna UHALALI wowote wa kujiita viongozi wakati mumeingia kwa ubabe.

Achieni uwanja uwe sawa halafu ndio mjisifu.
Sasa kama unajua ccm haitegemei kura za wananchi kukaa madarakani huo uimara wa chadema ya lissu utasaidia nini?.Endeleeni kuwaza kiharakati kwenye nchi iliyokaa chini ya chama dola nusu karne.inawezekana hamuelewi mambo yalivyo.
 
Sasa kama unajua ccm haitegemei kura za wananchi kukaa madarakani huo uimara wa chadema ya lissu utasaidia nini
Tunataka Lissu alete Siasa za kimapambano HAKI huwa inadaiwa HAKI yetu ya kujichagulia Viongozi tuwatakao tutaipambania kama Kenya Msumbiji nk.

Katika hayo mapambano tunataka mtu kama Lissu ambaye sio mla RUSHWA mtu ambaye yuko radhi liwalo na liwe.
 
Sasa kama unajua ccm haitegemei kura za wananchi kukaa madarakani huo uimara wa chadema ya lissu utasaidia nini?.Endeleeni kuwaza kiharakati kwenye nchi iliyokaa chini ya chama dola nusu karne.inawezekana hamuelewi mambo yalivyo.
Mkuu hawajui kuwa siasa na maazimio ya viongozi humalizikia kwenye party caucus!
Baada ya hapo ni vote of no/yes confidence.
 
Tunataka Lissu alete Siasa za kimapambano HAKI huwa inadaiwa HAKI yetu ya kujichagulia Viongozi tuwatakao tutaipambania kama Kenya Msumbiji nk.

Katika hayo mapambano tunataka mtu kama Lissu ambaye sio mla RUSHWA mtu ambaye yuko radhi liwalo na liwe.
Mkuu uanaharakati haujawahi kuendesha nchi, unless mtu anataka kuendesha nchi kwa sheria za kijeshi na kuweka katiba pembeni.
Uanaharakati hata ndani ya CHADEMA hautamssidia Lissu.
 
Mkuu uanaharakati haujawahi kuendesha nchi
Tunachotaka ni REFORMS kwenye mfumo wetu wa Uchaguzi ili usiingiliwe na uwe HURU ili sisi Wananchi tuwe HURU kuchagua Viongozi tuwatakao

Tunataka KATIBA nyingine bora kuliko hii ya sasa ambayo imepitwa na wakati.

Uanaharakati ni jambo zuri sana.
 
Wenzao CCM hatua hii huwa inafanyika hata kabla ya uchaguzi wa mwenyekiti wa chama, wakienda kuchagua mwenyekiti wao huwa wana a unanimous decicion
Una kumbukumbu yoyote ya Wagombea zaidi ya Mmoja kwenye Nafasi ya Mwenyekiti wa Ccm au makamu Mwenyekiti wa Ccm! ?
 
Back
Top Bottom