Mange Kimambi: "Mmetusaliti!" Awalipukia wanasiasa Baada ya Kukusanya "Tone Tone"

Mange Kimambi: "Mmetusaliti!" Awalipukia wanasiasa Baada ya Kukusanya "Tone Tone"

Jannatul Firdaus

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2026
Posts
446
Reaction score
1,113
Mwanaharakati wa mitandaoni, Mange Kimambi, amewajia juu wanasiasa na kueleza kusikitishwa kwake na hatua yao ya kubadili mwelekeo wa kisiasa baada ya kukusanya michango ya fedha kutoka kwa wananchi.

Kupitia ujumbe aliosambaza kwenye mitandao ya kijamii, Kimambi amedai kuwa wanasiasa hao wameanza kuhubiri amani, busara, na maridhiano na pande zilizohusika na matukio ya maafa ya Oktoba 29, badala ya kuendeleza msimamo wa mapambano kama walivyoahidi wakati wakipokea usaidizi huo.

Katika tamko lake, Kimambi ametaka kurejeshewa fedha hizo za michango, maarufu kama "tone tone" kwa niaba yake na kwa niaba ya wafuasi wake anaowaita keyboard warriors.

Amesisitiza kuwa michango hiyo ilitolewa kwa lengo la kuunga mkono mapambano ya haki, lakini sasa inatumiwa kueneza ujumbe wa upendo na uelewani na wale aliodai kuwa walisababisha maafa.

Alihitimisha mtazamo wake kwa kutoa onyo kali kwa umma akisema, "Aisee ogopa sana wanasiasa."
1789371533937.png
 
Kwa sasa wanachama wa Chadema wanawasikiliza zaidi Mange Kimambi na Sativa zaidi ya wanavyosikiliza viongozi wao.

Chama kuendeshwa na wanaharakati ni hatari sana , na imefikia hapo kwa sababu hao wanaharakati ndio walioshawishi watu wengi kukichangia chama kwa ajili ya Mkutano wa Kamati Kuu.

Hawa wanaharakati so called wao hawataki Maridhiano, hawataki kuona nchi inasogea hatua baada ya yale mauaji ya Oct 29, na ikumbukwe kua wao hawapo Tanzania.

Kuna upande wana hoja kua kama CCM inataka Maridhiano basi waliohusika na Mauaji ya Oct 29 wawajibishwe which is make sense lakini mimi naamini watawajibishwa, nchi haiwezi chukua maamuzi ya haraka namna hiyo wanavyotaka wao nchi iamue chap kama kutoa ushuzi au kupiga chafya, lazima kuwe na utaratibu. Na kuwajibishwa wahusika inatakiwa iwe ni agenda moja wapo ya maridhiano.

Pili Serikali iharakishe kesi ya Lisu iishe hii ni jambo lingine linakwamisha haya maridhiano, Majaji wale wanapofanya kesi kua ndefu ili wapate overtime na per dm wakumbuke pia nchi imesimama hii , tatu Serikali iwaachie vijana wote iliowakamata na kuwapa kesi zauongo , kesi za Ugaidi na zingine nchi nzima.

Haki itawale tuache hizi chuki za kike , nchi haiwezi kuendeshwa kwa kufuata mihemko ya Hormones , tufuate utawala wa HAKI NA SHERIA. Tusitese watu na kumwaga Damu Hovyo, nchi ita laaaniwa
 
Wauaji mnawewewseka sana.... Baada ya Pandikizi la Mbowe (Lema) kuwekwa wazi sasa naona mnakuja na Viroja......
Watanganyika tumegoma kuwasilikliza Wauaji...
 
Kwa sasa wanachama wa Chadema wanawasikiliza zaidi Mange Kimambi na Sativa zaidi ya wanavyosikiliza viongozi wao.
Kiongozi wa CDM kwasasa ni Makamu Mwenyiki wa CDM ambaye ni Heche... Huyo ndio Watanganyika na CDM wnamsikiliza...

Heche alishasema Hakuna Maridhano na Wauaji..... full stop and long Break..
 
Hawa wanaharakati so called wao hawataki Maridhiano, hawataki kuona nchi inasogea hatua baada ya yale mauaji ya Oct 29, na ikumbukwe kua wao hawapo Tanzania.
Ili Maridhiano Yafnayike yafutayo lazima yafanyike

1. Alliyetoa mari ya Kuua, Mpaka yule aliyevuta Trigger na Risasi ikatoka na kuuwa Watanganyika lazima wawajibishwe..
2. Maiti za Watanyika waliouwawa Oct 29 lazima zipatikane ili wazikwe kwa heshima.. wale sio Mbwa
3. Uchaguzi mkuu Urudiwe kwa kuwaSerikali yote ni Haramu.. Haikuchaguliwa
4. Katiba Mpya
5. Maridhiano

Bila hayo kamwe hakuna maridhiano na Wauaji
 
Pili Serikali iharakishe kesi ya Lisu iishe hii ni jambo lingine linakwamisha haya maridhiano
Waliouwawa ni Watangayika kwanini Lissu ndo Aridhienae...??

Kwani ni lazima CDM.. tumieni vyama vingine kama ACT, CHAUMA... Tumieni Taasisi kama BAKWATA NA KKKT Hao wanatosha...
 
Kwa sasa wanachama wa Chadema wanawasikiliza zaidi Mange Kimambi na Sativa zaidi ya wanavyosikiliza viongozi wao.
Chama kuendeshwa na wanaharakati ni hatari sana , na imefikia hapo kwa sababu hao wanaharakati ndio walioshawishi watu wengi kukichangia chama kwa ajili ya Mkutano wa Kamati Kuu.
Hawa wanaharakati so called wao hawataki Maridhiano, hawataki kuona nchi inasogea hatua baada ya yale mauaji ya Oct 29, na ikumbukwe kua wao hawapo Tanzania.
Kuna upande wana hoja kua kama CCM inataka Maridhiano basi waliohusika na Mauaji ya Oct 29 wawajibishwe which is make sense lakini mimi naamini watawajibishwa, nchi haiwezi chukua maamuzi ya haraka namna hiyo wanavyotaka wao nchi iamue chap kama kutoa ushuzi au kupiga chafya, lazima kuwe na utaratibu. Na kuwajibishwa wahusika inatakiwa iwe ni agenda moja wapo ya maridhiano.
Pili Serikali iharakishe kesi ya Lisu iishe hii ni jambo lingine linakwamisha haya maridhiano, Majaji wale wanapofanya kesi kua ndefu ili wapate overtime na per dm wakumbuke pia nchi imesimama hii , tatu Serikali iwaachie vijana wote iliowakamata na kuwapa kesi zauongo , kesi za Ugaidi na zingine nchi nzima.
Haki itawale tuache hizi chuki za kike , nchi haiwezi kuendeshwa kwa kufuata mihemko ya Hormones , tufuate utawala wa HAKI NA SHERIA. Tusitese watu na kumwaga Damu Hovyo, nchi ita laaaniwa

..inaelekea unakubaliana na hoja nyingi za Mange, na Sativa.

..halafu unawabeza na kuwalaumu Chadema kwa kukubaliana na hoja hizohizo.
 
Waliouwawa na Watangayika kwanini Lissu ndo Aridhienae...??

Kwani ni lazima CDM.. tumieni vyama vingine kama ACT, CHAUMA... Tumieni Taasisi kama BAKWATA NA KKKT Hao wanatosha...
Lissu ndio baba wa
 
ChatGPT Image Sep 17, 2026, 01_12_10 PM.png


Na Nulphin Charles, Katibu Mstaafu Kanda ya Serengeti

Mijadala katika mitandao ya kijamii imechukua sura mpya baada ya Mange Kimambi kutoa kauli za dharau kwa viongozi wa CHADEMA. Hii imefuatia kanusho lililotolewa na Katibu Mkuu wa CHADEMA Ndg. John Mnyika akiwaasa wana-CHADEMA kutomwamini Mange juu ya tuhuma alizozielekeza kwa GODBLESS LEMA na BONIFACE JACOB kuwa wamekuwa wakishiriki vikao vya siri na viongozi wa CCM na kupewa fedha.

Mange amesema ni yeye na baadhi ya wanaharakati ndio wenye ushawishi katika siasa za Tanzania na si CHADEMA. “Sisi wanaharakati ndio tulimsafisha Heche alipotuhumiwa kwa ufisadi na ni sisi tulioingiza watu barabarani, kuleta vurugu kwenye Uchaguzi Mkuu, na si CHADEMA. Sisi ma-Keyboard Warriors ndio wenye ushawishi, CHADEMA muelewe”

Kauli ya Mange inakinzana na nadharia ambayo viongozi wa CHADEMA wamekuwa wakiitangaza kuwa ni wao waliohamasisha vurugu kujaribu kuzuia uchaguzi mkuu wa mwaka 2025. Aidha, kauli ya Mange Kimambi inashabihiana na kauli ya mwanaharakati ROLANDA MALABA ambaye baada ya uchaguzi mkuu kwa bahati mbaya alivujisha taarifa za wanaharakati kulipwa na Ford Foundation fedha kiasi cha Dola Milioni mbili kwa ajili ya kuratibu uzuiaji wa uchaguzi.

Tambo na dharau za wanaharakati sasa zinathibitisha kuwa wameizidi CHADEMA nguvu na ushawish, jambo ambalo halina afya katika siasa za ushindani zinazohitaji uwepo wa taasisi imara badala ya sifa na umaarufu wa mtu mmoja mmoja.

Tambo za Mange hazijaishia kwa viongozi wa CHADEMA pekee; mapema wiki hii alitishia kuwajulisha Askari Uhamiaji wa Marekani kumrudisha Msanii ROMA Mkatoliki nchini baada ya msanii huyo kutoa mawazo yaliyotafsiriwa kukosoa dharau ya Mange kwa viongozi wa CHADEMA.
 
Kyoma we mambo ya Chadema umeyakomalia sana

Anyway

Unavyoona kina PATEL, ROSTAM AZIZ , YULE WA IRINGA wana nguvu CCM Ndivyo wanaharakati baadhi wana nguvu CHADEMA kisa kuwachangia pesa

Vyama vianze kujitegemea sasa
 
mapema wiki hii alitishia kuwajulisha Askari Uhamiaji wa Marekani kumrudisha Msanii ROMA Mkatoliki nchini baada ya msanii huyo kutoa mawazo yaliyotafsiriwa kukosoa dharau ya Mange kwa viongozi wa CHADEMA.
Kwani Roma mkatoliki kaua mtu. Akirudi anarudi kwa familia yake. Hakuna popote Roma Mkatoliki anatafutwa na Polisi kwamba kakimbia
 
Huyu nae ni kimama wa mwendokasi, hana uchungu kama anavyojitanabaisha, ana lake jambo nyuma ya pazia. Ogopa sana mtu ambaye anaamini yupo right all the time, tena kwa speculations with no vivid clarities. People need to re-examine her context instead of rushing to conclution.
 
Waliouwawa ni Watangayika kwanini Lissu ndo Aridhienae...??

Kwani ni lazima CDM.. tumieni vyama vingine kama ACT, CHAUMA... Tumieni Taasisi kama BAKWATA NA KKKT Hao wanatosha...

BAKWATA tena 😂😂 nilikua nimekuchukulia serious ulivyoweka bakwata nikacheka Lissu Ndo watanzania wana imani nae baada ya kuishi kwenye siasa za kilaghai na watu kujimilikisha na sisi kutuweka wananchi Bond na kukopa mikopo ulaya kuja kuwafaidisha wachache na kuweka mali bond Uchaguzi feki sasa hayo mambo lazima yafike mwisho wananchi wachague viongozi wanaowapenda wao
 
Benki ya dunia na IMF mwaka 2019 viliitangaza Tanzania kuingia uchumi wa kati baada ya maboresho makubwa ya kiuchumi yaliyofanywa na serikali ya awamu ya tano iliyokuwa ikiongozwa na hayati Magufuli na Makamu wake Samia.

Serikali ya awamu ya tano ilifikia hayo mafanikio ya kuingiza nchi uchumi wa kati baada ya kubana matumizi, kudhibiti ufisadi, kujenga viwanda na kuhimiza wananchi kuchapa kazi kwa nguvu zao zote.

Hali ilibadilika ghafla baada ya Rais Samia kuapishwa serikali yake ya awamu ya sita ikaacha kuhubiri viwanda wala wananchi wake kuchapa kazi na akatangaza sera mpya ya kula kulingana na urefu wa kamba yako! Matokeo yake ni kuuzwa kwa sekta muhimu za kuingizia nchi kipato kama bandari zote na makaa ya mawe.

Kutokana na kuzorota huku kwa usimamizi wa rasilimali za taifa Tanzania imeshushwa kutoka uchumi wa kati na sasa haieleweki iko uchumi gani! Hivyo Rais ajaye baada ya Samia atakuwa na kazi kubwa ya kubana matumizi, kudhibiti ufisadi serikali, kulinda rasilimali za taifa na kuirudisha nchi uchumi wa kati tena.

Kuna kila aina ya ushahidi kuwa Rais Samia amekata tamaa na haumizi kichwa tena kuhusiana na shida za watanzania ila inaonekana awamu yake hii ya pili alijipanga kula raha na kusafiri sana duniani ila mauwaji ya oktoba 29 yamempunguza speed baada ya kupigwa marufuku kusafiri ndani ya nchi za Ulaya.
 
Kyoma we mambo ya Chadema umeyakomalia sana

Anyway

Unavyoona kina PATEL, ROSTAM AZIZ , YULE WA IRINGA wana nguvu CCM Ndivyo wanaharakati baadhi wana nguvu CHADEMA kisa kuwachangia pesa

Vyama vianze kujitegemea sasa
Comrade Bado upo!?

Katika zama hizi za potea potea,tusipokuona humu tunahisi tayari!

Au una special mission somewhere!!?
 
Back
Top Bottom