CHADEMA nendeni na moja Kichwani

CHADEMA nendeni na moja Kichwani

Kuna sehemu nahisi CHADEMA hawaendi na moja Kichwani zile hesabu za darasa la pili, tatu, nne hadi la tano. Bahati mbaya mkiambiwa Ukweli huwa mnapiga kelele bila logic.

Hebu CHADEMA kwa unyenyekevu niwaombe mtumie logic bila kusahau hesabu za moja Kichwani. Moja ya jambo ninaloliona halina maana ni kelele za ushabiki wa baadhi ya wanachadema kupiga makelele mitandaoni ya Mzee Au waziri mkuu wa zamani ataka Katiba mpya.

Sidhani Kama Chenge, Sumaye au Msuya kusema Katiba Mpya ni sasa Kuna tija yeyote au ina maana yeyote ile. Badala yake CHADEMA naomba msitoke Kwenye reli ya kuweka mikakati ya kupata Katiba mpya.

Wale wazee walishastafu na walikuwa ngazi za juu serikalini walishindwa nini? Kutuletea hiyo Katiba Mpya, badala yake WANASEMA Leo. Naomba niwakumbushe CCM ni ile ile hutaki rejea uteuzi wa Kingai.
Chadema ilisha kufa zamani unapoteza mudawako bure hii katiba mbovu tuliyo nayo ikimpata kiongozi mzuri na mzalendo katiba inakuwa nzuri kwa sababu inampa nguvu zote huyo kiongozi ...kwa sasa ni kupigania tupate rais ambaye ni DICTATOR MZALENDO
 
Naunga mkono hoja ndiyo maana pamoja na kinachoitwa maridhiano wakati kinaendelea Chadema kupitia Bavicha wamekuwa wakiendelea na makongamano nchi nzima ya kuhamasisha na kutoa elimu juu ya Katiba Mpya.

Katika makongamano hayo sehemu nyingine wamekutana na ubabe wa Polisi na kufunguliwa kesi hiki kikiwa ni kiashiria kuwa maridhiano ni janja ya CCM kupoza moto wa Katiba Mpya lakini vijana bado wanaendelea kila kona ya nchi. CCM ni ile ile.
Chadema wao wametulia wanasubiria Kikosi Kazi kije na ripoti ndo wao wanze kuhamasisha wananchi na kampeni nchi nzima.
 
Back
Top Bottom