KwetuKwanza
Member
- Mar 13, 2023
- 82
- 150
Pazia la kuchukua fomu za kugombea nafasi mbalimbali katika uchaguzi wa serikali za mitaa ambao utafanyika mwaka huu 2024 limefunguliwa Jana Oktoba 26, 2024 kwa mujibu wa TAMISEMI.
Zoezi hilo ambalo litafanyika kwa siku Saba, Hadi Novemba 1, 2024, litaambana na kurudisha fomu kwa wagombea mbalimbali.
Nafasi zinazowaniwa ni Mwenyekiti wa Kijiji, kitongoji, mtaa pamoja na wajumbe wa serikali za vijiji, na Miata.
Zoezi hilo linafanyika katika Ofisi za wasimamizi wasaidizi ngazi ya Kata na vijiji, ambapo wagombea mbalimbali walioteuliwa na vyama ndiyo wanaendelea kuchukua fomu hizo.
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) katika Wilaya ya Bariadi, kimekuwa Chama cha kwanza kwa wagombea wake kuchukua fomu hizo.
Katika Kata ya Malambo iliyoko Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Viongozi wa Chama hicho Wilaya wakiwa na wafuasi wao, wamewasindikiza wagombea katika uchaguzi huo kata ya Malambo kwenye kuchukua fomu ofsi za Kata hiyo.
Mamia ya wanachama hao, wakiwa na bendera, pikipiki, walifunga kwa muda mitaa ya Mji wa Bariadi, wakiwasindikiza wagombea wao kwenye kuchukua fomu hizo.
Zoezi la kuchukua fomu lilimalizika Salama, na wagombea hao wakaridhishwa jinsi walivyopokelewa na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi huo Kisha kuwahudumia na kuwapatia fomu hizo.
Mgombea nafasi ya Mwenyekiti wa mtaa wa Ngashanda amesema wamejipanga kuhakikisha fomu hizo zinajazwa mapema iwezekanavyo na kwa usahihi Kisha kuzirejesha.
Wamewaomba wasimamizi wa uchaguzi huo kutenda haki katika kuteua wagombea, lakini pia kutenda haki katika zoezi la kupiga kura ili wananchi waweze kuchagua viongozi wanaowataka.
Mwenyekiti wa Chadema Wilaya, Martine Mogani, amesema kuwa mitaa yote na vijiji katika Wilaya hiyo, tayari wameweka wagombea na wote wameanza kuchukua fomu.
Soma Pia:
Nimekuwekea video hapo chini kwa hisani ya Global tv.
Chanzo: Global tv.

- Waziri Mchengerwa atangaza tarehe ya kuchukua na kurudisha Fomu za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, siku zaongezwa
- Waziri Mchengerwa: Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Bara utafanyika 27 November, 2024
- CHADEMA yakanusha kujitoa kushiriki uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa Mwaka 2024