Katibu wa CHADEMA Kanda ya Pwani, Benjamin Ntele, akizungumza Julai 17, 2026, amesema kuwa mtu aliyejitambulisha hadharani kwa jina la Shaban Ally Mchezo na kudai kuwa ni Mwenyekiti wa CHADEMA Jimbo la Kibaha Vijijini si kiongozi halali wa chama.
Ntele amesema katika kuthibitisha hilo, amemleta mbele ya waandishi wa habari Shaban Ally Mchezo halali, ambaye amewasilisha uthibitisho wa utambulisho wake kupitia Kitambulisho cha Taifa (NIDA) na Kitambulisho cha Mpiga kura.
Akizungumza katika mkutano huo, Shaban Ally Mchezo amesema amekuwa akirubuniwa mara kadhaa ili akihujumu CHADEMA, lakini alikataa kufanya hivyo. Amesema baada ya kushindwa kumshawishi, ndipo alijitokeza mtu mwingine akitumia jina lake na kujitambulisha kuwa ndiye Mwenyekiti wa CHADEMA Jimbo la Kibaha Vijijini.