CHADEMA pelekeni taarifa kwa Spika mubashara, mmeilinda vyema heshima ya chama chenu

Sababu yangu ni ujumbe unaobebwa na uamuzi huo: nidhamu kwanza, umaarufu baadaye. Wahusika walipaswa kujishusha kabla ya jana. Kusimama katika ubatili na kuutetea kumewaponza. Sasa wamevuna walichopanda.
Nimeelewa sana hoja yako mkuu.
 
Baada ya kugoma kwenda kwenye KK ya chama chao, bado walikuwa na mwaka mzima wa kurekebisha makosa yao, bahati mbaya wakadhani watapata uungwaji mkono kwa ule uhuni wao.

Hawa hawastahimili msamaha, kama mwaka mzima na zaidi waliokuwa bungeni hasakutambua makosa yao, inaonesha walivyo na viburi kwa kusimamia walichokiamini licha ya kwenda kinyume na maazimio ya chama chao.
 
Umesema vyema.
Lakini Kule kupigwa chenga za kwamba taarifa sinjapewa nk zilikuwa hila za spika yule muovu akishirikiana Kwa karibu na mwendazake.
Ila tahadhari ni muhimu hata hii spika iliyopo sii ya kuwekeza dhamana.
 
Mzee tupatupa unapoteaga sana.
 
Mkuu VUTA-NKUVUTE umemaliza mjadala juu ya hili. Umechambua vema.

Kazi iendelee.
 
Unatuambia Sisi ili iweje , et Tangu miaka ya 80 nilipomaliza chuo [emoji3]
Kwani umeona kuna tatizo gani katika maelezo yake? Siyo lazima kuandika kama huna cha kuandika.
 
Nawashauri CHADEMA, siku watakayopeleka taarifa ya kufukuzwa uanachama kwa akina Halima Mdee, walifanye jambo hilo mubashara. Hatutaki tena kumsikia Spika au Katibu wa Bunge akikana kupokea barua ya CHADEMA. Hatutaki kuona tena jambo hili linaendelea. Taarifa ipelekwe Bungeni; Spika awaondoe akina Halima Mdee Bungeni halafu CHADEMA waamue kupeleka Wabunge wengine wa viti maalum au la.
 
uko sawa mkuu ila hili la kupeleka wabunge wapya bado kuna ukakasi wa KUTAMBUA MATOKEO YA UCHAFUZI. cdm wakipeleka wabunge wapya ilhali inajulikana kuwa MATOKEO HAYAJAKUBALIKA .. itatambulika kuwa wameridhia kuwa uchaguzi ulikuwa huru na haki .. je hii iko sawa?
 
Mkuu kuna msemo wa kuwa kama humuwezi basi muunge mkono.

Cdm sasa inabidi tuingie kwenye siasa za kusikilizana ili tuweze kufanikisha malengo yetu.
 
Mkuu kuna msemo wa kuwa kama humuwezi basi muunge mkono.

Cdm sasa inabidi tuingie kwenye siasa za kusikilizana ili tuweze kufanikisha malengo yetu.
Kwahiyi CDM tunaingiza vifaa vipyaa mjengoni liwalonaliwe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…