SSH Anawajibika
New Member
- Nov 9, 2024
- 3
- -3
CHADEMA tumejikaanga wenyewe wagombea wetu kuenguliwa katika Kinyang’anyilo cha serikali za Mitaa
Na Amosi Kagilwa, Kanda ya Pwani.
Vilio na kwiki vimetawala leo kila kona ya nchi kutoka kwa viongozi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo( CHADEMA) na wagombea wao kwa Kuenguliwa katika kinyanganyilo cha kuteuliwa kugombea nafasi mbalimbali za katika uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika Novemba 27 mwaka.
Mimi kama mwanachama kindakindaki wa CHADEMA kanda ya Pwani nimekaa na kutafakari nikaona sisi tumejikaanga wenyewe, tumekurupuka na kupeleka wagombea bila maandalizi kama walivyo wenzentu wa CCM na vyama vingine vyenye usajili wa kudumu.
Baada ya kutoa machozi ya damu nikaona katika machungu niliyonayo nitoe sababu zilizotufanya CHADEMA tukapoteza wagombea wengi katika uchaguzi wa mwaka huu.
Maandalizi duni
Chama cha siasa chochote uanza maandalizi ya uchaguzi baada ya uchaguzi kuisha. Chama chetu baada ya kususa uchaguzi wa serikali za mitaa wa mwaka 2019 hapakuwa tena na maandalizi tena ya uchaguzi wa mwaka 2024 kama wenzentu wa vyama vingine walivyofanya. Matokeo yake tumekurupuka kama guta lililokatika breki kwenye mteremko na kuingiza wagombea hata ambao kusoma hawajui na hawakuwahi kupewa semina yoyote ya kujaza fomu wakaandika makorokocho matokea yake idadi kubwa nchi nzima imekosa sifa na kuenguliwa.
adaa ya madai ya katiba mpya
Viongozi wetu wamekuwa wanatuaminisha kuwa hatutaingia ktk uchaguzi wowote bila katiba mpya. Matokeo yake sisi wanachama tulisubiri katiba mpya. Tulishangaa kuambiwa tuchukue fomu tugombee tusisubiri katiba mpya. Sasa kuhama kutoka mawazo ya katiba mpya hadi kuchukua fomu bila katiba mpya viongozi wengi tuliona tuchukue fomu kuridhisha viongozi ila hatukujiangaisha kujaza fomu kwa umakini uliotakiwa. Matokeo yake leo vimekuwa vilio vya kimbuga cha sunami.
Kusimamisha wagombea walevi
Kwa kuwa chama kilijikita katika adaa mbalimbali, hakikuchuja wagombea matokeo yake walevi na wavuta bangi wakachukua fomu. Kati ya hawa kuna waliozipoteza njiani, wengine kuzitupa katika vilabu vya pombe na wengine kupata nazo ajali wakiwa walevi na kufa nazo. Matokeo yake wengi wao hawakurudisha fomu na idadi yao kupungua. Kundi hili halikurudisha fomu lilipotea nazo.
Hapakuwa na semina
Ukosefu wa semina katika mchakato wa wote wa serikali za mitaa umeathiri kwa kiwango kikubwa wagombea wengi wa CHADEMA kutemwa. Wakati vyama vingine vikiwa na jukumu la kuelimisha wanachama wake jinsi fomu za uongozi, chama changu cha CHADEMA na viongozi wangu wamekuwa busy kusafiri nje ya nchi, kuhubiri chuki na kuitisha maandamano yasiyo na ukomo. Huu niliona ni udwanzi uliopitiliza yaani tumekuwa “busy for nothing.” Kwenye hili tujiulumu sisi wenyewe na viongozi wetu.
Nini Kifanyike
Pamoja na Waziri wa TAMISEMI Mohamed Mchengelwa kutoa rai wale wasioridhika kukata rufaa nashauri viongozi wetu tuwaambie wanachama wetu kutofanya hivyo kwani tulijaza fomu vibaya, tuliandika makorokocho na tunaenda kuhaibika zaidi.
Kuteleza sio kuanguka nashauri tuanze maandalizi ya uchaguzi mwingine wa mwaka 2028 ili tuioneshe Tanzania kuwa mwaka 2024 tumepuyanga na kuyakanyaga wenyewe.
Onyo la Jeshi la Polisi
Tangu jana viongozi wa CHADEMA wamesikika katika mikutano mbalimbali wakiwaambia wananchi kuwa kama serikali inataka uchaguzi CHADEMA kitawasaidia kama hakitaki uchaguzi uchaguzi CHADEMA itaingiza wanachama barabarani. Mimi kama mwanachadema nawaaasa wanachama wenzangu tusigeuke kafara tukapigwa na polisi barabarani. Tutii sheria bila shuruti tusiende kwenye maandamano ambayo hatuna tunachokipigania.
Makamu Mwenyekiti wa Chama
Wanachama wenzangu tutii agizo la polisi tusiandamane kwa sababu kama Makamu Mwenyekiti wa Chama Tundu Lissu hakujiandikisha tunaandamana ili iweje. Yeye awe wa kwanza kuandamana tuone kama atakuwa sahihi. Tusiwe chambo cha vurugu wakati tumeharibu wenyewe.