tonicimmobility
JF-Expert Member
- Jun 17, 2025
- 493
- 1,040
Viongozi na makada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wilayani Nzega, Tabora, wamefanya maadhimisho ya Mashujaa Day kwa kuwakumbuka na kuwaenzi wanachama na viongozi wa chama hicho waliopoteza maisha wakiwa katika mapambano ya haki na demokrasia nchini.
Soma pia: Makalla: CCM isihushishwe na vurugu zilizotokea Tabora kwenye mkutano wa CHADEMA
Shughuli hiyo iliyofanyika Septemba 7, 2025 ilihusisha ziara maalum na utoaji wa rambirambi katika familia ya marehemu Batromeyo Edward, aliyekuwa kada wa CHADEMA aliyeuawa kwa kupigwa risasi mwaka 2014 wakati wa kupigania matokeo ya uchaguzi wa serikali za mitaa.
Akizungumza katika tukio hilo, Katibu wa CHADEMA Mkoa wa Tabora, Yohana Lulyeho, amewaasa viongozi na makada wa chama hicho kuendelea kusimama imara katika mapambano ya haki na demokrasia.
Kwa upande wake, Mchungaji wa Kanisa la Afrika Inland Church Tanzania (AICT), Richard Edward, amewahimiza viongozi wa CHADEMA kuendelea kuwa wavumilivu licha ya changamoto zinazowakabili, akisisitiza umuhimu wa kumtegemea Mungu kwa kuwa ndiye mwenye hatima ya maisha na mapambano yao.
Naye Fabian Edward, kaka wa marehemu Batromeyo, ameishukuru CHADEMA kwa kuendelea kuwa karibu na familia hiyo, akisema kuwa rambirambi walizopokea zitasaidia kuendeleza ustawi wa familia iliyoachwa na mdogo wake.