CHADEMA na washirika wake sio tu wanapaswa kuomboleza bali wanapaswa kufanya sala ya toba

zandrano

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2017
Posts
8,598
Reaction score
9,539
Tusijisahaulishe kuwa viongozi wa Chadema wakishirikiana na washirika wao ndio walio chochea watu kuingia barabarani na kufanya fujo na hatimaye baadhi yao kupoteza maisha, isingekuwa chadema na washirika wao kuchochea huenda hata mtu mmoja asinge kufa.

Nakubaliana na Chadema na washirika wake kufanya maombolezo lakini muhimu zaidi wanapaswa kufanya sala ya toba kwa kuchuuza roho za watu wengine.

Wale wote walio chochea, walio fadhili fujo na kuratibu wanapaswa ksali sala ya toba.
 
Vipi kuhusu nyinyi wauaji! Mnasherehekea umwagaji wenu wa damu au ndiyo mtaendelea kuishi kama digidigi maisha yenu yote? Inakuwaje mlishinda kwa 98% na bado mnakosa ujasiri wa kuwashukuru wapiga kura wenu nchi nzima kupitia mikutano mikubwa ya hadhara!
 
Yule sheikh Sharif Majini naye alichuuzwa na chadema?
 
Akili nyingine ni kama za Abdul na Bi Mkubwa wake vigodoro. Kwani CHADEMA ndiyo walitoa amri ya kuuwa watanzania wasio na hatia kwa kupigwa risasi za vichwa?
 
Yule sheikh Sharif Majini naye alichuuzwa na chadema?
View attachment 3702221

Kumbuka siku ile watu walio kuwa wanafanya fujo na kuchoma mali za watu walihusika pia kuuwa na kuwadhuru kama askari na watu wengine ambao walidhaniwa kuwa walipiga kura. Majambazi na wahalifu walio fadhiliwa walielekezwa kuwauwa walio piga kura.
Viongozi wa Chadema wanapaswa sio tu kuomboleze bali watubie kwakuwasababisha watu vifo.
Chadema na washirika wao wasinge hamasisha fujo na vurugu kusingetokea kifo hata cha mtu 1.
 
Vipi kuhusu nyinyi wauaji! Mnasherehekea umwagaji wenu wa damu au ndiyo mtaendelea kuishi kama digidigi maisha yenu yote? Inakuwaje mlishinda kwa 98% na bado mnakosa ujasiri wa kuwashukuru wapiga kura wenu nchi nzima kupitia mikutano mikubwa ya hadhara!
Jambo unalo paswa kujiuliza hapo ulipo ni; je?
Kama Chadema wasinge hamasisha vurugu na wafadhali wasingetoa pesa za kufadhili vurugu na waratibu wasinge panga vuru, je kuna mtu angeuwawa?
Jibu, ni hakuna hata mmoja angekufa siku ya octoba 29.
Viongozi wa Chadema na walio fadhili fujo sio tu wanapaswa kuomboleza bali wanapaswa pia kusali sala ya toba.
 
Shida yenu iko sehemu moja tu! Kutopenda kujadili chanzo hasa cha tatizo ambacho ni grievances za wananchi za muda mrefu mfano uminywaji wa haki za kiraia, wizi wa wazi wa kura, uonevu, utekaji, ufisadi, ubadhirifu, ukosefu wa ajira kwa vijana, upendeleo, nk.

Msipochukua hatua za kutafuta suluhisho la kudumu la manung'uniko sugu ya wananchi, ipo siku yatatokea machafuko makubwa zaidi! Na mtakosa wa kumlaumu.
 
Si kweli kwamba Serikali haisikilizi na kutatua kero za wananchi.
Mara kadhaa tumeshuhudia serikali ikichukua hatua.
Mfano wa baadhi ya kero;
1. Awamu ya 5 ilivifungia vyama kutokufanya siasa, awamu ya 6 ilisikiliza kero hiyo na kuviruhusu vyama kufanya siasa.
2. Alivifungulia vyombo vya habari vilivyo fungiwa/ uhuru wa vyombo vya habari.
3. Suala la katiba mpya awqmu ya 6 imelipokea na limewekwa kwenye ilani.

Shida ya Chadema na washirika wake ni kutaka kuvuruga mema yanayo tekelezwa kwa uchu wa madaraka.
Rais Dkt Samia ni mtu mwema na msikivu sana, ila ukimletea shobo kamwe hawezi kukuvumilia.
 
Mimi naongelea haki ya mwananchi kumchagua mgombea anayemtaka. Hii haki tangu Magufuli alipoingia madarakani aliiondoa. Na huyu mrithi wake naye ameiendeleza.

Utekaji na mauaji ya wakosoaji nayo yameongezeka! Wagombea wa upinzani wanaenguliwa kwa hila ili wale wa ccm wapite pasipo kupingwa! Kukithiri kwa vitendo vya rushwa na ufisadi! Matumizi mabaya ya fedha za walipa kodi, ukosefu mkubwa wa ajira kwa vijana, nk.

Wewe unaleta habari za kuruhusiwa mikutano ya kisiasa, uhuru hewa wa vyombo vya habari, nk. Hiyo Katiba mpya yenyewe unayo iongelea iko wapi?

Ndiyo maana ninawatahadharisha mapema! Mkiendelea kujificha kwenye kichaka cha CHADEMA na TEC, badala ya kuhangaika kuondoa kiini hasa cha yale machafuko; mjiandae 2030 kutokea vurugu kubwa zaidi.
 
Mimi naongelea haki ya mwananchi kumchagua mgombea anayemtaka. Hii haki tangu Magufuli alipoingia madarakani aliiondoa. Na huyu mrithi wake naye ameiendeleza.

Utekaji na mauaji ya wakosoaji nayo yameongezeka! Wagombea wa upinzani wanaenguliwa kwa hila ili wale wa ccm wapite pasipo kipingwa! Kukithiri jwa vitendo vya rushwa na ufisadi! Matumizi mabaya ya fedha za walipa kodi, ukosefu mkubwa wa ajira kwa vijana, nk.

Wewe unaleta habari za kuruhusiwa mikutano ya kisiasa, uhuru hewa wa vyombo vya habari, nk. Hiyo Katiba mpya yenyewe unayo iongelea iko wapi?

Ndiyo maana ninawatahadharisha mapema! Mkiendelea kuhangaika na CHADEMA na TEC, badala ya kuhangaika kuondoa kiini hasa cha yale machafuko; yaliyotokea Oktoba 29, 2025 yatakuja kutokea tena 2030. Endeleeni kujitoa ufahamu na kuwageuza wananchi ni wajinga. Hamtokuja muamini macho yenu.
Wananchi wengi wanataka katiba mpya. Madai hayo yalisikilizwa vyema tangu awamu 4 ya JK lkn mchakato ulikwamishwa na wanasiasa ambao ni wawakilishi wa wananchi.
Awamu ya 6 pia imeibeba hoja ya katiba mpya na ipo kwenye mchakato.
Madai ya utekwaji na suala la ushahidi toa ushahidi kama umeona mtu au watu wametekwa.
CAHADEMA na TEC wamekuwa wachochezi wakuu kwa lenho la kujaza chuki kwa wananchi waichukie Serikali yao, hili halipaswi kufumbiwa macho wala kuonewa aibu lazima waambiwe ukweli, kwani sisi sote hatuna Nchi nyingine zaidi ya Tanzania.
 
CHADEMA na TEC hawajengi chuki kwa wananchi ili waichukie serikali! Wanachokifanya wao ni kusimama tu kwenye haki na ukweli. Na hivi vitu viwili nyinyi ndiyo hamvitaki! Nyinyi mnataka kusifiwa muda wote na kuhubiriwa kwa amani iliyofichwa kwenye koti la woga.
 
Unakumbuka mauaji ya kimbari yaliyotokea huko Rwanda mwaka 1994? Kanisa lilihusika kwa 99% kuchochea chuki kwa kisingizio cha haki na matokeo yake ni mauaji makubwa.
Ni muhimu kila mtanzania ailinde AMANI ya nchi yetu kwa wivu mkubwa.
Binafsi sio mfuasi wa chama chochote kile ila ni raia mzalendo wa Taifa langu Tanzania.
 
Muwe mnasoma historia ndugu zangu.

Chanzo kikuu cha mauaji ya Rwanda ni ukabila uliokuwa umekithiri kati ya Watusi na Wahutu! Ukabila huo ulisababisha kuuwawa kwa Rais Juvenal Habyarimana tarehe 6 Aprili, 1994! Baada ya ndege yake kutunguliwa na waasi wa Kitusi wa RPF wakiongozwa na akina Paul Kagame!

Baada ya kutokea kwa haya mauaji ya kiongozi mkuu wa nchi ndiyo machafuko yalianza kwa Wahutu walio wengi kuwashambulia Watusi wachache! Ni nani aliyekudanganya ya kwamba Kanisa Katoliki lilihusika kwa 99% kutokea kwa hayo mauaji ni nani?
 
Tusijisahaulishe kuwa viongozi wa Chadema wakishirikiana na washirika wao ndio walio chochea watu kuingia barabarani na kufanya fujo na hatimaye baadhi yao kupoteza maisha, isingekuwa chadema na washirika wao kuchochea huenda hata mtu mmoja asinge kufa.

Tufanye Chadema walichochea maandamano, na watu waitikia wakafanya maandamano au hata vurugu kama wengine wanavyoita...

Hivyo basi na tusisite kufanya kwamba CCM yenyewe ikamalizia kazi ya kutoa roho za hao walioandamana...

Jambo la kweli tunalolijua wote mimi na wewe ni kwamba Chadema hawamiliki silaha za kuweza kuua watu 500 na ushee kama ilivyotajwa...
 
Kwanza nashukuru kwakukiri kuwa yale hayakuwa maandamano bali ni fujo zilizo ambatana na uharibifu wa kuchoma moto, hao waandamanaji walikuwa na silaha mbalimbali za kuweza kujeruhi na hata kuuwa.....tulishuhudia kwa macho yetu....vituo vya polisi vilichomwa moto.....sasa kwa akili yako ulitegemea polisi wasitumie risasi katika mazingira hatari kama yale?! isingewezekana lazima risasi ihusike katika mazingira yale haikwepeki, pia vifo ni lazima havikwepeki.
Kwa fujo zile njia pekee ya kuzikabili ilikuwa risasi maana wale hawakuwa waandamanaji bali walikuwa wahalifu ambao walikuwa na lengo la kufanya maangamizi.
Chadema na washirika wao wanapaswa kufanya sala ya toba kwa kuwachuuza vijana.
 
Muwe mnasoma historia ndugu zangu.

Chanzo kikuu cha mauaji ya Rwanda ni ukabila uliokuwa umekithiri kati ya Watusi na Wahutu! Ukabila huo ulisababisha kuuwawa kwa Rais Juvenal Habyarimana tarehe 6 Aprili, 1994! Baada ya ndege yake kutunguliwa na waasi wa Kitusi wa RPF wakiongozwa na akina Paul Kagame!

Baada ya kutokea kwa haya mauaji ya kiongozi mkuu wa nchi ndiyo machafuko yalianza kwa Wahutu walio wengi kuwashambulia Watusi wachache! Ni nani aliyekudanganya ya kwamba Kanisa Katoliki lilihusika kwa 99% kutokea kwa hayo mauaji ni nani?
Nenda kasome vizuri Makala ya Mary Fertitta " When Priest Forgot About God"
Utaelewa vizuri jinsi Kanisa Catholic lilivyo chochea migawqnyiko ya kikabila jambo ambalo lilipelekea kuchochea ubaguzi na chuki katika jamii ya watu wa Rwanda.
Viongozi wetu wa kidini wanapaswa kuwa makini sana. Kamwe tusijaribu kuichezea Amani ya Taifa letu.
Matamko viongozi wa kidini ni hatari dana.
 
Nenda kasome vizuri Makala ya Mary Fertitta " When Priest Forgot About God"
Utaelewa vizuri jinsi Kanisa Catholic lilivyo chochea migawqnyiko ya kikabila jambo ambalo lilipelekea kuchochea ubaguzi na chuki katika jamii ya watu wa Rwanda.
Viongozi wetu wa kidini wanapaswa kuwa makini sana. Kamwe tusijaribu kuichezea Amani ya Taifa letu.
Mimi naongelea historia (chimbuko la hayo mauaji) wewe unaleta habari za makala ya Mary Fertitta ambayo inaongelea namna Kanisa lilivyo shiriki!! Kweli walimu wanaofundisha wanafunzi wanastahili pongezi.
 
Kwa fujo zile njia pekee ya kuzikabili ilikuwa risasi maana wale hawakuwa waandamanaji bali walikuwa wahalifu ambao walikuwa na lengo la kufanya maangamizi.

Kwa hiyo hizo risasi ilikuaje zikaua hadi watu waliokuwa majumbani mwao, zikajeruhi watoto wadogo walio chini ya umri wa miaka 16, zikaua mama wajawazito?
Risasi zikatumika Mbeya, Mwanza, Mara, Dar, Arusha na kwingineko in a very "coordinated practice" kana kwamba huko kote kiwango cha fujo kilikuwa kinalingana...

Ukiacha kutuliza watu waliokuwa wanaandamana huko mabarabarani, polisi wakaingia hadi kwenye mitaa ambayo hakukuwa hata na dalili za watu kuandamana wakifyatulia risasi kila wanayemuona, wanaingia nyumba hadi nyumba kupiga risasi na kukamata wengine (kuna watu walienda kuchukuliwa wakiwa wapo ndani polisi walikuwa wakiulizia vijana tu)....hii ilikuwa ni broadligh manslaughter kwa jina la kutuliza ghasia na wala sio kuneutralize nguvu ya wananchi

Halafu pili unajua kwamba kwa sheria ya JMT, polisi wakifyatua risasi za moto ni lazima wapate order toka juu?
Sasa ni nani aliyetoa order kwamba kwa hali iliyopo kila sehemu ya Tanzania askari wafyatue risasi za moto?
 
Back
Top Bottom