CHADEMA saidieni wananchi wa Nyatwali mahakamani kwa dhuluma wanayotendewa na Serikali

koryo1952

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2023
Posts
948
Reaction score
1,627
Wananchi wa Kata ya Nyatwali wapatao 15,800 wanahamishwa na Serikali kupisha ongezeko la Hifadhi ya Serengeti bila sababu za msingi.

Tayari makadirio ya fidia zao zimekwishakamilika bado tu malipo.

Wananchi walitishwa kwa kuweka saini zao kwenye majedwali ya fidia na hawakuwa na namna yeyote.

Wapi umeona hekari moja mtu analipwa Tshs 2 millioni wakati Kata ya Nyatwali iko kwenye Halmashauri ya Mji wa Bunda ambapo kwa sasa hekari moja ni Tshs.15 millioni.

Chonde chonde tunawaomba viongozi wa CHADEMA mtutetee Mahakamani dhidi ya dhuluma hii ya Serikali.
 
Speke Bay Lamadi zone ..Lissu amekiwasha Jana Bunda
 
Yaani hii tanzania kila sehemu ni hifadhi, karibia asilimia 80% ya ardhi tanzania ni maji na hifadhi. Know wonder 🤔 ajira zimekuwa ngumu mtaani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…