Ngongo
Platinum Member
- Sep 20, 2008
- 20,654
- 35,887
Heshima kwenu wanajamvi.
Mgombea uRais wa CCM ni Samia Suluhu Hassan.
CHADEMA mgombea wenu nafasi ya uRais ni nani?
Kila nikichanga karata zangu mgombea anayefaa kubeba heshima ya kukiwakilisha chama ni Tundu Lissu.
CHADEMA ni chama kikuu cha upinzani kimeshiriki chaguzi nyingi tangu enzi za Freeman Mbowe,Dr Willy Slaa, Edward Ngoyai Lowassa na Lissu.
Mheshimiwa Lissu katika uchaguzi uliopita aliibeba bendera ya CHADEMA katika level ya juu sana ingawa resources zilikuwa haba na structure ya tume ilikuwa mbovu kweli kweli.
Mara nyingi CHADEMA inakosea kusema eti Late Ngoyai alipata kura nyingi kuliko mgombea yoyote wa upinzani. Nina uhakika kama Lissu asingeporwa kura zake zilikuwa nyingi kuliko za Lowassa.
Kitendo cha kumweka mgombea mwingine tofauti na Lissu ambaye ana uwezo mkubwa wa kujenga hoja,uwezo mkubwa wa kupambana na CCM ni kukirejesha chama nyuma.
Nimeiona mikutano ya Mwenyekiti Freeman Mbowe kanda ya kaskazini.
Nimefuatilia mikutano ya Msigwa ambayo kwa kiasi kikubwa inalenga mashambulizi makubwa kwa Mheshimiwa Mbowe. Nadhani si bahati mbaya CCM wameshanusa uenda mgombea ni Mwenyekiti.
Nadhani ni haki Mwenyekiti kugombea lakini kama nafasi hiyo angeachiwa Mheshimiwa Lissu ambaye bado ni mgombea muhimu na anayeweza kukisaidia chama kwenda mbele zaidi.
Ngongo kwasasa Iringa.