Pre GE2025 CHADEMA nawapa angalizo: Msivurugane kwa safu ya uongozi uliopo, mtajuta!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Mkuu nimekusoma vizuri sana, Kwenye Uchaguzi huu Chadema iko makini mno, hakuna shida yoyote
 
Aende mpaka mwisho upi?
 
Kama Vita ya Sugu na mchungaji Msigwa inakigawa Chama ujue itakapofika kwa Ayatollah Mtuhuru na Jasiri TAL Chama kitapasuka Katikati kama Ikweta 🐼
Kwan kuna vita? Uchaguzi si kura atakayeshinda si anaungwa mkono kazi inaendelea? Mfalme Suleiman alipoulizwa unataka nikupe nn alimwambia Mungu nipe HEKIMA. Kwani ni lazima mng'ang'anie nafasi hiyo moja mpaka mparurane?. Rushwa tuwaachie CCM. Walimu wa shughuli hiyo. Chadema ndicho chama kilichobaki CCM wananchi wameshachoshwa na vitendo vyao na siasa zao za maigizo hata kwenye kumbukizi za viongozi wetu waliotangulia mbele ya haki wanageuza sehemu ya kutaja madarasa na madaraja yaliyojengwa siyo kumbukizi tena ya mhusika na alicholitendea taifa. Ni aibu Kwa Sasa kutapatapa kote Makonda kahamishiwa huku tabu ni CHADEMA. CCM hawalali mpaka kwenye kata zetu tunawaona wanavyohangaika na vikao kisa CDM. Kazeni Uzi, Shikilieni hapohapo wameshaelekea kibla.
 
Tujichunge na Mapandikizi ya Kinana na Mama Abduli naona lengo lao ni kuingiza Virus ili tuanze kutafunwa kuanzia ndani.
 
Mbowe na Sugu wamepewa hela na Mama Abdul ili watuvuruge, timua hao wala rushwa. Tunawataka wazalendo Lissu na Msigwa
 
Chadema hata mpewe kiburi na mabwana zenu wa Denmark hamuwezi kushinda uchaguzi wa rais,hamjitambui
 
Chama hiki kimejengwa kwenye misingi ya kikristu sisi tusio wakristu tunakiangalia kwa tahadhari kuu. Kina ubaguzi wa kiimani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…