CHADEMA ni mti wenye maembe, lazima utupiwe mawe - Mbowe


Kuna watu haya maandishi mekundu hawataki kuyasoma na kuyatafakari, wao wanaona tuu kwa jicho moja hawataki kuona upande wa pili .well articulated.
 

- Mkuu Kieleweke, kwanza heshima yako mkuu sasa mkuu mbona umeruka mengi sana mpaka kufikia hapa, si ungeanza mwanzo kama kweli unataka kujadili haya, anyways hebu tujadili hoja yako,

- Unasema kwamba katiba ya Chadema, inaunda kundi la wazee as a kokasi ambayo inatambuliwa kikatiba na kupewa uwezo wa kumlazimisha au kumuomba mwanachama au kiongozi yoyote wa Chadema, kujitoa kwenye kinyang'anyiro chochote cha uongozi ndani ya chama, na tena kwa wakati wowote ule,

- Mkuu Kieleweke, unasema kwenye katiba ya Chadema kuna kipengele kinachoruhusu haya? Are you serious? au labda kiweke hicho kifungu hapa kutoka katiba ya Chadema mkuu, na kwa nini Mwenyekiti wa Chadema asitumie hicho kifungu kuwajibu critics kwenye mahojiano yake? Maaana angemaliza ubishi mara moja, wala tusingefika huku, infact bado anaweza kukiweka hapa tukaacha mara moja hii discussion.

Respect.

FMEs!
 

- Mkuu Orche, heshima yako ndugu yangu, unasema kwamba Mama Clinton, alichukua fomu ya urais, halafu kabla hajairudisha akaombwa na wazee wa Democratic Party kuirudisha fomu na kumuuunga mkono Obama, na akakubali eti unasema this is what happened? Halafu Mkuu Kieleweke, eti unasema haya ni maneno mazito sana, no wonder hili taifa linaendelea kurudi nyuma, ulikuwa una make a lot of sense ulipokuwa umenyamaza, kuliko hizi maneno!

- Chadema mnaposhindwa chaguzi huwa tunajiuliza kulikoni?, kwa majibu kama haya ndio unapata jawabu rahisi sana, kumbe hakuna tofauti na CCM!

- Unajua mnaharibu sana mnapojaribu kutumia uongo uongo wa kitoto kama wa CCM, kuhalalisha nonsense! Sometimes muwe mnalionea huruma kidogo hili taifa, hivi wananchi wa taifa hili watadanganywa mpaka lini?

Respect.

FMEs!
 
Mzee FMEs
Unajua mimi ni shabiki wako na sioni soo kusema hilo.
Lakini kwa hili la demokrasia ndani ya CHEDEMA napingana nawe.
Kusema wazee walimlazimisha Zitto unakosea maana hata Zitto mwenyewe hajawahi kujilazimisha akafanikiwa, sembuse kulazimishwa! We jaribu leo umlazimishe Zitto tuone kama atakukubalia.

Zitto alikubali ushauri, kwa maslahi ya chama, halii hii hutokea katika vyama vyote hata ndani ya CCM yetu. Kama huu ni mfano mbaya, si wa kwanza, tuendelee na maisha. Nijuavyo mimi CCM wamechukia kwa hatua ya Zitto na hiyo ni haki yao.
 
- Mkuu Orche, Mama Clinton aligombea urais as opposed na maneno yako, soma hapa chini infact kuna wakati hata alishinda kura za some of the states:-

 
 
Just joking: Kama CHADEMA ni mti wenye maembe, na lazima utupiwe mawe. Basi si vibaya tukakiita CHAMA CHA DEMOKRASIA ZA MAEMBE.
 
it is BB v/s fmes!

i hope ni mjadala wa kawaida tu,NO CONFLICTS OF INTERESTS btn the two parties
 
it is BB v/s fmes!

i hope ni mjadala wa kawaida tu,NO CONFLICTS OF INTERESTS btn the two parties

- Wala hakuna sababu mkuu just come out as you are, si unajua hapa kwangu ni mtakuja na mtasuuzika! ila tu stick kwenye hoja na sio viroja! Sasa labda useme hiyo conflict of interest maana ni wewe ndiye uliyeyaleta hayo?

Respect.

FMEs!
 
it is BB v/s fmes!

i hope ni mjadala wa kawaida tu,NO CONFLICTS OF INTERESTS btn the two parties

Kumbe ndivyo? Wengine tumekatazwa na nani?

Halafu hii conflict iko wapi? Mimi siioni hata moja.
 
Mwembe wa chadema upo ktk shamba la bibi wana ndugu ( Mtei Mbowe et al ) wanapopoa embe watakavyo!
 
- Mkuu Orche, Mama Clinton aligombea urais as opposed na maneno yako, soma hapa chini infact kuna wakati hata alishinda kura za some of the states:-

Kama sikosei hamna aliyesema mama Clinton hakugombea urais. Ulikuwa unafananishwa mchakato mzima wa uchaguzi wa Democrats na Chadema. Kwamba mama Clinton alikuwa ni mgombea mmojawapo mwenye ushawishi mkubwa na kwa kutaka kugombea MPAKA MWISHO chama kikawa kinapasuka kutokana na vijembe walivyokuwa wanatupiana. Obama alikuwa anashinda hivyo haikuwa busara chama kuendelea kuumizana wakati adui wao ni McCain. Zitto naye ana ushawishi mkubwa ndani ya chama chake. Kitendo cha kuchukua fomu kikaibua makundi yenye uhasama ambao haujawahi kutokea tena kwenye chaguzi za Chadema na baya zaidi ukichochewa kwa kiasi kikubwa na watu nje ya chama. Makundi haya yote mawili yakashindwa kudhibitiwa na Zitto, Mbowe na chama. Hivyo busara za wazee wa chama, ambao kikanuni wanapaswa kuchambua na kutoa ushauri kwa kamati kuu kuhusu wagombea, zikawatuma kumshawishi Zitto ajitoe. Ilikuwa ni tahadhari kwani suala la kampeni zinafanywaje ndani ya chama bado halijawekwa vizuri kwenye kanuni kwavile bado ni jambo jipya. Zitto nimjuavyo sio mtu anayekubali kuonewa. Kama angeona haki yake inadhulumiwa angekataa ushauri na kuendelea MPAKA MWISHO, ila naye alitumia busara zake na kwa maslahi ya chama akaamua kujitoa.
 
 
FMES kama nilivyosema hapo juu kilichokuwa kinafananishwa ni MCHAKATO MZIMA WA UCHAGUZI. Na mchakato huo unaanza kwa mgombea kuchukua fomu au kuonyesha nia yake ya kutaka kugombea. Zitto alichukua fomu hivyo alishaingia kwenye mchakato wa uchaguzi kama mgombea mtarajiwa kwa nafasi ya uenyekiti.

Vilevile kingine kilichokuwa kinafananishwa ni timing ya kujitoa ya Mama Clinton kwenye mchakato mzima. Angeendelea MPAKA MWISHO damage ingekuwa kubwa zaidi na hivyo ingekula kwao.
 
I love JF, lakini hapa ndio tunapotofautiana na wengi. Bwana Mbowe ameikwaza democrasia. Hakuna swala hata moja kwenye democrasia ambalo linasema kwamba kama mgombea mwingine atagombea na incumbent then anaweza kutishia usalama wa kichama. CHADEMA ni ya Watanzania, kwa nini wasiachwe waamue nani awe mwenyekiti wao? Instead ya kuimpose system ya kura ya ndio?

Bado naamini kwamba Mbowe ni tatizo ndani ya CHADEMA, na tupo wengi ambao tuna hari ya kujiunga na CHADEMA lakini Mbowe ni kikwazo sababu ya maono yake ya kisiasa.
 
Big up Mheshimiwa Mbowe.Una uelewa na upeoo mkubwa .Jamani naomba hiyo namba ya kuchangia CHADEMA tuanze au bado kuanza?
 

CHADEMA ni ya wanaCHADEMA. WanaCHADEMA wameamua nani awe mwenyekiti wao kwa kutumia mchakato walioamua wao wenyewe. Kama wewe unasubiri Mbowe atoke ndio ujiunge na chama ni bora uende kujiunga na vyama vingine. Wanaoitakia mema CHADEMA wanajiunga nayo na kuiboresha wakiwa ndani ya chama.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…