Uchaguzi 2020 CHADEMA siku zimeisha zingatieni yafuatayo ili muwe salama kuanzia sasa

Uchaguzi 2020 CHADEMA siku zimeisha zingatieni yafuatayo ili muwe salama kuanzia sasa

Mung Chris

JF-Expert Member
Joined
Sep 12, 2017
Posts
3,391
Reaction score
3,849
1. Msifanye Kampeni ambapo hamna vibali
2. Zungumzieni Ilani mwanzo mwisho
3. Acheni na maneno ya kusikia, zungumzieni mnacho kiamini
4. Msizidishe muda wa Kampeni
5. Msimzungumzie mtu au mgombea yeyote, muacheni na madhaifu yake wananchi wanayajua na yamewachosha
6. Heshimuni waliopo kweye vyeo na wanao waongoza
7. Ripotini kwa muda na kwa wakati maovu na makosa ya kuto fuata sheria, hili muhimu sana muwe na team kwa ajili ya kazi hii
8. Fanyeni Kampeni kwa weledi na hakikisheni kila mtu anafikiwa na kueleweka na watu wanao waamini,
9. Hamasisheni watu zaidi kwenda kupiga kura zaidi ya siku za nyuma.

EH MUNGU IBARIKI TANZANIA
 
Nakuunga mkono kwa yote isipokuwa pointi namba 5

Lazima wamseme mgombea wa CCM na madhaifu yake ili kuwakumbusha wananchi kuwa wakimchagua tena huenda akaendeleza madhaifu hayo hayo yaliyowaumiza wananchi katika miaka hii mitano iliyopita
 
Hawawezi kukuelewa hawa, chochote kinachotoka twetter wanakiamini na watakishadadia tu. Kifungo kingine kinakuja
 
Namba 9 ndiyo muhimu sana, maana hadi jana CCM inaushindi wa 89%
 
 
Mkuu, ukitaka kumuuwa mbwa ni lazima umpe jina baya. Sasa kama huyu tuliyenaye ana majina mengi tena na mabaya tayari ndani ya mioyo, na hata mbele za macho ya mamilioni ya Watanzania, ni lazima azidi kutambulishwa kwa majina yake halisi.
 
10. Maombi maalumu yafanyike ili Aron Kagurumjuli asisababishe kifo cha "Akwilina" mwingine asiye na hatia!
 
Hawawezi kukuelewa hawa, chochote kinachotoka twetter wanakiamini na watakishadadia tu. Kifungo kingine kinakuja
Kwa sababu mbeleko zipo na no moja ya mbinu yenu ya kisayansi ya kupora ushindi Basi andaeni kifungo,Ila mjiandae kwa matokeo yake. Sisi tunaweka tu kumbukumbu kwa maandalizi ya Yale yatakayo jiri.
 
Hiyo haiwezekani kwa nchi hii tz labda wamsifu jiwe ndio wataambiwa wanafuata sheria.
 
Suala la mawakala ni muhimu. Jambo jingine ni hili la kukatika katika kwa umeme. Si jambo lililozoeleka kwa siku za hivi karibuni. Nahisi kama naandaliwa kisaikolojia ili nisishangae nchi itakapokuwa gizani jioni na usiku wote wa tarehe 28/10/2020. Tahadhari. Mawakala wote nchi nzima wapatiwe taa za solar au za kichina za betri.

Na pia wazichunge maana kuna uwezekano mkubwa wa kuzikwapua. Kukiisha kuwa giza biashara ya kituo hicho kisicho na tahadhari hiyo kitakuwa Kimekwishilia mbali! Msiruhusu giza hata sekunde. One mistake one goal. Enzi zetu tulikuwa na maboksi yenye kura bandia, kinachofanyika ni *zima taa* badilisha box* washa taa. Mkija kwenye hesabu Mtakuta mmepewa kura utadhani wajumbe wamewapatia!

Niwakumbushe pia kwamba kutekana hakujaisha. Mawakala watatekwa, watanyang'anywa barua za utambulisho, n.k. isitokee wakala aliyempa, akapewa barua ya utambulisho eti yuko pekeyake mtaani, kaa vikundi, siku za kuvumilia si nyingi.

Kila la heri, Mwenyezi Mungu awatangulie!
 
Chama kina watu viburi

Anyway mioyo yao iendelee kuwa migumu kama wa farao, wapate pigo kubwa zaidi
 
Suala la mawakala ni muhimu. Jambo jingine ni hili la kukatika katika kwa umeme. Si jambo lililozoeleka kwa siku za hivi karibuni. Nahisi kama naandaliwa kisaikolojia ili nisishangae nchi itakapokuwa gizani jioni na usiku wote wa tarehe 28/10/2020. Tahadhari. Mawakala wote nchi nzima wapatiwe taa za solar au za kichina za betri. Na pia wazichunge maana kuna uwezekano mkubwa wa kuzikwapua. Kukiisha kuwa giza biashara ya kituo hicho kisicho na tahadhari hiyo kitakuwa Kimekwishilia mbali! Msiruhusu giza hata sekunde. One mistake one goal. Enzi zetu tulikuwa na maboksi yenye kura bandia, kinachofanyika ni *zima taa* badilisha box* washa taa. Mkija kwenye hesabu Mtakuta mmepewa kura utadhani wajumbe wamewapatia!
Niwakumbushe pia kwamba kutekana hakujaisha. Mawakala watatekwa, watanyang'anywa barua za utambulisho, n.k. isitokee wakala aliyempa, akapewa barua ya utambulisho eti yuko pekeyake mtaani, kaa vikundi, siku za kuvumilia si nyingi.

Kila la heri, Mwenyezi Mungu awatangulie!
Mwanajukwaa mzalendo wa kweli Ana Mambo ya muhimu wapenda haki wote najua mtakuwa mmemwelewa.Tafadhali ujumbe huu ufike kwa mawakala wore was vyama vyote,hii ni kwa maslahi mapana ya taifa letu. Tanzania ni yetu sote. Tuzidi kukumbushana.
 
Back
Top Bottom