Kwa mjibu wa matonyaji wangu wa karibu, Rafiki yangu wa siku nyingi sana tangu kuzaliwa CHADEMA wamendelea kujipima na kuona namna gani mugombea wao wa Urais amepokelewa na jamii ya watanzania. Kuna mabishano mengi Nyuma ya kapeti kwamba Mgombea wao anachuja mapema sana hata kabla CCM hawajapanda jukwaani.
Moja ya mijadala ni kuangalia jinsi Mugombea wao wa 2020 anavyoshuka chati ukilinganisha na Lowasa aliyekuwa anapanda chati siku hadi siku.
Kwenye mazungumuzo yetu ya simu (recorded ila natunza siri ya mtonyaji wangu) Rafiki huyu amenitonya kwamba sasa CDM wako tayari kuwaachia ACT Wazalendo majimbo yoyote watakayo yataka ili mradi Membe aongeze nguvu hili jahazi linalo zama.
Tangu Mgombea wao achaguliwe hakuna mwanasiasa yeyote maalufu kutoka chama chochote aliyejitokeza na kumuunga mkono tofauti na wafuasi walewale wakati wa Lowasa CCM kilimeguka na hii iliwapa nguvu CHADEMA .
Shida nyingine ni agenda/sera gani mgombea wao atatembea nayo wakati wa kampeni. Hapa ndipo penye shida pia maana CCM wamebeba agenda zote za maendeleo. CHADEMA sasa kimebaki na agenda ya uhuru wa nyombo vya habari na uhuru wa kujieleza.
Kuna shida pia iwapo CHADEMA kinataka kitembee na katiba mpya ambayo CCM wameachana nayo.. hii inawapa shida kidogo maana wakati wa bunge la katiba mpya CHADEMA walijitoa bungeni na kuwaacha CCM peke yao. Je, CCM wakitia doa hii sera itauzika?.
Inaonekana pia CHADEMA hawajafanya uchunguzi kupima nini haswa wananchi wanahitaji kwa sasa. Badala yake wamejikuta Mgombea akija na mahitaji yake binafsi ambayo hayawagusi watanzania hasa kundi la wapiga kura.
N.B. Mjumbe hauawi.