CHADEMA shikilieni hapo hapo nyoka ameanza kutoa kichwa.

CHADEMA shikilieni hapo hapo nyoka ameanza kutoa kichwa.

Quinine

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2010
Posts
22,227
Reaction score
49,628
Maridhiano yalitaka kuwatoa kwenye reli ila kwa sasa naona mmerudi kwenye mstari wenu ulionyooka, tunaiona Chadema tuliyoizoea.

Hotuba ya jana imedhihirisha hilo, ni hotuba iliyojaa hofu iliyochanganyikana na hasira. Ametumia muda mwingi kuizungumzia Chadema kuliko kilichompeleka, ilionekana ajenda kuu ilikuwa Chadema.

Anasema anapenda kukosolewa wakati huo akiambiwa umekosea kuuza bandari anasema anatukanwa,, akiambiwa kauza Ngorongoro anasema matusi, akiambiwa tunataka katiba mpya anasema mnamtukana.

Nafikiri lugha wanayoitumia Chadema kwa sasa ndio inayotakiwa kwa siasa za Tanzania.ya leo.
 
Kuna member humu JF ameandika hii
..lakini iko blocked kwenye computer mode.
Namnukuu!

"Mtwara wapo wananchi walirudisha kadi za CCM Rais Samia akamla kichwa DC na DED wake tena akiwa kachukia hasa.

Mara vitendo hivyo vikashika kadi, Tanga kijiji kizima kuanzia mwenyekiti hadi mama wa nyumbani. Tena mwenyekiti wa kijiji akafikia kutamka wazi kuwa Andazi na CCM yeye anachagua Andazi.

Mama huku akijitafakari na CCM yake muziki ukaangukia Ngorongoro. Mama ya kadi za CCM zikatupwa utadhani uchafu unaokera kisa Chadema kuwafumbua macho wamaasai juu ya utu na tamaduni zao kuenziwa.

Sasa sio siri tena Mama huyu kapanic na amejua kuwa yale yaliyokuwa yanaogopwa na watangulizi wake ya CCM KUWAFIA MIKONONI yanaenda kutimia kwake.

Hotuba ya jana kuivaa Chadema ilikuwa mbovu kuliko maelezo na imemtoa relini lakini sababu kuu ni wimbi la KUTUPA KADI."

Mwisho wa kumnukuu!
Kazi iendelee!
Hatupwi.
 
Nyongo yooote ile ya jana ni wananchi kuikataa CCM hadharani,wamezoea kuiba kura gizani sasa huu muziki wa mikutano ya Chadema wananchi wanaikataa CCM mchana kweupe lazima nyongo ipande tu. Kinachoendelea kwenye mikutano ya Chadema kama siyo wizi wa kura unaoratibiwa na vyombo vya dola ndiyo reflection ya matakwa ya wananchi kwenye Sanduku la kura. Na hiki ndiyo kilimfanya yule dhalim aichukie Chadema na kupiga marufuku mikutano hii.
 
Maridhiano yalitaka kuwatoa kwenye reli ila kwa sasa naona mmerudi kwenye mstari wenu ulionyooka, tunaiona Chadema tuliyoizoea.

Hotuba ya jana imedhihirisha hilo, ni hotuba iliyojaa hofu iliyochanganyikana na hasira. Ametumia muda mwingi kuizungumzia Chadema kuliko kilichompeleka, ilionekana ajenda kuu ilikuwa Chadema.

Anasema anapenda kukosolewa wakati huo akiambiwa umekosea kuuza bandari anasema anatukanwa,, akiambiwa kauza Ngorongoro anasema matusi, akiambiwa tunataka katiba mpya anasema matusi.

Nafikiri lugha wanayoitumia Chadema kwa sasa ndio inayotakiwa kwa siasa za Tanzania.ya leo.
Atuwezi kuendelea na ujinga huo,nasi tulikua tunamshangaa mwenzetu badala ya kujenga hoja yeye ni matusi,Samoa mwizi,Samoa mjinga,Samoa mpuuzi ,Samoa mzanzibar ,Samoa kauza nchi nk.
Huu ushauri kaupeleke huko CUF
 
Hi
Honorable causa kinacho muuma zaidi ni kitendo Cha CDM kutofika katika mkutano, ukizingatia kulikuwa na wadau muhimu wa maendeleo,hivyo CDM walikuwa nguzo muhimu sana hasa katika taswira ya tasmini ya demokrasia nchini.
Hivi wazungu walikuwepo?Maana hao ndiyo kete yetu sisi.
 
Maridhiano yalitaka kuwatoa kwenye reli ila kwa sasa naona mmerudi kwenye mstari wenu ulionyooka, tunaiona Chadema tuliyoizoea.

Hotuba ya jana imedhihirisha hilo, ni hotuba iliyojaa hofu iliyochanganyikana na hasira. Ametumia muda mwingi kuizungumzia Chadema kuliko kilichompeleka, ilionekana ajenda kuu ilikuwa Chadema.

Anasema anapenda kukosolewa wakati huo akiambiwa umekosea kuuza bandari anasema anatukanwa,, akiambiwa kauza Ngorongoro anasema matusi, akiambiwa tunataka katiba mpya anasema matusi.

Nafikiri lugha wanayoitumia Chadema kwa sasa ndio inayotakiwa kwa siasa za Tanzania.ya leo.
CHADEMA hawajawahi niangusha
 
Back
Top Bottom