Uchaguzi 2020 CHADEMA Taifa fuatilieni haraka tatizo la mgombea Ubunge Kibamba

Uchaguzi 2020 CHADEMA Taifa fuatilieni haraka tatizo la mgombea Ubunge Kibamba

Sir John Roberts

JF-Expert Member
Joined
Mar 1, 2017
Posts
12,835
Reaction score
23,584
Nimemsikilia kwa makini Mkurugenzi wa manispaa ya Ubungo akielezea tatizo la mgombea wa CHADEMA aliyechukua fomu na ambae viongozi wa CHADEMA wamesema hawamtambui.

Mkurugenzi ni wazi kasimama kwenye taratibu za uchaguzi na sheria kama inavyomtaka, sasa kwa ushauri wangu wa mapema hili suala lifikisheni haraka sana Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa sababu mkurugenzi haelewi la kufanya maana kama ni kuingizwa mjini na CCM tayari limeshafanyika.

Katibu Mkuu John Mnyika na viongozi wengine wa kitaifa jimbo la Kibamba ni ngome ya CHADEMA tafadhali msifanye mzaha mtalipoteza.
 
Mnaenda kubishana na mkurugenzi ofisini badala ya kuanza kupambana na huyo muhuni. Hapo Mkurugenzi keshabugi step either kwa kukusudia au kateleza.muhimu anzeni kufuatilia tume ya taifa ya uchaguzi litolewe ufafanuzi hili Mkurugenzi hataliweza huyo mama.
 
Ila mi bado sielewi,majina ya wanaogombea si huwa yanaenda Tume? Sasa mkurugenzi hakupewa nakala toka Tume?
Ndio maana tunasema chadema taifa waende hukohuko tume ya taifa ya uchaguzi. CCM wana mbinu za kishamba sana
 
Wafanye mawili:
1. Kwenda mahakamani kuweka zuio la kufanyika uchaguzi jimbo la Kibamba mpaka ufumbuzi upatikane
2. Kufatilia NEC.....
Tena wachangamke haraka sana.ccm inasubiri tarehe 25 saa 10 jioni kama hakuna pingamizi wanampitisha huyo mamluki wao.
 
Mnaenda kubishana na mkurugenzi ofisini badala ya kuanza kupambana na huyo muhuni. Hapo Mkurugenzi keshabugi step either kwa kukusudia au kateleza.muhimu anzeni kufuatilia tume ya taifa ya uchaguzi litolewe ufafanuzi hili Mkurugenzi hataliweza huyo mama.
Na pia waanze kumkataa huyu msimamizi mapema. Huyu ni hatari kuliko Covid 19
 
Wasiende polisi kwani kwenye uhuni kama huu polisi waga ni wahusika wakuu kiuzoefu.

Sijui tu wafanye nini kwani tume, polisi ni wale wale labda wajaribu kwa hiyo tume ilishindikana itabidi wamuunge mkono mgombea wa Act-wazalendo kwani hayo inaonekana yaliishapangwa kitambo na kibaya zaidi, Chadema siku hizi inaonekana intelligence iliishakufa.. very sad indeed.
 
Mbona NEC imenyamaza, au haijasikia kuwa kuna tatizo? Ifahamike kwamba huyu Mkurugenzi ni Wakala wa NEC kwa hiyo ni wajibu wa NEC kutoa tamko.
NEC inatakiwa kutatua mgogoro huu haraka iwezekanavyo
 
Back
Top Bottom