CHADEMA operesheni zenu ni maigizo ya mafanikio ni Sangara tu

CHADEMA operesheni zenu ni maigizo ya mafanikio ni Sangara tu

kipara kipya

JF-Expert Member
Joined
May 2, 2016
Posts
18,833
Reaction score
23,276
Ukweli unauma lakini ni lazima muelezwe ili mjitathimini na muda mnaoupoteza katika hiyo misafara yenu ya kufuja pesa za wananchi maskini mnaowalazimisha kuwachangia mafuta.

Lazima mkubali operesheni yenu iliyokuwa na malengo na ikafanikiwa na ikavuna wanachama ni moja tu ile operesheni sangara,
iliyoratibiwa na mtu makini katika uongozi anayejua kuweka mikakati kujenga hoja na kustawisha chama, aliyekuwa hajali ruzuku kuendesha maisha yake.

Alikubali kujitoa yeye na mkewe na aliwapa nafasi kila kiongozi kutoa mchango wake; alijenga nidhamu na kuzuia unafiki na umangimeza.

Makamanda hizi operesheni nyingine ni za kupasua ngiri maji tu na kuuza sura msione aibu kurudi na kupata ushauri Dkt. Slaa bado yu hai atawapa ushauri bure.

Leo hii kazi ni kupiga picha na kuweka maelezo tunakula bata kidigitali. Ina maana hizo pesa wanazochanga watu wa kipato cha chini wenye mapenzi yao ndio za kula bata badala ya kuwasaidia mafuta.

Makamanda msipoteze muda kwa operesheni; wananchi wa sasa ni waelewa sana wanajua giza na mwanga.

Kama mmewafukuza mbona hamjibu rufaa zao.

Nawasalimu kwa jina la Jamhuri ya Muungano.
 
Nilidhan ni Mimi tu ndio siwaelewi hawa watu.

Watanzania wametulia wanampima mama Yao kuona analeta nini . Huu sio muda wa kuijenga CCM Wala CDM. ni muda wa kuijenga Tanzania.

Always vyama vya upinzan ni against serikali sasa why muanze ziara wakati serikali hata miezi mitatu haina? Nani atawasikiliza?
 
Nilidhan ni Mimi tu ndio siwaelewi hawa watu...
Unajiona umeongea point?

Serikali gani haina hata miezi mitatu? Hii ni serikali ya CCM ina zaidi ya miaka hamsini, sasa sijui hiyo miezi mitatu unayoizungumzia ni ipi?

Samia mwenyewe pamoja na asilimia 90 ya wasaidizi wake ana miaka sita akiwa sehemu muhimu ya serikali.
 
Nilidhan ni Mimi tu ndio siwaelewi hawa watu.

Watanzania wametulia wanampima mama Yao kuona analeta nini . Huu sio muda wa kuijenga CCM Wala CDM. ni muda wa kuijenga Tanzania.

Always vyama vya upinzan ni against serikali sasa why muanze ziara wakati serikali hata miezi mitatu haina? Nani atawasikiliza?
Wana matatizo hao!
 
Ukweli unauma lakini ni lazima muelezwe ili mjitathimini na muda mnaoupoteza katika hiyo misafara yenu ya kufuja pesa za wananchi maskini mnaowawalazimisha kuwachangia mafuta...
Ndio tatizo la kulala huku unawaza kesho niandike nini kuhusu Chadema badala ya kuwaza utapataje chakula.

"Kufeli" kwa hicho unachosema nilitarajia kiwe furaha kwako, sasa nashangaa kinakuuma! Meaning hazikufail bali zimekua za mafanikio makubwa sana otherwise ungekaa kimya
 
Hii ya sasa hivi na kwasababu tupo kwenye digital zaidi (kwa maana ya mitandao ya kijamii), hata kama mimi sio chadema ninahisi watafanikiwa sana kuiadvertise na kurudisha upinzani ule uliokuwepo wakati wa kampeni za tundu lisu. ccm wawe macho sana mdogomdogo ndio wanaenda hivyo na watajikuta mafuriko ambayo hata kuyazuia haiwezekani.
 
Ukweli unauma lakini ni lazima muelezwe ili mjitathimini na muda mnaoupoteza katika hiyo misafara yenu ya kufuja pesa za wananchi maskini mnaowawalazimisha kuwachangia mafuta...
Nyie hamhitaji kupoteza muda kwani mnajua ushindi ulipo linapokuja swala la uchaguzi/uchafuzi.
 
hii ya sasa hivi na kwasababu tupo kwenye digital zaidi (kwa maana ya mitandao ya kijamii), hata kama mimi sio chadema ninahisi watafanikiwa sana kuiadvertise na kurudisha upinzani ule uliokuwepo wakati wa kampeni za tundu lisu. ccm wawe macho sana mdogomdogo ndio wanaenda hivyo na watajikuta mafuriko ambayo hata kuyazuia haiwezekani.
Kila mmoja anaamini ndoto yake lakini sio ya kuota huku unatembea!
 
Hii operation ni ya kidigital zaidi wanachama wanavunwa popote alipo a ha ushamba
 
Ukweli unauma lakini ni lazima muelezwe ili mjitathimini na muda mnaoupoteza katika hiyo misafara yenu ya kufuja pesa za wananchi maskini mnaowawalazimisha kuwachangia mafuta...
Unahangaika kipara kipya . Wasipofanya lolote mnasema chama kimekufa. Wakifanya operations zao mnakereka.

Nyinyi fanyeni mambo yenu. Ya Cdm waachieni hata kama wanakosea. Mwehu wako alizuia kila kitu. Ili afaidi mwenyewe . Lakini Mungu si kipara kipya
 
Ukweli unauma lakini ni lazima muelezwe ili mjitathimini na muda mnaoupoteza katika hiyo misafara yenu ya kufuja pesa za wananchi maskini mnaowawalazimisha kuwachangia mafuta...
Kwa habari yako ni kwamba CHADEMA bado hawajaanza operations zozote hapo wanatest mitambo tu.
 
Mbinu za chama usichokipenda kama hazileti matunda unatakiwa kufurahi tena kwakujigalagaza..

Unions vipi ungana kwenye misafara yao use unapanga ratiba
 
Unahangaika kipara kipya . Wasipofanya lolote mnasema chama kimekufa. Wakifanya operations zao mnakereka.

Nyinyi fanyeni mambo yenu. Ya Cdm waachieni hata kama wanakosea. Mwehu wako alizuia kila kitu. Ili afaidi mwenyewe . Lakini Mungu si kipara kipya
Mimi nawaacha kwanini msitulie nanyi hamuingizi timu 2025!
 
Back
Top Bottom