Countrywide
JF-Expert Member
- Mar 2, 2015
- 20,694
- 32,527
People'ssss powerrrr......!
Habari za jioni ndugu zangu wana JF, leo nijikite na kilichotokea Muheza.
Tunakumbuka vizuri sana kuwa mgombea wetu wa ubunge jimbo la Muheza awali alienguliwa na tume ya uchaguzi lakini siku mbili zilizopita tume walirudisha jina lake.
Mwanadada Yosepher Komba, aliahidi kupambana kufa na kupona ili watu wa Muheza waweze kupata mabadiliko wanayohitaji. Na kukaibuka kundi flani mtandaoni wakijinasibu kutumia kila aina ya ushawishi na nguvu ili mwanadada huyu aweze kushinda(ni jambo zuri).
Cha kushangaza ni siku ya leo ambapo Salum Mwalimu alipoenda kufungua kampeni kakutana na uwanja mtupu (watu ni wachache sana).
Ni jambo ambalo sisi kama wanachama na mashabiki wa CHADEMA limetufedhehesha sana, ni kitu hatukutegemea na tumebaki tunajiuliza "tumeikosea nini Muheza"??
Lakini ninaomba tuvute subra, tumtie nguvu mgombea ubunge ili aweze kuwa na hoja na mvuto kwa wapiga kura.
Mimi na-declare interest kuwa ni shabiki wa CHADEMA na hivyo nafuatilia kwa makini kwa kila kinachoendelea kuhusu kampeni za chama chetu. Ila leo cha kushangaza kwenye account ya CHADEMA Tanzania walikuwa wanapost nusu picha(picha imekatwa haionyeshi hadhira) hapohapo machale yakanicheza na kuona kuna tatizo huko kwenye kampeni, fasta nikaongea na mtu aliyepo huko anitumie picha za mkutanoni, nilichokiona ni aibu.
Chini hapa ni hali ilivyokuwa kwenye kampeni Muheza.