CHADEMA naombeni mulichukue hili suala la urasimu kwenye uhamiaji na Passport

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2021
Posts
9,189
Reaction score
16,128
Wakati wa ukomunisti, nchi za kikomunisti zilibana sana mipaka yake ili watu wasitoke. Ndiyo moja ya sababu ya ukuta wa Berlin. Ndiyo sababu hadi leo kutoka Korea kaskazini ni ngumu mno na hatari. Tanzania nayo kupindi cha ujamaa wetu ilikuwa hivyo.

Leo hii dunia ni kijiji, watu wanasambaa dunia kote na kusafiri. Lakini ajabu CCM bado wamekazania sera za kijamaa kubania watu kutoka nje. Kupata passport mpaka eti uwe na safari, useme lengo la kusafiri na urasimu mwingine wa kizamani na usio na mantiki.

Leo nchi haina ajira, vijana watoke labda wakatafute huko, uhamiaji wanamkwamisha kwa urasimu wao wa kizamani. Wamasai wanaenda nchi za nje kusuka na kuuza sendozi lakini wanaishi kama digidigi. Wangeonyesha kitambulisho cha taifa na kupewa passport zao shida ingekuwa wapi?

Nchi ingepata hasara gani? Nashauri CDM walichukue hili suala kwenye sera zao. Kupata passport na kutoka nchini hakupaswi kuwa anasa ya viongozi na matajiri.
 

Chadema haina serikali
 
Nilipata passport yangu uhamiaji ndani ya week 2 za kumaliza kutuma maombi.

Walinipigia simu nifuate passport yangu.

Sijajua urasimu uko upande gani.

Sent from my CPH1819 using JamiiForums mobile app
 
Lengo lake Iingizwe kwenye Chadema Party Manifesto.
Lishaingizwa tayari kwenye Ilani ya tundulissu na Ali Mwalimu, ingawa hakutaja kwamba watoto wake na mke wake ni raia wa Marekani, Nji ya mabeberu. Kabla ya kupewa uraia wa huko, walienda shule siku tatu wakaapa kama ifuatavyo (hasa zingatia MWISHONI):

ANZA*
The Oath of Allegiance;
“I hereby declare, on oath, that I absolutely and entirely renounce and abjure all allegiance and fidelity to any foreign prince, potentate, state, or sovereignty, of whom or which I have heretofore been a subject or citizen; …that I will support and defend the Constitution and laws of the United States of America against all enemies, foreign and domestic; …that I will bear true faith and allegiance to the same; …that I will bear arms on behalf of the United States when required by the law; …that I will perform noncombatant service in the Armed Forces of the United States when required by laws.
SO HELP ME GOD
 
Nilipata passport yangu uhamiaji ndani ya week 2 za kumaliza kutuma maombi.

Walinipigia simu nifuate passport yangu.

Sijajua urasimu uko upande gani.

Sent from my CPH1819 using JamiiForums mobile app
Muda siyo tatizo. Tatizo ni vigezo. Hakuna haja ya kuwa na safari wala kuwa na sababu ya safari. Kuhitaji tu passport ni sababu tosha ya kupewa.
 
Tatizo ni uvivu wa kufikiria. Serikali inatarajia matokeo ya kitofauti kwa kufanya mambo Yale Yale iliyokuwa ikiyafanya kipindi cha ujamaa.

Kwa kipindi cha Ujamaa, ingeweza kuwa na mantiki, lakini kwa zama hizi kuzikumbatia hizo sera, ni "uwendawazimu" fulani hivi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…