Lycaon pictus
JF-Expert Member
- Jan 31, 2021
- 9,189
- 16,128
Wakati wa ukomunisti, nchi za kikomunisti zilibana sana mipaka yake ili watu wasitoke. Ndiyo moja ya sababu ya ukuta wa Berlin. Ndiyo sababu hadi leo kutoka Korea kaskazini ni ngumu mno na hatari. Tanzania nayo kupindi cha ujamaa wetu ilikuwa hivyo.
Leo hii dunia ni kijiji, watu wanasambaa dunia kote na kusafiri. Lakini ajabu CCM bado wamekazania sera za kijamaa kubania watu kutoka nje. Kupata passport mpaka eti uwe na safari, useme lengo la kusafiri na urasimu mwingine wa kizamani na usio na mantiki.
Leo nchi haina ajira, vijana watoke labda wakatafute huko, uhamiaji wanamkwamisha kwa urasimu wao wa kizamani. Wamasai wanaenda nchi za nje kusuka na kuuza sendozi lakini wanaishi kama digidigi. Wangeonyesha kitambulisho cha taifa na kupewa passport zao shida ingekuwa wapi?
Nchi ingepata hasara gani? Nashauri CDM walichukue hili suala kwenye sera zao. Kupata passport na kutoka nchini hakupaswi kuwa anasa ya viongozi na matajiri.