Uchaguzi 2020 CHADEMA tujitofautishe na vyama vingine, michango iwekwe hadharani

Uchaguzi 2020 CHADEMA tujitofautishe na vyama vingine, michango iwekwe hadharani

Countrywide

JF-Expert Member
Joined
Mar 2, 2015
Posts
20,694
Reaction score
32,527
Habari za muda huu ndugu wana JF, napenda kuwashirikisha jambo moja ambalo kwa undani wake naona linatatiza watu wengi.

CHADEMA kupitia mgombea wetu uraisi imeweka wazi kuwa pesa hakuna na hivyo ni jukumu letu wapenda mabadiliko na wananchi kwa ujumla tukawachangia pesa ili waweze kufanya kampeni vizuri na kwa wakati.

Kuomba michango sio jambo baya ila ubaya unaweza kuja namna ya kuomba michango na matumizi yake yatakavyokuwa.

Zimepita siku 5 sasa tangu watu waanze kuchanga(wenye moyo wa kuchanga), ila kwa bahati mbaya kabisa hakuna update yoyoye kutoka chamani.

Chama kinatakiwa kiweke utaratibu ambao utaongeza uwazi wa michango na kuwapa watu ari zaidi ya kuendelea kuwachangia.
Hapa chama kinatakiwa kujitofautisha na vyama vingine ambaye haviendeshwi ki-taasisi.

Chadema inatakiwa kutoa updates za michango kila baada ya siku 3 hadi 5, juu ya ni kiasi gani kimechangwa na kinatumikaje. Hii ni nzuri kwa maana wananchi wanaochanga watajua malengo yamefikia wapi na kama bado waendelee kuchanga kwa kiasi gani kufikia malengo.

Hili ka kutoa updates naweza kusema ni la lazima kwa maana wanaochangia wanapaswa kujua kinachoendelea juu ya walichochangia, tusiwabeze.

Mwisho lakini sio kwa umuhimu, nimeshangazwa na michango inayoombwa kutoka kwa Pambalu-mwenyekiti wa BAVICHA Taifa na kutoka kwa Mrema, Mkurugenzi wa Mawasiliano na Masuala ya Nje.

Hawa ni watu ambao kwa namna yoyote ile wanapaswa kuwa supported na chama, hivyo sidhani kama inaleta picha nzuri kwa watu wengine kwa maana mtu anaweza jiuliza kampeni za jimboni mbona si za kuhitaji nguvu kubwa ya kipesa kwa namna hiyo? Za mgombea uraisi ni sahihi kwa maana ni nchi nzima na pia kwa maana ya ukubwa wa taaisisi ya uraisi.

Nawasilisha.
 
IMG_4472.png

Wewe si umegoma kuchanga unawashwa na nini tena!?

Ila wewe jamaa kama sio lumumba buku 7 [emoji3][emoji3] basi utakuwa na matatizo ya akili, au pengine umenyimwa utunza hazina huko chamani.

Wiki nzima wewe unakomaa na mada za michango tu!
 
View attachment 1555344

Nakushukuru sana kwa kumjibu kwa hiyo michango yake! Kuna coment zake nyingi sana za kujaribu kubeza michango ya CHADEMA! Umemjibu vizuri sana, lakini wote tunajua hataelewa, huyu labda akutane na Adamu ampige mtama wa Mbasha ndo apate akili!
 
Mimi sitachanga ila ni wajibu wangu kuwakumbusha chama kutoa mchanganuo wa pesa zinazochangwa ili wachangiaje waeze kupata muamko
 
Nakushukuru sana kwa kumjibu kwa hiyo michango yake! Kuna coment zake nyingi sana za kujaribu kubeza michango ya CHADEMA! Umemjibu vizuri sana, lakini wote tunajua hataelewa, huyu labda akutane na Adamu ampige mtama wa Mbasha ndo apate akili!
Kuchanga bila kujua ulichochanga kinatumikaje ni ujinga sana
 
Back
Top Bottom